Kuelekea 2015 na sifa za makundi hasimu CCM

Kipokola

Senior Member
Joined
Apr 16, 2013
Posts
175
Reaction score
93

Makundi haya yamegawanyika sana ila makubwa ni makubwa ni mawili, linalojitambulisha kupitia Sitta,Membe na Mwakyembe(Wapambanaji wa ufisadi ndani ya CCM) na lile linalosemekana kuongozwa na Lowassa( Linajulikana kundi la Mafisadi)

Ukianzia kundi la kwanza ambaye kinara kwa sasa ni Waziri wa Mambo ya Nje Ndugu Membe limekuwa likitumia sana mitandao ya kijamii na vijana vya vyuo vikuu kujitangaza, kundi hili lipo hapa JF na facebook. Linakua kwa kasi.
Kundi la pili, hili ndo inasemekana lina nguvu zaidi CCM na linajulikana kama kundi la mafisadi, kila mtu ambaye anaonekana kupwaya ndani ya CCM au kunkizana ki mawazo na kundi la awali yaani la Wapambanaji ufisadi huwekwa kundi hili yaani ukionekana kutofautiana kimawazo na kundi la Sitta na Membe basi wewe ni fisadi kwa maoni yao na itafanyika njia yeyote kukuchafua hasa kwa mitandao ya kijamii, kundi hili limeathirika sana kwa siasa za maji taka la kundi la kwanza( wapambanaji wa ufisadi) kila baya la CCM likirusha kwake na mazuri yote ni kwa kundi la wapambanaji.

Haya ndo makundi makubwa hasimu ndani ya CCM, thou yapo mengine ila bado hayajafahamika na yatatokea mengi kadiri tukaribiapo 2015. Sifa za makundi haya:

Kundi la kwanza, Linaloongoza na Membe kwa sas, hili linatumia vijana kutoka CCM na wengine hata Upinzani na njia yao kuu ni mitandao ya kijana na vyuo vikuu na wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa, vijana hawa wakiongozwa Riz na Makonda hasa Makonda wamekuwa wakijipambanua kama wazalendo katika taifa hili. Kundi linaonekana kufanikiwa hasa katika mitandao limekuwa likipata vijana wengi na Nape amekuwa msaada mkubwa kwa kufanikisha mafanikio ya kundi hili.
Kundi hili la Wapambanaji limekuwa likipata support kubwa hata kutoka kwa viongozi wakuu wa chama, likitumika kufanya siasa maji taka dhidi ya wana CCM wengine, utakumbuka ni kundi hili ambalo ambaye anatofautiana nalo kimawazo basi atakuwa fisadi na itatafutwa ya namna yeyote ya kumchafua mfano: J. Makamba ambaye kutokana na kutokuwa na mahusiano mazuri au mtazamo mmoja na Membe basi alionekana yeye ni wa kundi la pili, tetea mafisadi

Vinara wa kundi hili licha ya kuwa na sifa za siasa za maji taka pia ni watu ambao hawaeleweki yaani utendaji wao ni wa mashaka, wako busy zaidi kukosoa mapungufu ya wapinzani wao kuliko kuonyesha uwezo wao.. Mfano: ni Ndugu Membe yeye akilala na kuamka kulalamika kuwa anahujumiwa na anaowaita mafisadi, huku tukisikia kauli tata kama nikuoteshwa uraisi kuna watu watatafuta kwa kukimbilia, huu ni udhaifu mkubwa yaani huwezi kuwa unautaka urais wa nchi na tayari ukawa na nia ya wazi kuwadhuru wa Tanzania wengine kwa tofauti za ki mtazamo, inatia mashaka juu ya hata uelewa wake na uwezo wake binafsi wa kuwazua na kujenga hoja na hata utendaji wake, ni wa kawaida mno ila kete yake kwa urais ni kupitia kwa ukaribu wake na Mwenyekit wa Chama na Uwaziri wa Mambo ya nje, huu ni udhaifu sidhani kama tunaitaji rais wa namna hii!

