Kuelekea 2020

Kuelekea 2020

Salim A. Msangi

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2011
Posts
566
Reaction score
511
Salaam wanajamvi ...

Uchambuzi kuelekea 2020

Kwenye hii safari mengi yatatokea na kuonekana ... mengi yatashangaza kama yalivyo kwisha anza sasa..

Lakini kabla ya kufika 2020 turudi 2015...

Pamoja na madhaifu makubwa waliyokuwa nayo ccm kabla ya 2015 ... lakini bado hapa kuonekana kwa upande wa upinzani kuwa na 'upinzani' imara wa kuiangusha ccm. Kazi kubwa aliyoifanya Kinana na Nape kuelekea kipindi hicho kiasi fulani ilirudisha hamasa ya ccm kwa wanachi ... lakini hilo likiendelea kikaja kile kilicho itwa 'ukawa' ... hili lilionekana kuwapa nguvu wa pinzani, lakini ukawa kwa 'upinzani' ilikuwa ni sawa na kuokota 'dodo' chini ya mnazi .. hawakuwa na malengo yeyote ya pamoja kwenye 'ukawa' zaidi ya katiba, kama walikuwa wanabeep vile mara wakaona mbona ukawa inalipa kwanini tusiende nayo kwenye uchaguzi. Kumbuka hawakuwa na 'work plan' yoyote, mipango ilikuja baada ya tukio au muda mfupi kabla ya tukio na kwenye suala tete na pana kama hili la uchaguzi mkuu, mipango ya namna hii ilikuwa ni danganya toto. Lakini Mungu si Athumani ngoma ya ukawa ikawa ngoma na kuicheza shurti uwe mjuzi ... mh! CCM wakaanza kukuna vichwa!

Kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa uchaguzi wa vyama vingi, 'roho' thabiti ya kuungana kwa vichwa 'hasimu' vya upinzani ikaanza kusimama ... Pale Dr. Slaa, huku Lipumba, kule Mbowe, hapa Shariff kule Mbatia na wengine na wengine ... wote ndani chungu kimoja na wako tayari kuelekea magogoni ... we! ilikuwa mshikemshike. Kwa mara yakwanza ukiachana upinzani 'fake' wa Mrema wa mwaka 1995 CCM ilikuwa inakabiliwa na hatari ambayo haikupata kuitarajia kamwe! Hamasa ilikuwa kubwa kuliko kwa wananchi ... ishu ilibaki jina litajwe kutoka kwa vigogo wa upinzani kazi iyanze ... majina hatari ilikuwa Lipumba na Dr. Slaa kwa upande wa bara, visiwani tunamjua hakuwa na mpinzani .... aridhi ya ahadi mbele ya macho yetu .. ile pale tushaiyona ... kile walicho kuwa wakikitaka kwa beo yoyote tangu kuanza kwa vyama vingi kilikuwa mbele yao ... na hapakuonekana na kikwazo chochote kile .. ilikuwa ni suala la muda tu ... huu ulikuwa upepo wa katiba, ulibeba kila ulicho kikuta njiani .....

Then something happen ... 'wapinzani' wakawa wanasita kutaja majina ya mgombea ... mh! Wenye akili zetu tukajua kumesha haribika ... hata iweje kwanini wapinzani walisubiri ccm ipitishe mgombea wake ndiye wamtangaze wakwao? Mh! Sababu haijalishi nani ccm wangemsimamisha upinzani wa ule ulio onekana wa 'ukawa' ulikuwa na nguvu ya kumgaragaza yoyote yule! Lakini kwanini basi walisita kumtangaza mgombea wao?

CCM kwenyewe moja ilikuwa haikai wala mbili haikai .. jina lilikuwa ni moja tu Lowassa!
Ila chini ya kapeti kulikuwa na upepo mwingine ulikuwa unaimba nyimbo tofauti ... nani mwingine ukiacha Lowassa haijulikani..
Benchi la ufundi ccm ikaja na suprise nyingine matata ... ikaruhusu kila anayejihisi anaweza kucheza akachukue fomu ... chezea mikakati wewe ... sababu jina lilikuwa ni moja Lowassa, endapo lingeisimama jina jingine linalo karibiana na nguvu ya Lowassa jina hilo lingewekwa matatani na 'wanamtandao' sasa tunamfichaje mwali wetu ... isiwe tabu kwenye msafara wa mamba na kenge wamo ruhusu kila mtu achukue, mpaka ijulikane nani 'mamba' nani 'kenge' game imeisha!

