jMali
JF-Expert Member
- Nov 9, 2010
- 8,401
- 4,965
Kwa bahati mbaya ziara ya rais wa Tanzania mhe John Magufuli nchini Rwanda inapotoshwa sana hasa na mashabiki wa Rwanda/kagame humu mitandaoni mfano rejea: Wako wapi wale anti Kagame?.
Mhanga wa ziara hiyo amekuwa rais mstaafu Jakaya Kikwete, ambaye katika hali isiyo ya kawaida analaumiwa kwa ugomvi ambao kwa mtu yoyote makini ulishakwisha toka mwaka jana! Yafuatayo ni maoni yangu juu ya vitu muhimu ambavyo vinapotoshwa:
1. KUZOROTA UHUSIANO NI KOSA LA KIKWETE:
Ukisoma maoni ya wanazi mbalimbali wa Rwanda/Kagame, Tanzania inaonekana kuwa ndio iliyoikosea Rwanda. Suala hili sio kweli.
Jambo la kwanza lililozorotesha uhusiano wetu na Rwanda ni pale ambapo Tanzania iliamua kuungana na mataifa ya DRC na Afrika kusini kuwapiga waasi wa M23 kijeshi mwaka 2013. Maamuzi haya yalikuwa kinyume na mtazamo wa mataifa ya Kenya, Uganda na Rwanda ambao wakati huo walikuwa wakijiita COW (coalition of the willing), ambao wao walipendelea mazungumzo yasiyokuwa na tija yaendelee kati ya M23 na Uganda. Ni siri iliyokuwa wazi kuwa majeshi ya M23 yalikuwa ni vibaraka wa Rwanda. Hili limethibitishwa na ripoti ya umoja wa mataifa. Pia nchi za marekani na Uingereza zilisitisha misaada kwenda Rwanda kama adhabu (kama sisi tulivyokosa pesa za MCC) kutokana na nchi hizo kujiridhisha kuwa Rwanda ilikuwa nyuma ya M23, cha ajabu Rwanda haikuwahi kuzishutumu nchi hizi kama ambavyo ilimshutumu waziri Bernard Membe ambaye yeye alirejea taarifa hizo hizo za umoja wa mataifa.
Suala lingine lililoleta shida ni pale ambapo rais Kikwete, katika mkutano wa nchi za maziwa makuu, alishauri mazungumzo kati ya serikali na waasi wa nchi mbalimbali zenye vita ikiwapo Rwanda. (chanzo: KIKWETE Statement on Rwanda misquoted | The Rwandan). Ushauri huu ulipokelewa vizuri na nchi zote Uganda na DRC kasoro Rwanda. Hakukuwa na shida yoyote kama Rwanda wangepuuza ushauri wetu, lakini cha ajabu uongozi wa serikali ya Kagame ukalipuka kwa matusi na kashfa mbalimbali za kutuita interahamwe, uzushi kama kabila la mke wa Rais na mengineyo na mwishowe kwa rais Kagame binafsi kutishia kumpiga Kikwete. Hali hii ikapelekea Tanzania nayo kujibu mashambulizi kwa maneno mbalimbali.
Hata hivyo ugomvi huu ulikuwa ni vita baridi, kwani mahusiano ya kibalozi bado yaliendelea pale pale, hakuna siku wananchi wa Tanzania au Rwanda nikiwamo mwandishi wa post hii walizuiwa au kurudishwa mpakani pale walipotaka kuvuka. Hakuna manyanyaso yoyote ambayo raia wa nchi zetu walizipata wakiwa wanaishi na kufanya kazi kihalali nchi nyingine. Hivyo ugomvi huu ulikuwa ni wa ngazi za kisiasa zaidi na haukufika chini kwa viwango vya wananchi kuonana maadui, isipokuwa labda kwenye mitandao ya kijamii.
Kwa sababu zote kuu mbili za ugomvi wetu, hakuna uwezekano wowote kuwa rais Kikwete au nchi ya Tanzania ndio iliyokosea. Ni upotofu mkubwa kumlaumu Kikwete na Tanzania kutokana na ugomvi uliotokea. Uongozi wa rais Kagame wa Rwanda una historia iliyotukuka ya kugombana na nchi nyingi duniani kuliko nchi yoyote hapa Afrika labda na dunia kutokana na hulka yake ya kibabe. Mifano michache ni:
2. KURUDI KWA UHUSIANO KUNATOKANA NA ZIARA HII YA MAGUFULI:
Ukweli ni kuwa marais Paul kagame na Jakaya kikwete walikutana na kuzungumza hadharani kwa mara ya kwanza baada ya nchi zetu kupishana maneno kwenye mkutano wa 16 wa viongozi wa Afrika mashariki kwenye ukumbi wa KICC pale Nairobi mwezi februari mwaka 2015.
