huenda mpango huu ukawa sawa na mipango mingine ya kitapeli kama ule wa DESI na mingine.mikopo inayosemekana ya nssf kutolewa kupitia kilimanjaro cooperative bank kwa vikundi na mtu mmoja mmoja kwa wakazi wa kilimanjaro na arusha inatia shaka,mikopo hiyo yenye dhamana nafuu ya kuanzia shilingi milioni kumi hadi thelasinim imeahidiwa na waliojisajili katika mpango huo na maelfu ya wananchi ambao tayari wamekuwa wakitakiwa kulipia mchango ya kujiunga nssf sh 120,000 kwa kila mtu mmoja pia shillingi 30,000 kufungulia account ya bank na shilingi 100,000 hadi laki tatu kwa ajili ya kuandaliwa andiko la biashara.waliojiandikisha katika mpango huu ni takribani watu wasiopungua elfu kumi katika utaratibu huo ikiwa ni ndani ya miezi mitatu na hakuna aliyewahi kupewa mikopo hiyo hadi sasa na bado usajili mpaka wakati huu bado unaendelea.ni wastani wa malipo ya shilingi 250,000 kwa mtu mmoja ukizidisha kwa watu elfu kumi utapata 25 bilioni.ni dhahiri huu ni utapeli na mnaojua ukweli zaidi ya jambo hili mtujuze.