'Ukawa' bado tunasubiri jina litangazwe ... hatujui kwanini ... halafu lililokuwa likisemwa likatokea ... jina likakatwa! Ikawa taharuki na mshikemshike ndani ya wana mtandao, inawezekana vipi, kwa vipi, kwa faida ya nani? Hapakuwa na majibu mepesi lakini jina lilikuwa limesha katwa! Mchezo ukawa hatari zaidi na mgumu ndani ya ccm na huku 'ukawa' kukianza minong'ono ya kupokea jiwe la pembeni alilolikataa mwashi. Kule kijana machachari aliye wachomoka Chadema kwa staili yake ya kipekee 'Zitto Kabwe na chama chake kipya naye akaanza kuvuma sasa, labda muheshimiwa ACT ndiyo ilikuwa plan B yake, lakini wenye akili tulijua haiwezi kuwa hivyo ... hata kama yanayo semwa yangekuwa yana ukweli ACT kilikuwa kichanga mno kuhimili mikimiki ya uchaguzi mkuu ... na nguvu ya muheshimiwa na jeshi lake kama atachagua kwenda ACT ungekuwa mwanzo na mwisho kwa Zitto Kabwe kung'aa kwenye nyanja za kisiasa, sababu angefunika mpaka tusijua nani mgeni nani mwenyeji ... mwenyewe kimkakati hakusimama kugombea urasi sababu alijua chama chake bado kichanga na angevuja nguvu mapema wakati badi anasafari ndefu .. ndiyo akamtanguliza yule mwanamama ... nadhani plani ilikuwa ni 2020 ila kwa game ilivyo sijui ngoma imekaa vibaya sababu staili ya awamu hii ACT inazidi kuonekana bado changa na kwa Zitto itakuwa yaleyale aliyo yakataa 2015 ... lakini hatujui ya Mola mengi huendi ikazaliwa 'new Ukawa' ... sijui nasema tu.

Halafu usiyemtaka kaja ... jama sijui alifikiria nini kutunga wimbo huu ... Lowassa ndani ya Ukawa aka Chadema ! Halafu maajabu yakatokea .. wenye nyumba wakamuachia mgeni nyumba na kusepa! Ilikuwa joto kali ndani ya chadema halafu Ukawa yote. Dr. Slaa akafungasha virago ... maajabu zaidi ya kaja kumbe Slaa ni CCM ... Mh! Hii game mbona haieleweki ... kama kawa wenye akili tulijua na bado tunajua hakuna upinzani Tanzania ... hakuna hasa kwenye vyama vikongwe vya upinzani .... tutakumbuka wengi wa walio kwenda kuanzisha vyama vya upinzani walikuwa ni wana- ccm ambao walilazimisha kwenda kuunda upinzani kuridhisha matakwa ya mabwana wakubwa, wengi waliendelea kubaki na kadi zao na kuzilipia miaka ya kutosha! Wafya Chama wa Chadema wakashangaa Dr. ni CCM .... Halafu Lipumba naye akasepa! Mh!
Yaani bado hatua mbili, kufika kwenye kituo cha mwisho cha safari yako, anaamua kushuka kwenye gari! Hii ilishangaza wengi ... miaka yote wapinzani si walikuwa wanatafuta fursa hii na sasa iko mbele ya macho yao iweje sasa kwenye hatua ya mwisho kabisa wanaondoka .... hii ilikuwa ngumu kumeza.
Mtu kama Lipumba na Slaa walikuwa na ushaiwshi mkubwa mno kwenye vyama vyao na Ukawa kwa ujumla ... kitendo cha wao kuondoka ile ndoto ya upinzani kuingia ikulu ikafa na kuzikwa pale pale .... kilichokuwa kinawapeleka 'UKAWA' ikulu ni hamasa ya wanachi kuona kwamba sasa 'mwarobaini' wa ccm umepatikana, hii hamasa nyuma ya hayo majina makubwa ... na lau majina hayo yangeendelea kubaki pamoja na yote yaliyo tokea bado CCM ingekuwa na hali mbaya kuliko ....

Kuondoka kwa majina yale na kwa mgeni kukabiziwa nyumba ile, imani ya wanachi kwa 'ukawa' ikapungua ... watu kama Lissu walipokuja na kauli za kuyameza matapishi yao ndiyo kabisa nyumba ya chadema na 'ukawa' kwa ujumla ikazidi kuvurugika...

Kabla mgeni hajaondoka kwenda Chadema unakumbuka kulikuwa na 'mamba' na 'kenge' kwenye ule msafara ... na msafara ulivyo kuwa mkubwa ilishindwa kujulikana mapema nani ni nani ... wanamtandao wakatengeneza la kwao baada ya kumjua 'mamba' ni yupi kwenye msafara, 'on the spot' wakamuharibia na yeye nje ... hii inaitwa mwaga mboga ni mwage ugali .... halafu jamaa huyo akasepa zake ...

