Kuichagua tena CCM, Je ni kielelezo cha kufanya informed decision, au ni Ignorance? | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuichagua tena CCM, Je ni kielelezo cha kufanya informed decision, au ni Ignorance?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Sep 21, 2015.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,
  Salaam.


  Kuanzia leo, hadi tarehe 24 October, kwa siku hizi 30+ zilizobakia kabla ya kufanyika uchaguzi, nitajitolea kutoa makala za uhamasishaji ili wana jf tujitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura. Makala hizi zitakuwa ni makala elimishi, ili kuwasaidia Watanzania wenzetu ambao bado wamelala, waamke ili wakachague kwa kufanye informed decision, yaani wachague kwa sababu ya kuchagua, na sio kuchagua kwa mazoea tuu!, kuchagua kwa mazoea tuu mimi nimekuita ni ignorance!.

  Kuna msemo usemao "You can fool some people for some time, but you can't fool all the people all the times!".
  Ikitokea kuna watu ambao wote wanakuwa fooled all the times, then watu hawa watakuwa ni a bunch of fools and ignorants!. Jee sisi Watanzania wote ni a bunch of fools and ignorants?.


  CCM has been fooling us all for all the times kwa ahadi na ahadi zisizotekelezeka, na siku zote bado tunaichagua tena na tena. Miaka mitano ikifika, huja na visingizio hivi na vile vya kwanini ahadi hizo hazikutekelezwa, na kila baada ya miaka 5, huja na ahadi mpya kibao, zenye matumaini mengine mapya. Kipindi cha uchaguzi kinafika bila ahadi za zamani kutimizwa, hatuambiwi sababu kwa nini hazikutimizwa, bali tunaletewa ahadi mpya, na tunaichagua CCM tena na tena!. Jee kujiuliza kama sisi Watanzania ni ignorants au tumelogwa ni kutukana?!.

  Hii ni mada ni kufuatia mada yangu ya Jee Watanzania ni ignorants au tumelogwa? bandiko hili lilimgusa dada yangu Juliana Shonza , sijui kwa nini alishindwa kuchangia bandiko lile, ila na yeye akanzisha bandiko lake,Watanzania sio wajinga; tumekusikia, tumetafakari kujibu bandiko langu na hii ni sehemu tuu ya majibu yake


  Naomba nianze kwa kukuonya, kuna tofauti kubwa kati ya ignorance na utaahira, mimi nimesema Watanzania tunaichagua CCM kwa ignorance, naomba uliombee msamaha hili la kuwatukana watu ni mataahira kabla 'karma' ya utaahira haijakushukia, haswa kwa kuzingatia wewe bado ni binti mdogo, mbichi ndio kwanza unajiandaa kuingia kwenye ujenzi wa familia!. Omba tuu hata kimoyo moyo Mungu akuepushie mbali tukano hilo la kutukana watu mataahira!.

  Naomba niweke in points format, ili iwe rahisi kuchangia kwa kujibu hoja au kupangua hoja kwa hoja na sio hoja kwa viroja!.

