Kuharibika kwa Mimba: Fahamu Sababu, Kinga na Tiba za tatizo hili

Kajole

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
1,667
1,642

Habari wakuu,

Hili ni tatizo linalomkabiri mchumba wangu hvyo nimelileta kwenu kuomba msaada wenu. Tatizo lenyewe ni: alianza kusumbuliwa na maumivu ya mgongo hvyo tarehe 11/6 tukaenda kupima na akaonekana POSITIVE, mimba ipo. Lakini ajabu tarehe 9-13 mwezi wa 7 akaona siku zake kama kawaida.

Mwezi wa 8 hakupata siku zake kama ilivyotarajiwa yan kati ya tarehe 6-10 hvyo 2kaamua kupima nyumban na majibu yakawa POSITIVE, tukaenda hospitali kupima tena majibu yakawa yaleyale-ipo mimba lakini ajabu tena tarh baada ya wiki mbili, yaani tarehe 21/8 akaona siku zake japokuwa haikuwa ya kawaida kwani ilianza matone ya rangi ya zambarau na kisha mabonge mabonge na maumivu makali na ilidumu kwa siku tatu tu.

Tarehe 11/9 akapima tena hospital na akaambiwa ni NEGATIVE, haipo. Lakini anajisikia kuchoka pia kichefuchefu na anakojoa mara kwa mara. Ndugu zangu tusaidieni hili ni tatizo gani, anasumbuliwa na nini na tutatatua vipi hili tatizo?

Mungu awabariki sana.

BAADHI YA MASWALI YA WADAU WENGINE KUHUSU TATIZO HILI


BAADHI YA MICHANGO YA WADAU
 
Pole sana, subiri wataalam wanakuja natumaini watakusaidia.
 
Kwa maelezo yako,hiyo mimba ni kama imeshatoka mabonge ya damu na maumivu. Ingekuwa bleeding ndogo ndogo, uwezekano wa mimba upo.lakini mabonge ya damu na maumivu juu, ni kama mimba imeharibika, cha muhimu asichoke kwenda hospitali kupata uhakika zaidi.
 
Pole kaka. I experienced something similar to that a few months ago tofauti ni kuwa mimi sikuona period zangu kabisa. I went to three different doctors na wote walisema mimba inatoka sikuamini coz nilikuwa nableed kidogo kidogo(spot bleeding bila maumivu yoyote). Finally nilipata maumivu makali sana ya tumbo na nikafanyiwa D & C ikawa ndo mwisho wa habari. Nakushauri umpeleke huyo dada hospital mapema iwezekanavyo coz unavyoelezea ni kama mimba imeshatoka.
 
<br /> <br / Asante sana kwa ushauri wako mzuri na leo tutaenda tena hospital kwa uchunguzi zaidi japokuwa nakosa kuamini tena hospital maana napata majibu tofauti tofauti kwa the same problem.
 
Asante sana na ubarikiwe kwa maelezo yako,.leo natarajia kwenda hospital tena kwa uchunguzi zaidi.
 
Kajole,

Pole sana mkuu, pia mfikishie pole shemeji. Inatokea kwa wanawake wengi kupata kama damu ya hedhi akiwa na ujauzito mchanga (mwezi wa kwanza na/au wa pili), lakini huwa kidogo kiasi tu cha kustain chupi, na inaweza ikaendeana na siku zake za kawaida za hedhi au tofauti kidogo.

Lakini inapokuwa kiasi cha kutoa mabonge ikiambatana na maumivu makali ya tumbo la chini/uzazi...ni dhahiri hapo mimba inatoka na anahitaji kwenda hospitali haraka, aonwe na daktari wa magonjwa ya wanawake na amfanyie ultrasound kuhakikisha imetoka yote. Mimba zinapotoka zina tendency ya kubakiza uchafu kidogo (retained products of conception), na hizi husababisha bleeding kubwa sana ghafla au kwa muda mrefu. Na pia mimba nyingine haiwezi tunga mpaka hiyo product/uchafu utoke. Kama ipo basi atasafishwa (D & C), na hizo risk zote zitakuwa zimeondoka.
 
Asante sana na pole zimefika kwa shemeji yako,.leo tunatarajia kwenda hospital,ntarudi na feedback kuwajuza zaidi.
 
The same happened to my wife pole sana, hi hali inawatokea sana wanawake wakati wa mimba changa miezi 2-3. na kwa jinsi inavyo onekana ni kwamba mimba imekwishatoka (miscarage). Maumivu ya tumbo la chini na kutoa damu ya mabonge ni dalili za miscarage. Pole sana mkuu.
 
Kajole, bado hujaanza safari ya hosp? pole sana,wahi hosp na dr afanye yanayohitajika asije akapata maambukizi.wakati damu inaanza kutoka wakati akiwa mjamzto,alipaswa aambiewe cha kufanya.pengine alihitaji bed rest. msijali,mungu ndo mgawa baraka ya watoto.mtafanikiwa kwa wakati ambao sio wa kuchelewa wala wa kuwahi. kila la kheri.
 
Pole sana! wahi kwa madaktari bingwa wa kinamama hiyo mimba yaelekea imekwisha toka na asipowahi kuchekiwa itamletea madhara mengine, kawaone madaktari mapema usiogope garama za kuwaona okoa maisha ya mwenzi wako.
 
Tafadhali onana na dokta anayehusika na masuala ya uzazi kwa akina mama kwa ushauri na vipimo zaidi.
 
