Accidental Genius
Senior Member
- Aug 17, 2019
- 154
- 188
Bwana asifiwe wapendwa.
Tunamshkuru Mungu Ni siku nyingine tuko mbele zake, Ni kwa neema yake tu tunaiona siku ya Leo.
Neno la Mungu leo linatupa tumaini kuwa tukiwa tumempokea Yesu Kristo na kumuamini anatulinda na kutuzungushia ulinzi wake kama mboni ya jicho lake.
Hatuna haja ya kuhofia maana ametuzingira kwa boma la Moto wa Roho mtakatifu hakuna awezaye kutugusa.
Jizungushe wewe na familia yako kwa damu ya Yesu Kristo na Moto wa mtakatifu na ukiri moyoni mwako hakuna wa kutugusa sisi ktk jina la Yesu Kristo.
Zekaria 2:
5 Kwa maana mimi, asema Bwana, nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote, nami nitakuwa huo utukufu ndani yake.
8 Kwa maana Bwana wa majeshi asema hivi, Ili nitafute utukufu amenituma kwa mataifa wale waliowateka ninyi; maana yeye awagusaye ninyi aigusa mboni ya jicho lake.
9 Kwa maana, tazama, nitatikisa mkono wangu juu yao, nao watakuwa mateka ya hao waliowatumikia; nanyi mtajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma.
10 Imba, ufurahi, Ee binti Sayuni; maana, tazama, ninakuja, nami nitakaa kati yako, asema Bwana.
11 Na mataifa mengi watajiunga na Bwana katika siku ile, nao watakuwa watu wangu; nami nitakaa kati yako, nawe utajua ya kuwa Bwana wa majeshi amenituma kwako.
BARIKIWA