Wiki chache baadae mwezi march 2015 Kagame alikuja Tanzania na kushirikiana na rais Jakaya Kikwete kuzindua njia ya treni kutoka Dar e salaam kwenda rusumo/isaka mpakani mwa Tanzania na Rwanda. Kwa mara nyingine tena Paul Kagame akaja Tanzania mwezi November 2015 kuhudhuria uapishwaji wa rais John Magufuli.
Nashangaa kuona wapotoshaji wanaandika kuwa Magufuli kukubali mwaliko wa Rwanda ndio kumemaliza tofauti zilizokuwapo, pamoja na maneno mengine ya kutudunisha watanzania mbele ya Rwanda, kana kwamba Magufuli kaenda kuomba msamaha! Je kuja kwa Kagame nchini kwetu mara mbili, tena sio kusalimia bali kikazi hakukutosha kumaliza huo ugomvi na badala yake ni Magufuli ndio kamaliza ugomvi kwa kukubali mwaliko wa Kagame kwenda kutembea? Kwa nini Kagame alivyokuja hatukuambiwa kuwa kaja “kujifunza”, “anamkubali sana kikwete” na mengineyo?
kama kuna suala la msamaha kwa namna yoyote ile, ni Kagame ndie aliyeomba msamaha. Kwa tamaduni za kinyarwanda/kihima kutoa ng'ombe ni ishara ya kuomba amani na kuimarisha undugu, sio zawadi inayotolewa kiholela. Mara ya mwisho kwa kagame kutoa ng'ombe ilikuwa ni kurudisha uhusiano wake na rais Museveni na nchi ya uganda baada ya muda mrefu wa vita baridi kama ambayo tulikuwa nayo kati yetu na Rwanda. Bahati mbaya wenzetu wenye asili ya Rwanda humu JF wamekulia Dar es salaam hawaelewi the essence ya zawadi hii. Badala yake wanapiga propaganda zisizo na mashiko. Hata hapa nchini kwa tamaduni za makabila mbalimbali ukichukua mtoto wa mtu au 'mzigo' wa mtu unatozwa faini ya mifugo. Anayetoa mifugo ni yule mwenye makosa.
Anyway, ieleweke kuwa kuimarika kwa uhusiano wetu kwa sasa hakuna uhusiano wowote na nchi yetu kubadili msimamo wake juu ya masuala yote ambayo yalikuwa chanzo cha ugomvi wetu na Rwanda. Kwa bahati nzuri ni kuwa makundi ya M23 na FDLR yameondolewa nchini DRC (at least kwa upande wa vita), na hivyo hatuna sababu tena ya kupishana kauli. Lakini urafiki huu haumaanishi kuwa Tanzania itaungana na Rwanda/Kagame katika kila jambo, bado Tanzania ni ile ile isiyoyumbishwa kimsimamo.
Wenu katika ujenzi wa taifa, Jmali

- Kufukuzwa kwa ubalozi mzima wa Rwanda nchini Kenya mwaka 1996 kutokana na mauaji ya mpinzani/mkimbizi wa kisiasa Seth sendashonga yaliyofanywa na maafisa ubalozi huo
- Kufukuzwa kwa ubalozi wa Rwanda nchini afrika kusini 2014 kutokana na majaribio ya mauaji ya mpinzani/mkimbizi wa kisiasa Gen Kayumba Nyamwasa.
- Kufukuzwa kwa diplomat wa Rwanda Evode Mudaheranwa nchini Sweden 2012 kwa tuhuma za kufanya ujasusi dhidi ya wakimbizi wa kisiasa nchini humo.
- Kufukuzwa kwa diplomats wa Rwanda nchini Burundi 2014 akiwamo Desire Nyaruhirira ambaye baada ya kutoroka inadaiwa nyumbani aliyokuwa anaishi kulikutwa silaha nzito za kijeshi na kiasi kikubwa cha fedha za kimarekani!