Kuhusu VolksWagen Golf. Bei, uimara, spea etc

Kuhusu VolksWagen Golf. Bei, uimara, spea etc

muuza ugoro

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2012
Posts
334
Reaction score
61
Wana Dijitali,
Salaam. Nime fall kwa hii VW golf, sasa b4 maamuzi ningependa pata ushauri kuhusu Bei, upatikanaji wa spea, uimara na mengineyo. Katika pita pita zangu, nikaulizia kwenye Yard flani pale mwenge karibu na mlimani city(wanauzaga baskeli pia) nikaambiwa ni 12.5M, mijicho ilintoka kwa kweli. Sasa waTZ wenzangu em nambieni kama ntapata below that offer
 
Kimbia haraka sio gari hizo, kama huna fedha za wizi usijaribu, maana kila ikisumbua kidogo tu diagnosiss test kabla ya matengenezo
 
Golf ni gari nzuri (performance,style,comfort,durability etc). Sijui kwa TZ kwa sasa, ila magari mengi yanamekuwa sophisticated sana kwa maana ya Technology hivyo kupelekea kuhitaji kufanyiwa diagnosis kwa nza ili kuwa na hakika tatizo ni nini.

bei uliyotaja siwezi kuisemea maana hujesema Golf yenyewe: 1. Ni ya mwaka gani 2.Diesel/Petrol 3.Auto au Manual 4.Engine size

Angalia sana usinunue gari ya petrol ambayo engine ni zaidi ya 1.8cc
Ubora wa barabara unatufanya tuhitaji Economy cars na sio power!
 
acha na hiyo gari,itakutia umasikini mtu mwenyewe mbangaizaji!!
 
Ni ya mwaka 99-2002. Grey colour, 1600CC, petrol na Automatic.
 
Ni ya mwaka 99-2002. Grey colour, 1600CC, petrol na Automatic.

Kuna generation 7 za VW Golf. Engine kuanzia 1200cc hadi 3200cc(VR6). Uliyotaja kwa kukadiria mwaka inaweza ikawa Golf Mk4(1J). Ikianza mambo ya umeme utaimba. Nakushauri utafute MK5(1K) au MK6. Ukizingatia service, uwe makini na warning lights gari itadumu.
 
Back
Top Bottom