  1. Tulipopata uhuru ile miaka ya 60, tulikuwa na maadui wakubwa watatu, ujinga, umasikini na maradhi!, tulikuwa na all the resources to make this country move forward, watu, ardhi, siasa safi, na uongozi bora, tena ilisemwa, fedha sii msingi bali ni matokeo!, tulikuwa na udongo wenye rutuba, vyanzo lukuki vya maji, mali asili, utalii, utajiri mkubwa wa madini, etc, etc, in short we had everything, na wenzetu tuliopata nao uhuru, had nothing compared!, leo wenzetu have everything and sisi not only we have nothing!, bali umasikini umeongezeka mara dufu!, tulikua tuna object poverty sasa tuna stinking poverty!, ni umasikini uliotopea, kila siku ni afadhli ya jana!. Ujinga umeongezaka maradufu!, wakati wa Nyerere, there was a time litaracy level yetu ilikua juu, hadi wazee walifundishwa elimu ya watu wazima na elimu ya kujua kusoma na kuandika katika elimu ya ngumbaru!, leo mwanafunzi anamaliza darasa la saba hajui kusoma wala kuandika!. Maradhi ndio usiseme!, lakini leo sio tuu bado tuna wale maadui watatu, bali sasa tumeaongeza na maadui wengine wawili zaidi ambao hawa ni CCM's own making!, rushwa na ufisadi!.
  2. Nakubalina na wewe Baba wa Taifa hili, Mwalimu Nyerere amelifanyia makubwa taifa hili, na pia ni kweli mchango wa Tanzania katika ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika na Vita vya Kagera, vimechangia kururudisha nyuma maendeleo yetu, but to what extence?!.
  3. Mwalimu Nyerere alifika mahali, akakubali makosa, akakiri kufanya kosa sii kosa, kosa ni kurudia kosa, hivyo kwangu tatizo sio Mwalimu bali hawa waliomfuatia sio tuu kwa kurudia makosa bali kuongeza na makosa mengine mapya ya kijinga kabisa!, ujinga huu ndio ignorance ninayoizungumza mimi, mjinga, akikupa sababu za kijinga na wewe ukaendelea kumchagua, wewe unaemchagua ndio mjinga kabisa!. Hivyo nimeuliza Jee sisi Watanzania wote ni wajinga ki hivyo?. Are we all that ignorants?!.
  4. Mimi sio miongoni mwa lile kundi wanaosema CCM, haijafanya kitu, kuna mengi tuu mazuri CCM imefanya, na nimeyasema humu,Miongoni Mwa Mazuri ya CCM, but it is not enough!, uzuri wangu, mazuri ya CCM nimeyakubali na kuyataja humu, ila pia mabaya ya CCM na madudu ya CCM nimeyataja!,Mapungufu ya CCM: A Constructive Criticisim!, madudu ni mengi zaidi kuliko mazuri, hivyo nimeuliza,does CCM deserve kupewa another chance?, au kupumzishwa ni halali?! ila tukiamua kuipumzisha, nikashauri na tuipumzishe kwa upendo na amani.
  5. CCM imefanya mismanagement kubwa ya resources za nchi hii for too long!, sasa nchi yetu imefikia stage tunona pride raisi wetu kupanda ndege kusafiri kwenda ulaya kutembeza bakuli!, wakati tuna utajiri mkubwa wa maliasili na rasimali za kutosha kutufanya kuweza kujitegemea!, kitendo cha Tanzania kuwa bado ni taifa omba omba!, its just unacceptable and it is a shame!.
  6. Rushwa ya petty corruption is an order of the day!, kiasi kwamba baadhi yetu ukikamatwa na kosa la traffic, kuliko kusubiria hiyo notification ya bila risiti, bora mmalizane hapo hapo na kusave time!. Hata kujiandikisha tuu kwenye daftari ya kudumu la wapiga kura, I had to do something!, nakiri sikuombwa chochote na yoyote, bali nilipofanya time management ya kuamka saa 10 alfajiri ili kuwahi foleni, na kushinda siku nzima kituoni, nika opt kuitumia ile dawa ya 'penye uzia!'. Mwanzo rushwa ilikua siri, sasa ni mambo hadharani, wazi wazi!, Trafick hawaendi tena kupokelea pembeni au uchochoroni kwa kujificha, bali wameihalalisha wazi wazi kwa kutembea na vitabu fake vya notification, unaandikiwa na kuambiwa risiti uipitie baadae!.
  7. The grand corruption ndio usiseme, sisi tulio sekta binafsi tunajua, ili ushinde tender unapaswa kufanya nini!. Manunuzi ya umma ni kwa kickback za kueleweka!, ile ya Rada imerudishwa kwa uadilifu tuu wa Waingereza tena kwa taarifa yako tuu, kama hujui, ule mgao wa Change ulikua ni vijisenti tuu, laiti Watanzania wangesikia wale wazee 'wanene' wa kule top walivuta ngapi, hata kusubiria tuu hadi mwaka wa uchaguzi ufike ndipo wafanye mabadiliko, watu wangeona mbali!, wangemarch streets moja kwa moja hadi kwenye ile nyumba pale, kwenda kuwafurusha na kuwatoa baru!. CCM waishukuru sana BAE kwa kuyahifadhi majina ya waliolipwa hizo kickbacks na badala yake kukubali kulipa faini ya non-disclosure ndio hicho kinachoitwa change ya Rada!.
