Kuhusu Dk. Magufuli, Mungu amejibu Maombi!

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,618
12,283
Kama wewe ni mmoja wa watu wasio amin Mungu yupo, bas leo kupitia makala hii nakuomba uamin Mungu yupo tena sio yupo tu ila yupo karibu na watu wake kuliko mama na mtoto mchanga wake.

Yapata miaka kumi ilio pita mim na watu ambao siwajuwi kwa majina wala sura tulianza kulilia taifa hili kwa namna ambayo hata mpaka leo sijajuwa kwanini.

Wengi wetu ktk kikosi hiki cha maombi tuliuwona utawala wa Rais alie staafu kama utawala ambao haki nyingi za watu zingewekwa rehani uku wenye nacho wakizidi kuneemeka wakati wasio kuwa nacho wakizidi kuwa hawana kitu.

Jambo hili lilikuwa dhahiri mbele ya Mungu na malaika zake jambo lilifanya wakati mwingine Mungu kushuka nakuhukumu mwenyewe.

Nisingependa kusema yale Mungu alihukumu ila kiuhalisia kunawakati taifa lilitikisika na wakuu wa taifa hili waliuwona mtikisiko ila Mungu hakutaka kuuangusha utawala aliwapa sign anajuwa wanachofanya na watu wake wanalia. Baruwa kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Ktk hali isiokuwa yakawaida siku Moja nikipita maeneo ya ikulu Mungu alinipa ujumbe niupeleke kwa Rais.

Nakumbuka siku ile kwa mara ya kwanza nili ingia ikulu na kuomba ofisi ya mapokez kunipa anuani yao ili nimuandikie Rais baruwa.

Kwa ukarim walinipa anuan ya ikulu na nilimpa ujumbe wake Rais. Ujumbe ulikuwa mzito na kwa hakika ulikuwa na picha ya kule tumetoka nakule twa elekea.

Wakati hayo yakiendelea mim nawenzangu ambao siwajuwi kwa majina tulipewa kazi nzito yakumuombea Rais ajaye baada ya Kikwete.

Maana ilishathibitika chini ya Mh Kikwete Mungu alisha andika kwenye ukuta mwisho kabla mwisho haujafika.

Mungu aliweka watu kulilia taifa hili kumpata Rais atakaye jibu kero za watanzania nakuwafuta machoz walio dhulumiwa nakunyanyaswa na watu ndani ya utawala ulio pita.

Kama ulikuwa hujuwi zipo dhuluma mambaya sana zilifanyika chini ya utawala ulio pita kiasi watu walikana utanzania wao nakulaani kuitwa watanzania.

Wapo wamama na watoto walikufa uku wakiulaani uongoz wa taifa hili na jambo hili lilimuumiza sana Mungu alie wapa watanzania taifa hili teule chini ya hayati baba wa Taifa Mwl Nyerere leo wana angamia kwa kukosa kiongozi mwenye uchungu na raia wake.

Kwahakika tulio kuwa tukimuomba Mungu tuliona mambo mazito ktk ulimwengu wa roho lakini Mungu akifunua mwanzo mpya kwa taifa hili nakuleta mabadiliko makubwa ktk kila sector.

Wakati Dodoma kukifukuta na taifa likiwa ktk wakati mzito watu wachache tuliamini wakati huu Tanzania haito toka kapa nilazima tumpate kiongoz shupavu atakaye itiisha nchi na ikatikisika.

Binafsi nilijuwa rais ajaye uwenda akaja kwa namna ya Daud, ambaye alitumika kupeleka mifugo machungon nakupeleka chakula vitani huyo ndie mtawala. Mh Magufuli amekuja kwa dhahiri kama Daudi na huwez kubisha Mh Magufuli ameitiisha nchi na imetikisika.

Wakati watu wanabishana kwenye vibaraza na vijiwe eti Mh Magufuli amepata urais kwa bahati mim nawashauri wakatafute historia ya Daud kama alimuangusha Goliat kwa bahati.

Mh Magufuli alipaswa kuwa rais wa Taifa hili na Mungu alie juu ukitaka kuamini angalia vile taifa amelitiisha na limetikisika.