Ndugu Sita naye huyu ni mtu ambaye kwa vijana wengi wa leo anaonekana kuwa ni nguzo na mpambanaji wa ufisadi nchini na ndani ya chama ila kwa wale wanaofuatilia siasa kwa muda mrefu nchini wanatakubaliana na mimi kuwa naye ni mtua ambaye haeleweki hasa kwa matukio yaliyotokea akiwa spika, wale tuliokuwa tukifatilia bunge kuanzia miaka ya 2006 mnakumbuka yaliyotokea, kukumbushia ndugu Zitto Kabwe kijana mwenzetu alitoa taarifa bungeni juu ya ufisadi mkubwa wa Meremeta na kuomba bunge kuunda kamati ndogo kuchunguza suala husika lakin spika mara moja alimwita Zitto ni mzushi na mchonganisha bila kuona ya kwamba Zitto alikuwa hamtulumu mtu ila anaomba bunge kuunda kamati ndogo kuchunguza kashifa husika kujua kiini ila aliambua kufungiwa vikao kadhaa vya bunge kwa kupeleka uzushi ule bungeni. Hii inanishangaza mpaka leo huku Sitta akijiona ni msafi na kiongozi mwenye uweledi kweli nyani haoni kundule.
Lakini haikuishia hapo, Mkurugenzi wa TBC wakati ule ndugu Mhando aliandaa mjadala kuelezea kilichotokea bungeni hasa kuhusu Zitto kufungiwa vikao kadhaa vya Bunge na lile tukio la ndugu Malima na Mengi ambalo spika aliunda kamati ya bunge kulisuluhisha huo mgogoro na kamati ilitumia Milioni 100 na Malima alipatakana na hatia hata hivyo Sitta alisema kuwa Malima ni motto akikuwa ataacha… Tido alioji kuhusu double standard hii na kwenye panel ile alikuwepo pia Prof. Maina kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam, kitengo cha sheria, mtu makini kabsa na waliojitambulisha kama wanafunzi kutoka vyuo vikuu, Basi Prof.Maina alimuuliza spika kuhusu kilichotokea kwanin Zitto kufungiwa vikao kadhaa just kwa sababu ameleta kashifa ile ya Meremeta na huku akiwa anaomba bunge tu kuunda kamati kuchunguza ila alimwita mzushi na mchonganishi tena akiongea huku akitoa makaratasi mengine ikionekana wazi kajiandaa, akisema “eti hebu oneni haya ni makaratasi ameniletea Dr.Slaa (Taarifa za EPA) uzushi mtupu wa kwenye internet hakuna kitu hapa”
Ananishangaza sana, kwani yote aliyoyaita uzushi leo hii ni ya kweli na anachonishangaza zaidi ni kule kujiita mpambanaji wa ufisadi kwa kusimamia kashifa moja tu iliyomfanya Waziri mkuu wa wakati huo kujihudhulu tena wengine wakisema ilitokana nay eye Sitta kuwa na maslahi binafsi.. Ninakubaliana na Mwandishi mmoja wa Mwanahalisi aliyewai kuandika wapambanaji ufisadi ndani ya CCM ni Wanafiki na watafuta madaraka na huruma ya kisiasa(political sympathy) leo tunawaona wengi ni mawaziri, wakamtelekeza mwenzao Mpendazoe kwa maslahi yao.. hii tabia ya Sitta na wenzie inanitisha tukiwapa watu wa haiba yao nchi twafa.