  8. Ufisadi ni kila kona, mfano mdogo ni ununuzi wa ndege ya rais bei yake imeonekana wazi ni bilioni 18 tuu!, ajenti analeta bili ya bilioni 43 serikali inaonyeshwa hadi bei halisi ya kiwandani, lakini bado inaendelea tuu kulipa!, only the fools and the ignorants ndio wataamini there was no kickbacks hadi kule the highest office!. Ajenti wa ndege hiyo ndio huyo huyo ajenti wa rada, ndio huyo huyo ajenti wa zile helcopter mbovu, ndie ajenti wa magari ya jeshi mtumba na vifa vya kivita viwivyofanya kazi!, na siku za sherehe za Ikulu, ukiondoa magari ya viongozi wakuu wa kitaifa ambao magari yao ndio huruhusiwa kupaki ndani ya Ikulu, gari la ajenti huyu, Red Ferrarri, ndilo hupaki ndani ya Ikulu tena pale garden ili kila mtu alione na kumtambua yuko karibu na familia ya rais, hata magari ya mawaziri na mabalozi hupaki nje!, ni ignorant tuu pakee ndiye atakayeamini 'jamaa' hahusiki.
  9. Serikali ya CCM, haina vipaumbele muhimu bali inendeshwa kwa matukio!, tangu tumepata uhuru ujinga ulikua ni adui namba moja, tumefanya nini kuinua elimu yetu!, CCM imewekeza on ignorance na inaitumia hiyo ignorance kama mtaji wake wa ushindi, na ukiangalia maeneo yenye low literacy level, hizo ndizo ngome za CCM!, mkoa wenye the highest literacy level ni ya Kanda ya Kaskazini, angalia hali ya CCM!, kwa watu waelewa hawadanganyiki tena!, na ikitokea CCM ikashinda hata jimbo moja, then labda Upareni kwenye umasikini na Simanjiro kwenye ujinga!.
  10. Mzigo mkubwa unaotuongezea umasikini huu ni gharama kubwa za uendeshaji wa serikali, nchi yetu ni ndogo tuu tena masikini wa kutupwa, lakini yenye serikali kubwa for nothing!, kinchi kidogo tuu kama Tanzania kuwa na mawaziri 54!, huku linchi likubwa na tajiri kama Marekani wana mawaziri 6 tuu!, huu kama sio ujinga ni nini?!. Tukiwa na mfumo mzuri hata ma DC ni redundant, just a wastege of resources!, Tuna baadhi ya idara zinazojitegemea, hazina kichwa wala miguu mfano baada ya kuwa na Vizazi na Vifo halafu tunaanzisha NIDA kufanya kitu kile kile ambacho kingefanywa vizuri zaidi na Vizazi na Vifo!.
  11. Madini tumetoa bure!, na gesi pia tunatoa bure!. Gesi asili: Is it "day light robbery?!"- watanzania tunaibiwa Mchana Kweupe! .
  12. Handling ya issue ya Escrow, ni kielelezo cha ignorance ya hali ya juu!.Escrow: Jee Watanzania ni Ignorants? au Tumelogwa?!.
  13. Hakuna ubishi kuwa siku zote, CCM imekuwa ikishinda chaguzi mbalimbali ka mbinu tuu na mtaji wao mkubwa wa ushindi ni kuitumia ignorance ya "watu" ambao CCM imewekeza!.
  14. Hakuna ubishi kuwa CCM kama chama, kimechoka, dalili zote za chama kichovu kinachosubiri kifo, tayari, zimeisha jitokeza kwa CCM, kinachosubiriwa sasa its only a matter of time ni lini kitaangwa rasmi, hiyo October 25 is the day of the judgement!, yaani it is Judgment Day!. CCM Imechokwa, Mtazamo: CCM imechokwa mpaka basi!
  15. Hakuna ubishi kuwa wengi wa hao "watu", wamekuwa wakiichagua CCM sio kwa sababu wanaipenda sana!, (waipende kwa lipi?), la hasha!, "watu" wamekuwa wakiichagua CCM kwa mazoea tuu! kufuatia ignorance yao!.
  16. Hakuna ubishi, kuwa wengi wa hao "watu" waliokuwa wakiichagua CCM kwa ignorance ya mazoea tuu, sasa wameamka kutoka katika usingizi wameichoka, hivyo October 25, hawatachagua tena chama kwa mazoea, bali watachagua chama kwa "sababu"!.
  17. Tatizo kubwa la Watanzania au adui mkubwa wa Tanzania sio CCM, CCM is just a vehicle, haikujiweka hapo ilipo, imewekwa, kwa ignorance yetu, hivyo tatizo sio CCM iliyowekwa, bali tatizo ni sisi, wale walioiweka CCM hapo ilipo!. That simply means, tatizo ni sisi Watanzania tulioiweka CCM madarakani kwa ignorance yetu, and it plays games on us again and again na sisi tukiendelea kuiweka madarakani again and again and again na sitashangaa kama hata October 25, hawa ignorants ambao hawajabadilika kama ni wengi kuliko walioamka, then sitashangaa wakiirudisha tena CCM ikulu ya Magogoni!, huku kutakua ni uthibitisho wa ignorance!.
  18. Chaguzi nyingine zote, CCM imekuwa ikichaguliwa kwa walkover victory kwa ignorance tuu kwa sababu we had no choice to choose from, uchaguzi wa mwaka huu, tuna altenative, we have a choice kati ya kuichagua CCM au kuipiga chini!, watu tutaingia kwenye uchaguzi with choice na sio walk over kama mazoea, hivyo CCM ikichaguliwa tena, then hiyo ndio itakua choice yetu tumechagua tena kwa sababu na sio kwa mazoea ya ujinga (ignorance)!.