Pole ndugu yangu, wadau wote wametoa ushauri mzuri ambao utanisaidia na mimi pia maana mchumba ame-experience the same thing leo asubuhi na ilinifadhaisha sana nashukuru kwa ushauri ambao nimeupata kupitia ujumbe wako.
 
Jaman asanteni sana wote kwa ushaur na mawazo yenu ambayo kwa kweli ni constructive sana na yametupa faraja na kutupungua maumivu kwa kiasi fulani. Ok mchumba ndio ametoka hospitali na majibu aliyopewa ni haya: kapimwa na ni negative-HAKUNA MIMBA wala tatizo lolote tena ktk mwili wake maana yake imetoka na kuhusu maumivu na dalili nyingine ni kwamba atakuwa anakaribia kupata HEDHI nyingne tena yan anarudi ktk mzunguko wake wa kawaida.

Mungu awabariki sana na kiukweli JF ni mambo yoooote!
 
Mkuu,

Hao madaktari hawakumfanyia UTRASOUND mkeo inavyo onyesha tayari mkeo ameshapata abortion kulingana na maelezo yako. Lakini kama utaenda Hospital Fanya ultrasound, i mean lower abdominal ultrasound to check for uterus size and other things.

Pia wanaweza kucheck Viginal kwa sababu inaweza kuwa incomplete abortion, Na kama ni complete abortion wataangalia then itakuwa saafi kabisa na tatizo hilo ina sababu nyingi. Katika suala la kuchoka ni kutokana na loss of blood so anatakiwa kupata fluid ya kutosha kama replacement

Note Utrasound ndo confirmation test vingine miyeyusho tu.
 
&lt;br /&gt; &lt;br / Asante sana kwa ushauri wako mzuri na leo tutaenda tena hospital kwa uchunguzi zaidi japokuwa nakosa kuamini tena hospital maana napata majibu tofauti tofauti kwa the same problem
Nenda mkuu then usisahau kurudi ulete riport mkuu.
 
Nenda mkuu then usisahau kurudi ulete riport mkuu.

Dio, asante sana kwa yote pia nilienda jana hosp na feed back nimeandika hapo juu. Nimeeleza alichosema doctor,.kwa kifupi amesema kuwa hana tatizo lolote kwa sasa ila ni kweli mimba imetoka kama wachangiaji weng walivyoona.

Pia kuhusu kuchoka, maumivu ya kichwa, kukojoa mara kwa mara anadai ni kwa sababu anakaribia kupata hedhi nyngne na kurudi ktk mzungu wake wa kawaida. Tunawashukuru wanaJF wote kwa kweli mnafariji na kusaidia sana kwa michango yenu.
 
Mkuu Hao madaktari hawakumfanyia UTRASOUND? Note Utrasound ndo confirmation test vingine miyeyusho tu.[/QUOTE] Mkuu Rodcones, mi sielewi ni kwanin madaktar wote 2naoenda wanakwepa kupiga ultrasound, hata jana 2memueleza ni vizur kama atapgwa ultrasound akasema atatumia kipimo cha kawaida tu na kikishndwa kutoa matokeo ndo atapga ultrasound (2mekuwa 2kielezwa hvyo na zaidi ya madaktar 3 2liowaona).

But 2tapima kwa kipimo hcho tarh 20/9 pale KCMC maana 2natarajia kwenda huko kwa kazi nyingine hvyo 2tafanya na hilo. Nazidi kuwaombea baraka na moyo huo huo wa kusaidiana.
 
Hebu jiulize, kwa nini mimba huwa zinaharibika? Unaweza kukadiria, kwa siku moja ni mimba ngapi huwa zinaharibika? Ukienda kumuuliza mtaalamu yoyote wa tiba, atakutajia sababu nyingi sana zinazopelekea mimba kuharibika ikiwemo ile ya mimba kuharibika yenyewe au kuharibiwa kwa makusudi. Lakini bado jibu halijajibiwa, kwa nini iharibike yenyewe au iharibiwe? Je, kuharibu (kutoa) mimba kuna ubaya gani? Huo ubaya unaouona wewe, unafikiri huyo anayetoa hiyo mimba anauona pia? Kama hauoni kwa nini?

Je, ni kweli kilicho kibaya/kizuri kwako na kwa wengine kiko hivyo? Kwa nini?. Jiulize tena. Hivi kama kusingekuwa na kuharibika au kuharibiwa kwa mimba dunia ingekuwaje? Bila shaka ingekuwa imemalizika kutokana na wingi wa watu. Nasema hivyo kwa sababu, ukiangalia idadi ya mimba zinazoharibika na zinazoharibiwa kwa siku moja zinaweza kuwa sawa au ni nyingi kuliko idadi ya watoto wanaozaliwa kwa siku moja.

Lakini si mimba zote zinaweza kuharibika au kuharibiwa, kuna zingine huharibika kirahisi sana hata kama mwenye nayo ataitunza kama yai, kuna zingine huharibiwa kirahisi sana hata kwa kunywa dose ya kawaida ya dawa au kwa kufanya kazi nzito kidogo, unafikiri ni kwa nini? Mfano; mama anaweza akawa anafanya kazi nzito kila siku, akanywa dawa za kila aina au akatumia kila njia kuharibu mimba aliyonayo ikiwemo ile ya kwenda kwa madaktari lakini mimba isiharibike, unafikiri ni kwa nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…