kuhusu JKT,

Joined
Jan 30, 2015
Posts
18
Reaction score
1
mwezi wa pili ndio huu unaingia.kama ilivyokua imetangazwa tangu awali kwamba mchakato wa kujiunga na Jeshi letu JKT utaanza.
Naomba sana wahusika Mutuangalie na sisi Graduate,tunatamani kujiunga na Jeshi lakin Mmetubana sana kwenye suala la Umri,,,,wengi tunamaliza chuo tukiwa na miaka 24,25 na 26,,,
tafadhali sana.
 

Kaka mbona wanasema wamesitisha utaratibu huoo wa Jkt cz hawana pesa!!
Kuingia huko ni hadi mwezi wa 6 mwaka huu!!
 
Kaka mbona wanasema wamesitisha utaratibu huoo wa Jkt cz hawana pesa!!
Kuingia huko ni hadi mwezi wa 6 mwaka huu!!

Mwezi wa 6 ni ufunguzi wa kozi na si kwamba watu ndo wataanza kwenda muda huo…
 
yaas,mwezi wa 6 ni kuingia rasm vikosini,lakin mchakato unaanza rasm mwezi wa 2 asee,,
 
kuchukua form,kuna form zitatolewa wilayani kwa wanaohitaj wataenda kuzifata,,,pitia website ya jkt uone tangazo linavyosema,
 
Bishaneni weee lakini "The Time Will Tell"
 
Tangazo lao hili hapa:

MAFUNZO YA VIJANA WA JKT (KUJITOLEA). TANGAZO LA MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA VIJANA WOTE WANAOTAKA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA MWAKA 2015. UTARATIBU UTAKUWA KAMA IFUATAVYO: BARUA ZA MAELEKEZO ZITATUMWA MIKOANI FEBRUARI 2015, MCHAKATO WA KUCHAGUA VIJANA WILAYANI NA MIKOANI (MACHI HADI APRILI 2015), TIMU ZA USAILI TOKA MAKAO MAKUU YA JKT ZITAKUWA MIKOANI MEI 2015 NA VIJANA WALIOCHAGULIWA KURIPOTI VIKOSINI JUNI 2015. LINATOLEWA ANGALIZO KWA VIJANA, WAZAZI/WALEZI KUEPUKA KUDANGANYWA NA MATAPELI WANAOJIHUSISHA NA UUZAJI WA FOMU BANDIA ZA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA. FOMU ZINAZOTOLEWA SASA NI BATILI. JESHI LA KUJENGA TAIFA HALITATAMBUA USAILI WOWOTE UTAKAOFANYIKA KINYUME NA UTARATIBU ULIOAINISHWA.
TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA MAKAO MAKUU

Pitia hapa

kuhusu swala la umri, isikupe shda kwa wewe graduate unaweza omba kwa kutumia vyet vya form six, au subir nafas kwa magraduate huwa znatoka pia..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…