  Namalizia kwa kukumbushia lile swali la msingi, baada ya kusoma haya, kweli bado kuna watu wataichagua CCM?, na iwapo wataichagua tena CCM, kuichagua huku CCM, jee ni kielelezo cha kufanyika kwa informed decision au ni uthibitisho wa muendelezo wa ignorance ya Watanzania kuendelea kujichagulia tuu kwa mazoea?!.

  Tafakari kwa makini, fikia maamuzi ya busara, hakikisha Tarehe 25 October, unajitokeza kifua mbele, kwenda kuitumia haki yako ya kidemokrasia kuamua hatima ya nchi hii kwa kupiga kura.

  Nawatakia Jumatatu Njema.

  Paskali
   
 2. delusions

  delusions JF-Expert Member

  #21
  Sep 21, 2015
  Joined: Jan 11, 2013
  Messages: 4,943
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  Ichaguliwe tena kwa lipi la maana kwa kutuwekea vasco da gama?
   
 3. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #22
  Sep 22, 2015
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 26,400
  Likes Received: 17,583
  Trophy Points: 280
  Tupo pamoja.Na pia atuambie kwenye zile bilioni 262 alikatiwa ngapi???Kwenye nyumba za serikali je??Kivuko/meli ya mwaka 1970 iliyonunuliwa kwa bilioni 8,alipatiwa ngapi???Barabara zisizo na kiwango inakuwaje???Ni bora kuwa na barabara 5 zenye viwango vya kimataifa kuliko kuwa na barabara 10 mvua moja tu hatuna barabara.
   
 4. Simple

  Simple JF-Expert Member

  #23
  Sep 22, 2015
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 249
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Well said! Lakini wasiwasi wangu ni je wewe mwenyewe pasco ni ignorant? au hauna enough information, au umeamua kujitoa ufahamu:

  Siku hizo naona wewe na yericho mnachosema ni kimoja: sorry kama nitakuoffend kukufananisha na mheshimiwa yericho
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #24
  Oct 23, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  With just two days to go, there is nothing new to say, yote yameishasemwa, sasa imebaki kukumbushana tuu, tulisema nini, nini kimefanyika, uchaguzi ndio keshokutwa Jumapili, nini kitafanyika siku hiyo, na baada ya hapo, tukutane tena wiki ijayo, au tupongezane, au tupeane pole!.

  Nchi hii inaweza tuu kubadilishwa kwa watu wenye uthubutu wa kuchukua maamuzi magumu, na kusimama wahesabiwe!.

  I'm very proud kuwa ni mmoja wa wapiga kura hiyo Jumapili.

  Haya shime kwa wote waliojiandikisha, tujitokeze kwa wingi, tuitumie haki yetu ya kidemokrasia kujichagulia viongozi wetu,

  We have to choose our leaders and love our choices and live with or without!.

  Pasco
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #25
  Oct 24, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  Namalizia kwa kukumbushia lile swali la msingi, baada ya kusoma haya, kweli bado kuna watu wataichagua CCM?, na iwapo wataichagua tena CCM, kuichagua huku CCM, jee ni kielelezo cha kufanyika kwa informed decision au ni uthibitisho wa muendelezo wa ignorance ya Watanzania kuendelea kujichagulia tuu kwa mazoea?!.

