Kuhusu Clinical Dentistry

History-Victory

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2021
Posts
325
Reaction score
738
Za asubuhi wakubwa.

Mdogo wenu nimemaliza kidato cha 4 mwaka 2020,na matokeo yangu ni Chem C,Bios B na Phys D,Math C,English C nikiwa na division II ya point 19...kutokana hali ya kiafya nimeshindwa kwenda Advance na pia siko interest nayo.

Kuna kozi moja nimependa kuisoma mwakani nikiwa afya itakaa sawa nayo ni Clinical Dentistry,naomba kujua ABC za hiyo kozi vigezo na vyuo vya diploma hasa serikalini,module zake na vipi ushindani ba je,kwa matokeo yangu hayo kuna chance ya kupata iwapo nitaomba?

Asante.
 
Natumaini vigezo unavyo maana wanachukuwa kama vigezo kama vya CO tu, muhimbili pale ipo sikumbuki kama wanadahiliwa kupitia mfumo wa muhimbili au wizara ya Afya, fanya utafiti zaidi.

Kwa maoni yangu ni kozi nzuri, maana kozi yoyote ya afya hata kama ukikosa ajira una uwezo wa kujiari ni nzur kwa maoni yangu.

npia ni vyema uwe na option B in case ukikosa kozi hiyo coz siku hizi kuna ushindani mkubwa sana hususani kwenye vyuo vya serikali.
 

Muhimbili hakuna diploma ya dental “kwa ninavofahamu”......
Vyuo vya serikali diploma ya dental ipo chuo cha TANGA na kile cha MBEYA....
Kuhusu vigezo umekidhi sana na utapata ila ushauri wangu sasa kama kaka yako........kama nyumban uwezo upo tafuta chuo cha Private ukapige hio kozi ili ukimaliza uweze kwenda barchelor,sababu vyuo vya government kutoboa vizurii ni shida sanaaa ila kama uwezo home haupo KAPAMBANE YOTE YANAWEZEKANA.
 
Muhimbili kuna dental technology



Dental therapey/clinical dentistry Vya serikali kuna Mbeya, Iringa Tanga na Lugalo wameanza mwaka huuu
 
Muhimbili kuna dental technology



Dental therapey/clinical dentistry Vya serikali kuna Mbeya, Iringa Tanga na Lugalo wameanza mwaka huuu
Mkuu tofauti ni nini hapo? Tupe shule
 
Kwa mtazamo wako ipi best hapo?
Dental technology Hawa wanahusika na meno bandia

Clinical dentistry Hawa wanatibu hata kama anaweza kutengeneza meno bandia nk lakini hawezi kumzidi Dental technologist
 
Mimi ni Clinical Officer nafikiri kutafuta kozi ndani ya kada ya afya dip niongeze utundu kidogo maana digrii ushindani mkubwa na hela ndefu imenishinda.
Soma clinical dentistry uwe mtoa Tiba

Lakini procedure za Dental technology ujifunze kwa vitendo yaani kutoka kwa wenye hiyo taaluma na kuhudhuria clinic
 
Mimi ni Clinical Officer nafikiri kutafuta kozi ndani ya kada ya afya dip niongeze utundu kidogo maana digrii ushindani mkubwa na hela ndefu imenishinda.
Kasome dermatology advance Diploma Muhimbili
 
Hiyo niliitamani ila vigezo vyake wanataka C.O aliyesoma nje sasa hapo tabu tupu nikishindwa nitaenda kusoma macho
Kasome dermatology advance Diploma Muhimbili
 
Nina Matokeo yafuatayao (2018)
Chemistry B
Biology A
Physics C
Maths C
Language A
Na 1 ya Point 13
Naomba ushauri juu ya course ya Afya ya kusoma kwa Mwaka 2022/2023. Lengo ni urahisi wa kujiajili na kipato cha kuridhisha katika Mradi husika.
Msaada tafadhali, Ahsanteni.
 
Pia naomba kusaidiwa naweza kupata Chuo MBEYA,KIBAHA,MTWARA,LUGALO,KILOSA,TANGA au Muhimbili? Na vp kuhisu Mwanza College?
 
Optometry, dental, Radiology.. ukikosa nenda medical lab, ukikosa kabisa nenda Nursing. Mwisho.
 
Radiology, optometry na Dental kwa diploma hizo kazi uhakika na value haishuki kwenye pesa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…