Kufungwa kwa Sahara Media liwe funzo kwa machawa, Dialo alijua akiwa CCM atakwepa kodi milele ila Hayati Magufuli alimshenyenta

Kufungwa kwa Sahara Media liwe funzo kwa machawa, Dialo alijua akiwa CCM atakwepa kodi milele ila Hayati Magufuli alimshenyenta

Sifi Leo

Platinum Member
Joined
Mar 30, 2012
Posts
5,937
Reaction score
10,815
Nchi YETU ya Tanzania imebarikiwa sana kuwa na MACHAWA ambao kwa namna Moja au nyingine huchangia sana tabaka tawala kututawala watakavyo wakiamini ya kuwa wao ni sehemu ya watawala hao.

Hapa nataka nieleweke, watu kama akina Pascal Mayalla walikuwa ni MACHAWA wa Taasisi mbalimbali za serikali hata zile zilizotangazwa kuiingizia hasara serikali lakini inapofika Taasisi hizo zina tafrija fulani basi wanaalikwa watu kama akina Pascal Mayalla na vyombo vyao wanatangaza mambo ya kichawa chawa huku wanalipwa fedha za UMMA Ili kuwapaka mafuta kwa mgongo wanini kama wasemavyo waswahili.

Alipokuja Rais ambae yeye uchawa ulikuwa na mipaka watu kama hao waliishia kufirisiwa Ili likae hivyo na lieleweke hawakufilisiwa Hawa walikuwa wakwepa Kodi.

Utawala wa Magufuli uliwatikisa sana wenye viti wa ccm mikoa mbalimbali ambao wengi wao walikuwa wafanya biashara.
Moja ya makada waliotikiswa ni Anthony Dialo,huyu maisha yake mengi alikuwa mkwepa Kodi hii iliyotangaswa anadaiwa Leo hii sio aliyokuwa anadaiwa aliuza Mali zake nyingi KULIPA limbikizo la Kodi ambalo hakulitegemea kamwe kisa yeye ni ccm

Leo kampuni yake inafungwa kisa uchawa ni television yake iliangaliwa kwa wingi na watu wa Kanda ya ziwa enzi za kampeni Sasa Kiko wapi?
 
Tujikite hapo kwenye kichwa cha habari.
Kufungwa kwa Sahara media LIWE FUNZO kwa MACHAWA, Dialo alijua akiwa ccm atakwepa Kodi MILELE ila Mzee MAGU alimshenyenta
 
Sahara imefungwa kwa kukosa mapato, vipindi havivutii, wafanyakazi elimu ndogo,ubunifu hakuna
 
Isije kuwa amefanyiwa zengwe ili yule mzee wa media za africa mashariki aipate na hii kirahisi.
 
Back
Top Bottom