  Tafakari kwa makini, fikia maamuzi ya busara, hakikisha Tarehe 25 October, unajitokeza kifua mbele, kwenda kuitumia haki yako ya kidemokrasia kuamua hatima ya nchi hii kwa kupiga kura.

  Nawatakia Uch
  aguzi mwema.

  Pasco
   
 7. P

  Prime Dynamics JF-Expert Member

  #26
  Oct 24, 2015
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 525
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  To me this ignorance. Kumbuka ignorance is too expensive. Ccm haitakiwi kurudi madarakani. The only difference between ccm and Magufuli is the similarity. Hana jipya.
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #27
  Oct 27, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  wanabodi, mimi nimekubali matokeo kwa roho safi, kwa roho nyeupe!, na maadam niliishaiona possibility hii, sasa tujiandae kuufunga huu ukurasa, tuyaanze maisha mapya ya baada ya uchaguzi!.

  Pasco
   
 9. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #28
  Oct 27, 2015
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,192
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Whenever dealing with people of a heterogenous origin. . . . . have some reservations

  Next time. . . .
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #29
  Mar 22, 2016
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  Kama walivyofanya Bara, na Wazanzibari wameamua kwa kauli moja kuirudisha CCM.

  Hongereni Wanzanzibari, tumeushuhudia uchaguzi, ulikuwa huru na wa haki, utulivu na amani,

  Sasa uchaguzi umekwisha, tusonge mbele!.

  Pasco
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #30
  Apr 13, 2016
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  Nimeikuta hli mahli humu jf, nikaguswa nimeomba kulitumia bandiko hili kuboresha bandiko langu hili.

  Pasco
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #31
  Sep 5, 2016
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  Naona watu wanazidi kumlalamikia Rais Magufuli kwa udikiteta, na kwa kauli zake!,it is as if Magufuli alijiweka mwenyewe!, Magufuli hakujiweka bali tumemuweka sisi wenyewe kwa ridhaa yetu, hivyo tumwacheni rais wetu afanya kazi tuliomtuma jinsi ile yeye mwenyewe ataona inafaa!.

  Pasco
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #32
  Nov 27, 2017
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  Huu ushindi wa kishindo wa CCM kwenye udiwani, ni uthibitisho wa bandiko hili, kiukweli wajameni, safari bado ni ndefu sana, na ni ngumu sana!.

  Paskali
   
 14. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #33
  Feb 13, 2018
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  Uchaguzi wa Marudio wa Majimbo ya Kinondoni na Siha ni Jumamosi hii. Sitashangaa kama majimbo yote mawili, CCM itashinda kwa kishindo!.
  Hivi ndivyo Watanzania tulivyo.
  P.
   
 15. Hercule Poirot

  Hercule Poirot JF-Expert Member

  #34
  Feb 13, 2018
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 1,245
  Likes Received: 517
  Trophy Points: 280
  Na haitashangaza wakishindwa pia.

  Suala ni tunajenga desturi mbaya ya matumizi ya fedha kwa kisingizio cha domokrasia.

  Tusahau uzalendo wa nchi kwanza kama tunaendekeza ushabiki huu wa vyama mfu visivyo na itikadi wala ajenda za kueleweka.
   
 16. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #35
  Feb 13, 2018
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 26,400
  Likes Received: 17,583
  Trophy Points: 280
  Ukitumia Polisi na mabomu ya Machozi lazima washinde.Na ukiamua kuwanyima Mawakala haki ya kuwa mashahidi wa Muwakilishi upande wa upinzani,kwanini CCM wasishinde?

  Unajisikiaje unaenda kuoa halafu Mshenga anakwambia utakachokiona kinafanywa humo ndani usikiseme nje ,unakuta Mchumba ana Kijana mwingine ndani na bado unalazimishwa kuoa maana umeishaambiwa utakachokiona ndani usikiseme upo?
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #36
  Feb 13, 2018
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  Mkuu the invincible, hapa ulikuwa unamaanisha nini?. Kwa sasa huyu ni waziri, jee inaaminisha hizo huduma amezitoa mahali ndipo zikampatia huo uwaziri?.
  P
   
 18. d

  defence JF-Expert Member

  #37
  Feb 13, 2018
  Joined: Aug 13, 2008
  Messages: 570
  Likes Received: 260
  Trophy Points: 80
  Paskali hawa huwa HAWACHAGULIWI BALI WANAPINDUA MATOKEO ILI YAWE WAYATAYO WAO, on FREE BETTEL FIELD HAWANAUBAVU, ASUBUHI TU WANANG'OLEWA :D:D:D:D:D:D:D
   
 19. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #38
  Feb 13, 2018
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 26,400
  Likes Received: 17,583
  Trophy Points: 280
  Wewe ni mwandishi wa habari na bahati njema ni wale wanaojiita Wakili Msomi,je ulishauliza kilichotokea jana kwenye ofisi za Chadema?Na kama uliuliza kuna kiongozi yeyote toka CCM Waziri wa Sheria na Katiba,Waziri wa Polisi au Mkurugenzi/Mwenyekiti wa NEC-CCM imeishatolea ufafanuzi au hata kukemea?