Mwenye 'bahati' akajiokotea dodo lake kiulainiii .... chini ya mnazi!

Swali likawa Lowassa kaenda Chadema katumwa au kaenda kwa maslahi yake binafsi ya kutimiza ndoto? Suala hili litajibiwa na muda! Lakini tangu alipokuwa huko hapakuonekana ule upinzani wa wa kujitoa muahanga na siku zilivyo kwenda na hasa baada ya uchaguzi Chasema na Ukawa wakwa ni wagonjwa wanao dhoofika taratibu ...

Je ilikuwa ni mkakati wa CCM Lowassa kwenda Ukawa au ni 'personal' ya muheshimiwa mwenyewe?
Kama ilikuwa ni 'move' ya CCM basi hii itakuwa ni moja of the best move, CCM kuwahi kufanya dhidi ya upinzani ... sababu joto la UKAWA halikuwa la kumuacha mtu salama ... muungano wa vile vichwa ndani ya UKAWA kaburi la CCM lilikuwa linasubiri kufikiwa na CCM ndani.............
Lakini CCM ile na vurugu zake ni wapi lilikua wazo hilo ni wapi lilikuwa ' entertained ' na nani mpaka iwe ni 'move' ya chama, MAZINGIRA YALIKUWA HAYARUHUSU, hasa ukianali nguvu, hamasa, ushawishi na gharama ambazo muheshimiwa alianza kuziingia mapema kabisa ili kujihakikishia nafasi hiyo, iweje tena yeye ndiyo akubali kuwa 'mbuzi wa kafara'? Bado haiingii akilini kama ilikuwa ni move ya chama.

Kama haikuwa ni move ya chama basi Lowassa kwenda Chadema na Ukawa yake ukuliitoa CCM kaburini ... adui yako muombee njaa ati! Vita vya panzi furaha ya kunguru ... UKAWA ilisambaratika, Chadema ikapoteza muelekeo na upinzani halisi ambao CCM angekutana nao ukafa! Hapa Lowassa kama ilikuwa ni Personal haikumfaidisha yeye ... lakini ilikiokoa chama alichotoka!

Ushawahi soma Novel Moja, ya mtu anaitwa Ben R. Mtobwa, 'Nyuma ya Mapazia' ikizungumzia uchaguzi wa 1995 ... kuna mahala panasema pa kimaanisha kuwa ni maneno ya mwalimu kuwaambia vijana wake na wengiene wasikie kuwa 'hawezi kumpa mbwa nchi ..' maneno hayo inamaana alikuwa akimbaiwa Mrema. Kwamba pamoja na nguvu na ushawishi na kila kile mabacho kilionekana kwamba Mrema anaenda kuwa Rais, palihitaji baraka ya mtu mmoja kulifanya hilo kuwa ndilo, na mtu huyo kesha kataa, kwamba hawezi fanya hivyo. Hivyo kinacho hitajika ni zaidi ya kura kwa mgombea kukabidhiwa ikulu, na hasa ikiwa natoka upinzani.

Sasa najiuliza na 'smrtness' ya Lowassa na muda aliyo itumikia ccm na serikali zake hakuona kwamba inahitaji zaidi ya kura kuingi ikulu kupitia upinzani? Nini basi kilimpeleka kule ... au suala la kwenda ikuli lilimfanya apite beyound reason capacity yake kutimiliza ndoto yake? Kama ilikuwa ni personal move, basi kwa upande wake haikuwa smart move, ingawa kwa uapnde wa chama ilikuwa ni move ya dhahabu.

Sasa gari 'linaonekana' haliendi ... hali tete na 2020 hiyo hapo ... karata zinaanza kuchangwa. Safari hii karata zenye mvuto ni zile za rangi ya njano na kijani, kila mtu anatupia jicho namna zinavyo changwa na kuchangnywa ... kama kawa tetesi au hamu za watu zinaogeuka kuwa maneno na maneno kuwa vitu halisi zimeanza ... karata zinachangwa makundi mawili tofauti kwa malengo tofauti .... halafu Paaa! Muheshimiwa karudi kundini ... halafu paaa! Huyu kapelekwa kule na yule karudishwa huku .... Mh! ni matokea ya kucnga karata hayo au kuna jingine ... Je muheshimiwa karudi kwenye kundi lipi kati ya mawili haya ... Mh! Hizi habari nzito mi sijui 2020 safari imeanzaa ....

