Kufanya malipo/manunuzi kupitia mitandao ya simu

Kufanya malipo/manunuzi kupitia mitandao ya simu

ukweni

Member
Joined
Jul 13, 2018
Posts
11
Reaction score
12
Kumekuwa na kero kubwa sana pale, mfano mtu unanunua LUKU kupitia mtandao wa simu, unaanza kufanya mwamala kuanzia hatua ya kwanza hadi ya mwisho na kupata ujumbe kama 'mwamala wako unashughiliwa utapokea uthibitisho hivi punde'. Ukishapata huo ujumbe, hupati tena huo uthibitisho hadi upige simu kampuni husika na kuishia kuambiwa 'kuna shida ya mawasiliano suala lako linashughulikiwa'. Sioni kwa nini haya makampuni ya simu yasimfahamishe mteja kabla hajamaliza kufanya mwamala kwamba kuna tatizo la mawasiliano ili mteja atafute namna nyingine ya kununua LUKU badala ya kusubiri hadi amalize utaratibu wa manunuzi na kumkata pesa yake halafu asipate huduma aliyoinunua?
 
We ungesema directly mtandao uliotumia na ukakuletea shida na wakati gani. Umegeneralise wakati uhalisia hauko hivyo ingawa kuna inconveniences sometimes.
 
Back
Top Bottom