  Je kuna Sheria au kifungu cha Katiba kinachjotoa kibali kwa Polisi kutesa mpaka kiasi cha kufanya mtu atapike damu mikononi mwake?.

  Ukishamaliza kuyafikiria haya utapata jibu la Invincible
   
 20. 50thebe

  50thebe JF-Expert Member

  #39
  Feb 13, 2018
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 1,960
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  Mkuu Pascal Mayalla

  Pongezi kwako kwa kuendelea kuikosoa CCM kila mara unapopata nafasi. Wachache wamekuwa na msimamo huu bila kuyumba wala kuyumbishwa. Hongera sana.

  Hoja hii ya mwanajukwaa Petition ni hoja kubwa mno. Ijapokuwa wasomaji na wachangiaji wengi wanaweza kuibeza, uhahika ni kwamba imebeba mantiki pana iliyo bayana.


  Hoja mahsusi hapa ni kwamba, ukiindoa CCM badala yake akae nani? Ndiposa neno la wahenga: "heri shetani umjuaye kuliko malaika usiyemjua" linapata nafasi. Hili la kwanza.

  Pili ni hizi chaguzi zetu zinazoendelea kufanyika pamoja na udhaifu mkubwa wa sheria yetu ya uchaguzi. Kwa lugha rahisi, uchaguzi wa nafasi za uongozi ni sheria, kwamba zoezi la kwenda kupiga kura, kuzihesabu na kutangaza matokeo ni utekelezaji tu wa sheria yenyewe. Laiti tungetaka mabadiliko ya kweli, tungejikita kushinikiza mabadiliko ya sheria ya uchaguzi inayoelekeza hitaji la uchaguzi, sifa za wagombea, mchakato wa uchaguzi, vyombo/chombo kinachosimamia uchaguzi, utaratibu wa kampeni na kupiga kura, utaratibu wa kutangaza matokeo,utaratibu wa kukubali ama kupinga matokeo kisheria. Mwelekeo huu utajibu maswali ya msingi kuhusu uchaguzi ikiwa umefanyika kwa haki na uhuru wa kutosha ama vinginevyo.

  Tatu, kwa mwelekeo wa hoja ya pili, vyama vya upinzani vingekuwa credible kidogo tu, vingejiwekea utaratibu wa kubadili sheria kandamizi, walau kubadili sheria tatu (3) kila baada ya miaka mitano. Ndio kusema toka mwaka 1992 tulipoanza vyama vingi mpaka leo hii, walau tungekuwa na sheria kandamizi 15 zilizobadilishwa kujibu mahitaji ya wananchi. Pamoja na uwepo wa upinzani kwa miaka 23 sasa, sheria kandamizi zilizokuwa zinalalamikiwa kama sheria ya uhuru wa habari na kupashana habari ya mwaka 1976, sheria hii ya uchaguzi, sheria zinazoelekeza kinga na mamlaka ya Raisi bado hazina maboresho stahili ya kujivunia hapa nchini. Kinyume chake tumekuwa na operesheni mahsusi za kuichafua CCM na watendaji wake ili wachukiwe na wananchi, huku tukibeza na kusahau kwamba chama hiki kikongwe kinatumia mianya ya kikatiba na kisheria kuendelea kubaki madarakani.

  Hivyo basi, hoja ya mwanajukwaa Petition inapata nguvu vizuri tu. Maana yake ni kwamba, CCM itaendelea kupata nafasi mpaka pale upinzani utakapokuwa na dira maalumu ambayo wananchi huku mtaani wanaweza kujihusisha nayo kirahisi.

   
 21. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #40
  Feb 13, 2018
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,465
  Likes Received: 22,760
  Trophy Points: 280
  Mkuu 50Thebe, thanks for this, very objective.
  P
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...