Kundi la Pili, Ni la Mafisadi, likisemekana kuongozwa na Edward Lowassa anayetulumiwa na kashifa tata Richmond, nasema tata kwa kuwa kuna mengi yamefunikwa kuhusu hii kashifa na yakifumuka ni hisia zangu kuna watu watashindwa kuinua nyuso zao kwa aibu..
Kiutendaji Lowassa ni mzuri toka akiwa waziri wa ardhi, mazingira, mifugo na maji na baadaye waziri mkuu. Ni wazi alipokuwa waziri mkuu serikali ilionekana kufanya kazi la alipojudhuli mambo yalienda kombo bila shaka yeye ndo alikuwa rubani wa serikali ile toka 2006 mpaka alipojiuzuli kwani serikali ilifanya vizuri ukilinganisha na serikali ya tatu, ila toka kuachia ngazi imekuwa ikiyumba sana ikiwa haina collectivity, imejaa fitina na matukio ya hovyo.
Kundi hili, linaamini Lowassa alionewa na linaamini ndiye kiongozi ambaye anaweza kufanya maamuzi magumu, kundi tofauti na la awali halina wanafiki watu wake wako wazi wanakubali kukosolewa na inaonekana ndo limejaa vijana wasomi na smart kama kina J.Makamba, Bashe na Wengine, hawa wamejaa hekima tofauti na wakundi la awali.. kwa kifupi hawa wananivutia hafanyi siasa maji taka kuchafua wengine kama kundi la kwanza.
Hata kiongozi wa kundi hili yaani Lowassa ni mfano, wa kiongozi mvumilivu yaani pamoja na kashifa nyingi ambazo amekuwa akizotoa Membe na wengine dhidi yake na wakati mwingine personal attack amekuwa mtulivu sana, asiye jibishana na wa yeyote.. Kiukweli kwa hili ananivutia sana. Ila kosa ni moja kumpigania kikwete kuingia ikulu, ingawa hii hoja dhaifu mana hata wengine walimpigia kampeni na kura pia.. na hata hawa akina Sitta na Membe walimpigana tena bora huyu ambaye hivi hapatani na kiongozi husika kuliko huyo ambaye ndo rafiki wa familia maana bila shaka watakuwa wanafanana mengi kuliko EL, Membe akiwa karibu sana na JK ni mtu ambaye tulitegemea angeshauri kuhusu kuboresha serikali ili aweze kuthibitisha uwezo wake kuongoza lakin wap??? Nahisi hajui hata huko Ikulu anaenda kufanya nin, bora Lowassa anasisitiza maamuzi magumu, ni kweli nchi inaitaji maamuzi magumu ingawa naye inabidi atuelezee kwa upana kuhusu maamuzi hayo magumu! Kwani kauli yake ni wazi inawatisha baaadhi ya wana CCM hasa wenye Haiba za uvivu na uzembe.

My take; ni kwa vijana kufikiri kwanza kabla ya kutumiwa na wanasiasa kwa maslahi yao, kesho tutahukumiwa kwa tunayoyafanya leo na wenzetu au vizazi vijavyo yanayotokea sasa ni maandamano na vijana kujitoa muhanga kwa matukio ya kidini ni dalili za dhahiri ya kwamba watu wamechoka katika taifa hili kuona wengine wanakula wao wakibaki kutoa macho..tunakoelekea tutegemee mengi zaidi ya haya kutokana na kutokuwa na usawa kwa ugawanaji wa keki ya taifa na fursa nchini, kwani ni wazi hata ajira vijana wa leo kupata ni tabu, ni chache na hata hizo chache hupatikana kwa kujuana jambo ambalo si nzuri na lina hatari. Kwa hivyo tuache ushabiki na kufanya mageuzi yenye tija kwa taifa letu na si vinginevyo.
 
Umeandika vizuri sana kaka kutuonyesha hali ilivyo ndani ya CCM. Ushauri wangu ni kuwa ni vema mafisadi wakaitwa mafisadi hakuna jina jengine zaidi ya hilo. Naamini kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuhusiana na hao wanaoitwa mafisadi ndani ya CCM ndo maana wanaitwa hivyo na usitake waitwe majina mazuri wakati hawana sifa hizo.

Ni jukumu la kila mmoja kuona kuwa kama kuna watu ndani ya CCM wameamua kufungamana na mafisadi halafu wakafikiri ndo wako njia sahihi na kwamba waungwe mkono, sisi watanzania wa kawaida tunasema NOOO kwa mafisadi. CCM kama mmeshindwa kutuletea mwanachama asiye na kasha katika utendaji na uongozi wake kwa umma, basi mtambue kuwa mmepoteza sifa ya uongozi bora na hamhitajiki kushika dola ya tz.
 
WW kipokolo, mbwembwe zote, ni kumlmba lowassa miguu, shame upon, eti mchapa kazi, ukweli ni kwamba lowassa ni mchapa kazi wa kuiba mali za umma na kujenga matandao wa magenge ya kudhuru watu,
Koma kabisaa kusema mwizi lowasaa eti vijana wasomi wanamkubali, bila nachojua hawa ni makusuku wanaohongwa pombe na vocha za simu.
MIMI NASEMA KWA CCM HAKUNA MSAF,I ALIKUWA NYERERE NA SOKOINE TU WENGINEO WOTE VICHECHE TU MAJAMBAZI WATU MALI ZA UMMA KWA KUTUMIA MGONGO YA UMMA/WANANCHI
HATA MWANDIKE KWA KALAMU YA DHAHABU LOWASSA ATABAKI MWIZI TU WA MALI ZA UMMA.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom