Kuelekea uchaguzi

Kuelekea uchaguzi

totoo brst

Member
Joined
Jun 3, 2014
Posts
85
Reaction score
22
MAGUFULI NA CCM WAKATAA RASMI KURA ZA WAKRISTO BAADA YA KUWASEMA VIONGOZI WAKIKRISTO HADHARANI
Na Fandre

Katika takwimu za dunia na ambazo zimejaa kwenye tafiti nyingi maarufu duniani zinaonyesha ya kuwa kuna dini kubwa tano tu dunaini ambazo zimekadiriwa kuwa na waumini kama ifuatavyo:
•Christianity: 2.1 billion.
•Islam: 1.3 billion.
•Hinduism: 900 million.
•Buddhism: 376 million.
•Sikhism: 23 million.
•Judaism: 14 million.


Source: World Religions for Children - Primary Homework Help
World Religions for Children


Takwimu hizi zinaungwa mkono na mashirika mengi binafsi na ya kiserikali kwani zinatoa picha halisi juu ya mgawanyiko wa taasisi za kidini duniani huku Uislam ukiwa umeenea zaidi na kuwa ndio dini kubwa sana na yenye nguvu katika ukanda wa Mashariki ya Kati na Arabia. Kwahiyo kwa lugha nyepesi kabisa ni kuwa; Dini kubwa mbili za ulimwengu ni Ukristo na Uislam huku wakriso wakiwa na idadi kubwa ya waumini kulinganisha na waislam.

Maana halisi ya maneno yangu ni kuwa, kwa sehemu kubwa makundi haya mawili ndio yenye nguvu kubwa ya kuamua juu ya nani awe nani na yupi asimame wapi pale panapokuwa na umoja kati yao na utenganifu kati yao maana yake ni kuwa basi lazima upande mmoja uibuke kidedea kutokana na wingi wa waumini ulionao kama hakutakuwa na mabadiliko yeyote yanayoweza kubadili taswira halisi.

SASA, kwa kipindi cha siku za hivi karibuni tokea siku ya tarehe 03/10/2015 mpaka siku ya tarehe 05/10/2015 katika kampeni zake Bw. Magufuli(Mgombea Urais wa CCM) akiwa pamoja na Bw. Abdallah Bulembo(Mwenyekiti wa Wazazi CCM) wameonekana dhahiri wakisema HAWAZIHITAJI KURA ZOTE ZA WAKRISTO NCHINI.

Lakini hawakuishia hapo wakaenda mbali zaidi na kuwasema viongozi wa dini wanaomuunga mkono mgombea Urais wa CHADEMA na anayeungwa mkono na vyama vinavyounda UKAWA huku akisahahu ya kuwa yeye pia ni muumini wa dini ya kikristo HAIKUTOSHA bado aliamua kutumia majukwaa ya kisiasa pamoja na mwenzake kuwasema vibaya viongozi wa dini ya kikristo na kuwakatisha tamaa waumini wao pamoja na wananchi wanaowaunga mkono viongozi hao wa dini wenye kupendwa na kukubalika sana nchini kwa sasa kutokana na misimamo yao juu ya masuala mbalimbali nchini.

Ikumbukwe, Sula la imani ni suala linalogusa sana hisia ambazo katika hali ya kawiada huwezi kuzipima na kujua ukubwa wake ama mtu anamiliki hisia kiasi gani juu ya ile imani ya dini ambayo yeye ni muumini.
Pili, imani hizi kubwa za wakristo na waislamu zimegawanyika katika makundi madogo madogo yanayoitwa MADHEHEBU lakini mwisho wa siku wao wote wakikutana tutawaita ama WAKRISTO au WAISLAMU.

Sasa unapoamua kuwasema viongozi wa dini tena hadharani pasipo kuona haya ya maneno unayoyasema tena ukirusha Live kutoka kwenye majukwaa ya siasa za kitaifa unakuwa unajenga CHUKI isiyokwama baina ya Waumini wa kiongozi husika wa kidini(kiroho) pamoja Chama cha kisiasa kwa kujitambulisha kwao kuwa wewe ni adui yao wa wazi.

Lakini, kama umeweza kumsema kiongozi mmoja wa dini hadharani na kumkashifu kwa maneno yasiyofaa ukidhani unafurahiwa na jamii kubwa ya kitanzania ina maana yakwamba hata kesho utakapopata nafasi yakuwa rais utaweza kuwaonea na kuwasema vizuri viongozi wengine wote wa kidini pasipo kuwaonea haya.

