Kuichagua tena CCM, Je ni kielelezo cha kufanya informed decision, au ni Ignorance?


Tupo pamoja.Na pia atuambie kwenye zile bilioni 262 alikatiwa ngapi???Kwenye nyumba za serikali je??Kivuko/meli ya mwaka 1970 iliyonunuliwa kwa bilioni 8,alipatiwa ngapi???Barabara zisizo na kiwango inakuwaje???Ni bora kuwa na barabara 5 zenye viwango vya kimataifa kuliko kuwa na barabara 10 mvua moja tu hatuna barabara.
 
Well said! Lakini wasiwasi wangu ni je wewe mwenyewe pasco ni ignorant? au hauna enough information, au umeamua kujitoa ufahamu:

Siku hizo naona wewe na yericho mnachosema ni kimoja: sorry kama nitakuoffend kukufananisha na mheshimiwa yericho
 

With just two days to go, there is nothing new to say, yote yameishasemwa, sasa imebaki kukumbushana tuu, tulisema nini, nini kimefanyika, uchaguzi ndio keshokutwa Jumapili, nini kitafanyika siku hiyo, na baada ya hapo, tukutane tena wiki ijayo, au tupongezane, au tupeane pole!.

Nchi hii inaweza tuu kubadilishwa kwa watu wenye uthubutu wa kuchukua maamuzi magumu, na kusimama wahesabiwe!.

I'm very proud kuwa ni mmoja wa wapiga kura hiyo Jumapili.

Haya shime kwa wote waliojiandikisha, tujitokeze kwa wingi, tuitumie haki yetu ya kidemokrasia kujichagulia viongozi wetu,

We have to choose our leaders and love our choices and live with or without!.

Pasco
 
Namalizia kwa kukumbushia lile swali la msingi, baada ya kusoma haya, kweli bado kuna watu wataichagua CCM?, na iwapo wataichagua tena CCM, kuichagua huku CCM, jee ni kielelezo cha kufanyika kwa informed decision au ni uthibitisho wa muendelezo wa ignorance ya Watanzania kuendelea kujichagulia tuu kwa mazoea?!.

Tafakari kwa makini, fikia maamuzi ya busara, hakikisha Tarehe 25 October, unajitokeza kifua mbele, kwenda kuitumia haki yako ya kidemokrasia kuamua hatima ya nchi hii kwa kupiga kura.

Nawatakia Uch
aguzi mwema.

Pasco
 
Voting Lowasa counts as being fooled again, he represents the fraction of CCM which is most virulent when it come to graft and corruption. We would rather give CCM 5 more years as we reorganize proper change.

To me this ignorance. Kumbuka ignorance is too expensive. Ccm haitakiwi kurudi madarakani. The only difference between ccm and Magufuli is the similarity. Hana jipya.
 

wanabodi, mimi nimekubali matokeo kwa roho safi, kwa roho nyeupe!, na maadam niliishaiona possibility hii, sasa tujiandae kuufunga huu ukurasa, tuyaanze maisha mapya ya baada ya uchaguzi!.

Pasco
 
wanabodi, mimi nimekubali matokeo kwa roho safi, kwa roho nyeupe!, na maadam niliishaiona possibility hii, sasa tujiandae kuufunga huu ukurasa, tuyaanze maisha mapya ya baada ya uchaguzi!.

Pasco

Whenever dealing with people of a heterogenous origin. . . . . have some reservations

Next time. . . .
 
Kama walivyofanya Bara, na Wazanzibari wameamua kwa kauli moja kuirudisha CCM.

Hongereni Wanzanzibari, tumeushuhudia uchaguzi, ulikuwa huru na wa haki, utulivu na amani,

Sasa uchaguzi umekwisha, tusonge mbele!.

Pasco
 
Nimeikuta hli mahli humu jf, nikaguswa nimeomba kulitumia bandiko hili kuboresha bandiko langu hili.

Pasco
 
Naona watu wanazidi kumlalamikia Rais Magufuli kwa udikiteta, na kwa kauli zake!,it is as if Magufuli alijiweka mwenyewe!, Magufuli hakujiweka bali tumemuweka sisi wenyewe kwa ridhaa yetu, hivyo tumwacheni rais wetu afanya kazi tuliomtuma jinsi ile yeye mwenyewe ataona inafaa!.

Pasco
 
Huu ushindi wa kishindo wa CCM kwenye udiwani, ni uthibitisho wa bandiko hili, kiukweli wajameni, safari bado ni ndefu sana, na ni ngumu sana!.

Paskali
 
Uchaguzi wa Marudio wa Majimbo ya Kinondoni na Siha ni Jumamosi hii. Sitashangaa kama majimbo yote mawili, CCM itashinda kwa kishindo!.
Hivi ndivyo Watanzania tulivyo.
P.
 
Na haitashangaza wakishindwa pia.

Suala ni tunajenga desturi mbaya ya matumizi ya fedha kwa kisingizio cha domokrasia.

Tusahau uzalendo wa nchi kwanza kama tunaendekeza ushabiki huu wa vyama mfu visivyo na itikadi wala ajenda za kueleweka.
 
Uchaguzi wa Marudio wa Majimbo ya Kinondoni na Siha ni Jumamosi hii. Sitashangaa kama majimbo yote mawili, CCM itashinda kwa kishindo!.
Hivi ndivyo Watanzania tulivyo.
P.

