Kiongozi awaye yote siku zote hupewa habari na wasaidizi wake. Kama wakimpatia habari za uongo
hakika kosa si la mtawala. Ila kama kuna habari ya uhakika basi sisi wenye nchi tuna hiyari
ya kuiscan na kuiweka hapa bila woga. Hiyo inamfanya rais ajue kipi ni kipi.
Rais kwa vyovyote vile hawezi kwenda kila mahali na kuulizia ulizia habari. Ila asiwe mvivu, bali
awe na ki system chake cha siri cha kumpatia mambo muhimu.
Nakumbuka watoto wa Mwl. walikuwa wakimpa baba yao viswahili vya mtaani, n.k Ndo maana
Mwl. Nyerere ilikuwa si rahisi kutoa taarifa za uongo. Kuna wakati alifika mahali akauvuta mgomba
ukang'oka kwani alikwisha ambiwa kuwa pale hakukuwa na shamba ila kiini macho. na kuwa ile
migomba ilikuwa imepandwa asubuhi tu ili kumridhisha macho.