Si bahari au nchi kavu na hata watoto wanazaliwa this time wanamtukuza Mungu maana yupo kiongoz alie jitoa kwa ajili ya Taifa hili.

Sii Magufuli anayafanya haya ila nguvu za Mungu zimemfunika amezungukwa mpaka watu wabaya wanajuwa huyu sio Rais wakawaida.

Ndio maana nikasema kuhusu Mh Magufuli Ni Mungu mwenye amejibu maombi. Mambo makubwa na mazuri yanaenda kutokea ndani ya taifa hili nakila mtu atabaki mdomo wazi.

Mwaka 2020 Mh Magufuli atapata kura asilimia 99 ya watanzania kwanin? Mungu yupo na anajibu Maombi. Mungu uibarik Tz na rais wake.

Amen
 
Mungu katukumbuka...tuzidi kuomba huruma, NEEMA na Rehema zake katika nchi yetu TANZANIA!

MUNGU ANATUPENDA!
 
Acha unafki kumuhusisha Mungu wetu mwema na Tawala za Afrika,! Nikuulize ivi bila wiz wa kura na Tume lenu la ovyo leo mngekuwa madarakan? Achani maneno ya kumchukiza Mungu, Maombi ya watanzania Mungu aliyajibu kupitia chaguo lao ambalo linajulika, ila Ibilisi ametibuwa Mpango wa Mungu, na usione kimya hasira za Mungu utaziona Juu ya wote waliyopo madarakan kwa wizi kura na kupitia tume
 
Hata Yakob alichukua uzaliwa wa kwanza wa Esau. Nampaka leo Yakob ni taifa kubwa Israel. Kama wali iba ama hawakuiba Magufuli ndie taifa kubwa na hakuna njia yeyote kumtengua kile ameshakupata.
 
Hamuachi kujifedhehesha ninyi manabii?? Ni nyiye mlipiga panda kuwa Kikwete ni chaguo la Mungu, tena mkasema ni Mungu kashuka, tena mkasema amepewa roho ya wakuu wote walio mtangulia. Leo, mnadiriki kumsema vibaya Chaguo la Mungu. Shame on yu.
Sasa mmeanza kujikomba kwa Magu, haya, ngojeni muitwe Ikulu mkanywe soda na joice. Wajinga wenu watawasikiliza ila wenye akili watakaa mbali nanyi.
Acheni kulitaja jina la Mungu hata asikofika
 
Acha unafki kumuhusisha Mungu wetu mwema na Tawala za Afrika,! Nikuulize ivi bila wiz wa kura na Tume lenu la ovyo leo mngekuwa madarakan? Achani maneno ya kumchukiza Mungu, Maombi ya watanzania Mungu aliyajibu kupitia chaguo lao ambalo linajulika, ila Ibilisi ametibuwa Mpango wa Mungu, na usione kimya hasira za Mungu utaziona Juu ya wote waliyopo madarakan kwa wizi kura na kupitia tume
Wewe lazima umekumbana na hii tumbua majipu ya JPM...........Mungu mpe maisha marefu na ujasiri Rais wetu azidi kutumbua hayo majipu yaliyokomaa......!!
 
Nimechoka kusoma hata sikumaliza nimekumbilia hitimisho na nikagundua ni upuuzi mtupu....then unadoriki kutumia jina la mwenyew Mungu kumsifia raisi .....pole sana hujitambui....hayo ni ma picha picha tu ,,by the way subiri movie ..,whats so special with magufuli???.,,,for the past two years the literate rate was 69%,but as for now and the current trend of dirty politics and unnecessary show off i bet it should have went down Tripple.,,....hata kama ni ma badiliko ni Kwa muda mfupi tu and this is what makes people in a transient confusion .....overrated!!!.....yangu macho and I can't just wait to hit july this year!
 
Hata Yakob alichukua uzaliwa wa kwanza wa Esau. Nampaka leo Yakob ni taifa kubwa Israel. Kama wali iba ama hawakuiba Magufuli ndie taifa kubwa na hakuna njia yeyote kumtengua kile ameshakupata.
Narudia tena Acha unafiki na kiligeuza neno la Mungu utakavyo ili maslahi yako yashangiliwe, acha kabsa!
 
Back
Top Bottom