Ukitumia Polisi na mabomu ya Machozi lazima washinde.Na ukiamua kuwanyima Mawakala haki ya kuwa mashahidi wa Muwakilishi upande wa upinzani,kwanini CCM wasishinde?

Unajisikiaje unaenda kuoa halafu Mshenga anakwambia utakachokiona kinafanywa humo ndani usikiseme nje ,unakuta Mchumba ana Kijana mwingine ndani na bado unalazimishwa kuoa maana umeishaambiwa utakachokiona ndani usikiseme upo?
 
Pasco bana
Unatumia muda wako kujibizana na huyu aliyefukuzwa na Bavicha?
I take this girl as political wh0re.
Mkuu the invincible, hapa ulikuwa unamaanisha nini?. Kwa sasa huyu ni waziri, jee inaaminisha hizo huduma amezitoa mahali ndipo zikampatia huo uwaziri?.
P
 

Paskali hawa huwa HAWACHAGULIWI BALI WANAPINDUA MATOKEO ILI YAWE WAYATAYO WAO, on FREE BETTEL FIELD HAWANAUBAVU, ASUBUHI TU WANANG'OLEWA
 
Mkuu the invincible, hapa ulikuwa unamaanisha nini?. Kwa sasa huyu ni waziri, jee inaaminisha hizo huduma amezitoa mahali ndipo zikampatia huo uwaziri?.
P

Wewe ni mwandishi wa habari na bahati njema ni wale wanaojiita Wakili Msomi,je ulishauliza kilichotokea jana kwenye ofisi za Chadema?Na kama uliuliza kuna kiongozi yeyote toka CCM Waziri wa Sheria na Katiba,Waziri wa Polisi au Mkurugenzi/Mwenyekiti wa NEC-CCM imeishatolea ufafanuzi au hata kukemea?

Je kuna Sheria au kifungu cha Katiba kinachjotoa kibali kwa Polisi kutesa mpaka kiasi cha kufanya mtu atapike damu mikononi mwake?.

Ukishamaliza kuyafikiria haya utapata jibu la Invincible
 
Mkuu Pascal Mayalla

Pongezi kwako kwa kuendelea kuikosoa CCM kila mara unapopata nafasi. Wachache wamekuwa na msimamo huu bila kuyumba wala kuyumbishwa. Hongera sana.

Hoja hii ya mwanajukwaa Petition ni hoja kubwa mno. Ijapokuwa wasomaji na wachangiaji wengi wanaweza kuibeza, uhahika ni kwamba imebeba mantiki pana iliyo bayana.

Pasco, i disagree with you, that those who still support ccm are ignorant or outright ------. Up to this moment there no other credible and trustworthy alternative to ccm...not chadema or ukawa .

Hoja mahsusi hapa ni kwamba, ukiindoa CCM badala yake akae nani? Ndiposa neno la wahenga: "heri shetani umjuaye kuliko malaika usiyemjua" linapata nafasi. Hili la kwanza.

Pili ni hizi chaguzi zetu zinazoendelea kufanyika pamoja na udhaifu mkubwa wa sheria yetu ya uchaguzi. Kwa lugha rahisi, uchaguzi wa nafasi za uongozi ni sheria, kwamba zoezi la kwenda kupiga kura, kuzihesabu na kutangaza matokeo ni utekelezaji tu wa sheria yenyewe. Laiti tungetaka mabadiliko ya kweli, tungejikita kushinikiza mabadiliko ya sheria ya uchaguzi inayoelekeza hitaji la uchaguzi, sifa za wagombea, mchakato wa uchaguzi, vyombo/chombo kinachosimamia uchaguzi, utaratibu wa kampeni na kupiga kura, utaratibu wa kutangaza matokeo,utaratibu wa kukubali ama kupinga matokeo kisheria. Mwelekeo huu utajibu maswali ya msingi kuhusu uchaguzi ikiwa umefanyika kwa haki na uhuru wa kutosha ama vinginevyo.

Tatu, kwa mwelekeo wa hoja ya pili, vyama vya upinzani vingekuwa credible kidogo tu, vingejiwekea utaratibu wa kubadili sheria kandamizi, walau kubadili sheria tatu (3) kila baada ya miaka mitano. Ndio kusema toka mwaka 1992 tulipoanza vyama vingi mpaka leo hii, walau tungekuwa na sheria kandamizi 15 zilizobadilishwa kujibu mahitaji ya wananchi. Pamoja na uwepo wa upinzani kwa miaka 23 sasa, sheria kandamizi zilizokuwa zinalalamikiwa kama sheria ya uhuru wa habari na kupashana habari ya mwaka 1976, sheria hii ya uchaguzi, sheria zinazoelekeza kinga na mamlaka ya Raisi bado hazina maboresho stahili ya kujivunia hapa nchini. Kinyume chake tumekuwa na operesheni mahsusi za kuichafua CCM na watendaji wake ili wachukiwe na wananchi, huku tukibeza na kusahau kwamba chama hiki kikongwe kinatumia mianya ya kikatiba na kisheria kuendelea kubaki madarakani.

Hivyo basi, hoja ya mwanajukwaa Petition inapata nguvu vizuri tu. Maana yake ni kwamba, CCM itaendelea kupata nafasi mpaka pale upinzani utakapokuwa na dira maalumu ambayo wananchi huku mtaani wanaweza kujihusisha nayo kirahisi.

 
Mkuu 50Thebe, thanks for this, very objective.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…