Kuelekea 9 Desemba.....

Omary Ndama

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2017
Posts
3,367
Reaction score
4,074
RAIS MAGUFULI ANAHITAJI KUOMBEWA, TUMUOMBEE!!

Nimesikiliza hotuba ya Rais Magufuli, ile ya Ikulu kuhusu siku ya Uhuru wa Tanganyika. Nimeitazama tena na tena ile video, kila nilipoirejea nilipata picha hiyohiyo, "Rais anahitaji kuombewa".

Nimefanikiwa kumtizama vizuri Ndg. Rais, kupitia miwani yake ya mviringo isio na rangi nimefanikiwa kuyaona macho yake, sio yake. Uangavu wake umepungua mno, nuru usoni imepotea!

Sauti yake si ile ambayo nilizoea kuisikia mara kadhaa, inasikika ikitoka ktk kifua kilichojaa mno, kifua chenye makubwa. Ninahisi Rais wangu ana maumivu makubwa, kwa vyovyote vile liko jambo linamtatiza zaidi. Tumuombeeni jamani!!

Hata pale alipolazimisha tabasamu, bado hakufanikiwa. Limefifia mno, huyu sio yule JPM aliekuwa akitangaza ununuzi wa korosho hivi majuzi, sio yeye. Huyu vita ya Uchumi imemkabiri kwelikweli na inavoonekana ni kama amebakia pekee.Tumuombeeni Rais!!

Rais anasema Nchi ipo ktk vita lkn no one cares. Ukiisikiliza kwa makini sauti ya Ndg. Rais akituomba tuache maneno maneno, inaumiza! Rais alizoea kusema Serikali yake(Yangu) ameona haeleweki, kwa mara ya kwanza nauona unyonge wa Rais wangu!
Rais anasema "iungeni mkono Serikali yenu", neno yangu amelitoa, halipo. Rais amekubali yaishe ili apate ushirikiano ktk vita hii. Rais ameumizwa na ameumia kwelikweli "Tumuombee!"

Wakati wote wa Hotuba ile, Rais amejitahidi kuangalia huku na kule kubadili uelekeo ili kama unamsoma ukose jibu lkn wapi. Imegoma plan. Wenye timamu tumeona, tumeelewa kuwa Rais anajambo kubwa zaidi linamhangaisha. Yale maneno sio mepesi, pale yupo Ikulu. Kwa maneno yale Rais ametangaza Vita. "Tumuombee!"

Nimevaa viatu vyake, kama mtoto nikamfanya kuwa mzazi wangu, kweli nimeumia. Kwa mara ya kwanza namuona Rais akishindwa kuficha maumivu. Amejitahidi sana lkn macho yamekataa katakata, sauti imemgomea kabisa! Pengine ni udhaifu wangu ktk kuchambua mambo, lkn nimefanya vizuri ktk fasihi huko nilikopita. Nina uhakika JPM ana maumivu makubwa, Vita imekua kubwa pengine kuliko alivyoitarajia. "Tumuombeeni jamani".

Ukipata nafasi itafute video hiyo ya Ikulu. Nadhani ni ya juzi tarehe 07.12. 2018, Rais akizungumza na Taifa kuhusu Siku ya Uhuru. Ktk video hiyo, Rais ametangaza mambo mawili makubwa kama Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu. Mosi, ameitangaza tarehe 09.12.2018 kuwa siku ya mapumziko. Pili, ametangaza Vita ya Kiuchumi, ameitangazia Dunia kuwa Tanzania ipo ktk Vita, vita ya kiuchumi lkn Watanzania bado wamelala fofofo.

Kuna watu wanaweza kuwa hawajui uzito wa kauli hiyo ya Rais. Tofauti ya kauli hii na ile ya Nyerere mwaka 78, ni moja tu. Vita ya Nyerere ilipiganwa field hii ya Magufuli inapiganwa Ikulu. Zote ni vita kwa uzito uleule!! Wasiojua, kumbukumbu kuanzia jana zinaonesha Marais waliotangaza vita kuwa wawili tu, yaani Nyerere na huyu. Mmoja vita ya Bunduki, mwingine Vita ya Uchumi. Rais anatangaza vita, Wananchi wanasema "Kazi na Bata". Inauma sana, "Tumuombee!"

Jumapili njema...
 
Hahaa sio wananchi waliosema kazi na bata sijui bata batani ni mh Zito zuberi Kabwe

Au Membe kusemwa atawania uraisi 2020 ndio chanzo? Yajayo yanasikitisha vip kuhusu ujenzi wa bandari ya bagamoyo?

Hii vita labda ni kati ya mmarekani na mchina ndani ya ikulu ya Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…