Watanzania wote tunaamini katiika siasa safi na zisizo na chuki ndani yake kwani mwisho wa siku baada ya Uchaguzi tutabaki kuwa watanzania na sio watu wa CCM wala wa UKAWA kwahiyo tabia ya kuwasmea vibaya viongozi wa dini huku mkiwanyima uhuru wa kuongea wala kujihusisha na siasa ni jambo la kipuuzi, kijinga na lisiloungwa mkono na mtu yeyote mwenye akili timamu kwani kufanya hivyo ndio mwanzo wa kuzalisha vizazi vyenye chuki na hasira zisizokoma kwa CCM kama ambavyo ilivyo sasa.

Ikumbukwe wakristo wote wana jukwaaa lao ambao linwaunganisha na kuwa chombo kimoja na Kiongozi wa dini aliyesemwa na kuambiwa maneno mabaya naye ni mjumbe katika chombo hiko kinachounda baraza hilo la wakristo nchini sasa kuamua kumsema vibaya ni kuamua kuwasema wakristo wote na viongozi wote wa baraza hilo kuwa nao hawafai na hawana thamani yeyote katika safari yako.

Kama leo ameweza kusemwa kiongozi huyu wa dini na Bw. Magufuli pamoja na Bulembo ambao kwa pamoja ndio CCM yenyewe, Je itashindikanaje kesho kuwasema viongozi wengine wa dini katika Taifa?

NI MUDA SASA TUNAHITAJI MABADILIKO YA KWELI, MABADILIKO YATAKAYOFANYA TUHESHIMIANE NA PIA TUHESHIMU MAKUNDI YOTE KATIKA JAMII IKIWEMO VIONGOZI WETU WA KIDINI.


Ndugu zangu Wakristo na Waislamu nawasihi sana tuiondoe CCM katika dola kwani imekosa heshima na muelekeo wa kuliongoza taifa hili na kuleta umoja kama zamani. Itakua ni aibu kwa taifa la Tanzania kuongozwa na Magufuli mtu ambaye anaweza kumtukana baba yake alafu akasema anampenda mama yake, HUU NI UONGO WA WAZI. Kuwadharirisha viongozi wetu wa kidini ni dhambi isiyosameheka mpaka pale itakapoombewa msamaha hadharani kama ambavyo aliamua kumdharirisha kiongozi huyo hadharani.

Magufuli na Bulembo kuanzia Singida hadi Arusha wamekuwa wakitudhihirishia kuwa wao hawahitaji kura za wakristo hata kidogo ndio maana wamekuwa tayari kuwakejeli viongozi wetu wa kidini hadharani, hivyo basi nawaombeni ndugu zangu tumpigie kura kwa wingi ndugu yetu Edward Lowassa ambaye ameonekana kuwajali viongozi wa kidini huku akiamini kuanza na Mungu na kumaliza na Mungu.

Tukumbuke idadi ya misikiti na makanisa ambayo Mh. Lowassa ameshiriki kuyajenga, kukarabati na hata kufika kushiriki ibada pamoja na waumini. Tunaumbuka vyema Msikiti wa Kinondoni ulivyoungua moto Mh. Lowassa alikuwa wa kwanza kufika na kuchangia pesa nyingi za ukarabati wa Msikiti ule maarufu nchini. Ni muda sasa umefika wa kumuweka madarakani kiongozi anayejali wananchi pampja na kujali imani zao na viongzoi wao wa kidini.

Mbali na kuwakemea vikali Bw. Magufuli na mwenzake Bulembo ninaomba watanzania wote tumuunge mkono Mh. Edward Lowassa katika siku ya tarehe 25/10/2015 kwa KUMPIGIA KURA YA NDIO kwani ameonyesha yeye ni mkomavu katika siasa kwa kujikita katika siasa safi zisizo za chuki wala kuwasema wapinzani wake ila kuelezea ilani ya chama chake na kutoa ahadi zake toafauti na alivyo huyu mwingine ambaye mpaka sasa anatilia shaka kama atakuwa rais maana ana kundi kubwa la washauri wabovu na wasiojua maana ya siasa za kistaarabu kwa manufaa ya taifa ila kueneza chuki na matusi tu majukwaani.


Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Wabariki wana Mabadiliko.
 
Back
Top Bottom