Kuelekea hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika JS Saoura dhidi ya Simba SC, Show ya Kibabe!

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,263
Wawakilishi pekee Tanzania na Afrika Mashariki na mabingwa wa Nchi, Simba SC, Mnyama wanatarajiwa kuondoka jioni hii kwenda nchini Algeria kupitia Dubai, UAE, kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura utakaochezwa siku ya Jumamosi Machi 9, 2019 kwenye uwanja wa Aout 1955 Bechar mjini Bechar Algeria.

•••Mwana Kulipewa..Mwana Kulitaka

Mtendaji mkuu wa Simba SC, Lunyasi Crescentius Magori, amesema kuwa uongozi umejipanga vizuri na kuweka mikakati ya kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huo ikiwa pamoja na kutoa ahadi ya fedha kwa wachezaji endapo watawafunga waalgeria kwao.

Alisema Bodi ya klabu ya Simba SC, imekaa na Kocha Patrick Aussems kwa ajili ya kumweleza mchezo wetu dhidi ya JS Saoura kuhakikisha wanakuwa makini na kufanyia kazi makosa yaliyojitokeza kuwa hayajirudii tena ili klabu iweze kupata ushindi ama kutoka sare ili tuweze kukaa katika mazingira ya mazuri ya kuingia robo fainali na kuendelea kupeperusha bendera ya Tanzania.

•••Show ya Kibabe Kituo Kinachofuata ni Algeria.

Wanachama, Mashabiki Kindakindaki wa Simba SC ndani JF OKW BOBAN SUNZU King Ngwaba Shunie Sapta Sapta barafuyamoto Tui sembo Jaby'z nyakubonga Mshuza2 Kinyungu, tunaamini Simba SC inaweza kupata matokeo chanya hata kama tupo ugenini kwasababu mpira ni dakika 90' na lolote linaweza kutokea uwanjani.

Tutaendelea kukujuza zaidi hapa hapa, usibonyeze kitufe...This Is Simba SC Mnyama..NguvuMoja

Update;

Simba imesafiri kutoka mji Algeris nakuelekea mji wa Bechar Algeria ambapo ndipo utapigwa mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Js Saoura kesho saa 4: 00 usiku..This Is Simba...NguvuMoja.

IMG_20190305_124614_710.jpeg
IMG_20190305_124531_690.jpeg
 
Hv caf wamebadili ratiba? Maana ilikuwa mkipige na wale vijana wa kongo fc vita.
 
Back
Top Bottom