Watu wanasema muheshimiwa kasepa sababu ya Lissu!

Lissu huyu huyu au mwingine ...? Credibility ya Lissu ilishuka sana kipindi alicho mpokea muheshimiwa ndani ya chama na kumkingia kifua na kuanza kumeza matapishi yake, ilimradi credibility ya chama kizima iliporomoka na watu machachari ndani ya Chadema wote wakaufyata ... kimya ... ikawa watu wanakwenda akwa matukio. Leo hiyo Credibility ya Lissu inatoka wapi? Unatak kuniambia Lissu ananguvu kushinda aliyo kuwa nayo Slaa kabla ya 2015?
Lakini Slaa hakuweza kuuzima upepo wa muheshimiwa aliondoka na kumuachia muheshimiwa ... leo vp Lissu awe na nguvu ya kumtisha muheshimiwa mpaka amkimbie .. au ndo kujipa matumaini huko?

Move ya muheshimiwa kurudi kundini inayo maswali kama yale yale iliyo yazua wakati anakihama chama, kwamba ni Personal au ni move ya chama, na hapa si semi Chadema bali chama anacho kwenda.
Mi naona ni ule mtindo wa kuchanga karata sasa umeanza ... hii move ilianzia mbali kidogo haya ni matokeo, inawezekana baada tu ya uchaguzi mafaili yalianza kupangwa upya ... tukaona watu fulani wa karibu na muheshimiwa mmoja mmoja wakirudi kundini na kupokelewa na kusamehewa .. hapo upepo ulianza kubadilika. Huku upinzani muheshimiwa kama kakiweka chama mfukoni na ushawishi wa chama ukizidi kupungua kwa wafuasi wake.

Halafu watu fulani wa karibu na muheshimiwa wakaanza kuonekana pale magogoni ... mh! Mara muheshimiwa na yeye ndani, magogoni, picha za kutosha ... sifia sana ... halafu huyoooo ..... watu tuko; Mh! tunaguna guna tu.

Halafu mara 'mwenye' chama chake ndani .... wakati mwingine nahisi kama mwenye chama chake alikuwa naijua hii move kama hakuwa 'part' ya hii move, huku mara paaa! muheshimiwa kaondoka, halafu kule mwenye chama chake anaachiwa ... kama ilisubiriwa muheshimiwa asepe ndiyo huyu atoke, ambayo hii itamfanya mwenye chama chake apate mahali pakushikilia na kujitetea kwamba alikuwa hajui mchezo mzima n.k, lakini vp kaka alikuwa anajua na hii wote ni janja yao moja?

Move hii inaoneka kuchezwa moja kwa moja kutoka magogoni ... mh! Je muheshimiwa kaamua kuchagua upande mapema kiasi hichi ... au na yeye anahesabu zake ...

Hata baada ya waziri wa mambao ya sheria kupelekwa nje ... watu wakaanza kusema kapelekwa kumshughulikia Lissu ... lakini ni kweli Lissu anakitisho cha namna hiyo ... nadhani timu inapangwa kwa ajili ya vuguvugu hasi ndani ya chama na siyo nje ya chama ... sababu kama alivyo sema muasisi wa chama Mwalimu, 'Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM', na ndicho tunacho kiona .. nadhani 'wanamkakati' na wana 'mtandao' ndani ya chama wanahofia upinzani mkubwa kutoka ndani ya chama kuliko nje ya chama kama wengi wanavyo fikiri. Kama ilivyokuwa 2015 safari hii mamba na kenge wanaweza kuwa wengi ndani ya CCM kuliko kawaida ...

Pamekuwa na tetesi kuwa yule mamba aliyetendwa na wanamtandao anaweza karudi ... lakini huo upande wake umekuwa kimya ... mbali na kila kile ambacho kinaokena kuletwa kwa ajili ya kuwafokonyoa na kuwachokoa waoneshe sura zao halisi watu wako kimya kama wanayo maji mdomoni ... wanachangaje karata zao haijulikani ni kimya, mchangishaji ni nani kama yupo kiza kizito kimya... mbona hawajibu shutuma na lawama zinazorushwa ... kimya ... wapo kweli au khofu yetu ... kimya .. eh! hii inatisha, ilimradi upande mmoja wa timu wachezaji wameanza kuonekana na hata kubashiri aina ya uchezaji utakao kuwepo ... huo upande mwingine sasa ... wapo au hawapo ni kimyaaaa! minong'ono tu.clock is tiking ... 2020 is like tomorrow, but its hotness its laready here and everybody feels it and every eyes is on Yellow and Green Flags! ...

Let's Pray to make to the other side safe and sound!
 
Back
Top Bottom