Kuchokwa kwa chadema (chadema fatigue)

Kuchokwa kwa chadema (chadema fatigue)

RABIN GHYOOT

Member
Joined
Sep 17, 2014
Posts
10
Reaction score
2
Haya maandamano ambayo CHADEMA wanataka kufanya ni kipimo kizuri cha kuwaangalia uwezo wao wa kuhamasisha watanzania. Na pia kama watanzania wamewachoka.

Mpaka sasa hivi hatujaona uthibitisho kwamba watanzania wamehamasika kufanya maandamano au kugoma.

Hata humu Jamii Forum wanaoleta taarifa na picha ni wale wanaojulikana wanafanya kazi hiyo kwa malipo sio kwa moyo

Mpaka sasa hivi taarifa za maandamano zinaletwa na majina yale yale tu (Henri Kilewo) na hata picha za maandamano ni zile zile tu zinazoonyesha range ya lema ambayo kila mtu anaijuwa. Kwani hakuna watu wengine au sehemu nyingine?

Kama ukweli Mbowe alishindwa kuhamasisha watu wa Dar kumsindikiza wizara ya mambo ya ndani ikabidi alete watu na mabasi kutoka Moshi. Hii itakuwa kweli imemvunja moyo Mbowe. Huwezi ukawa kiongozi unayeweza kuhamasisha wachaga tu.

Mimi nilifikiri mambo ya kubeba watu kwenye mabasi wanafanya CCM tu kumbe mpaka CHADEMA. Ni dalili watanzania wamechoka na siasa.

Watu wakichoka na siasa hata uwaambie vipi wanaona ni wale wale matapeli, bora nichague shetani ninayemjuwa. I rather choose devil i know.

Kama hali hii ndio ukweli wenyewe basi kuingia ikulu ni Ndoto ambayo haitatimia.

Hata hapa watakaokuja kunitukana ni hao hao wanaolipwa sio wanaofanywa hivyo kwa moyo.

Hii ndio kuchokwa kwa siasa ambako pia kunaiathiri CHADEMA (CHADEMA FATIGUE).
 
.....


Huo ni mtaa moja tu hapo Musoma !!!



attachment.php
 
Hii ndio sababu ya kuchokwa CHADEMA:

Uzuri wa Mbowe ndio huo huo ubaya wa Mbowe na uzuri waShibuda ndio huo huo ubaya wa Shibuda. Tuliya nitakufafanulia.
Faida ya Mbowe kuwa mwenyekiti wa CHADEMA ni kwamba CHADEMAinakuwa na uhakika wa kuungwa mkono na wachaga, na hichi ni kitu muhimu. Ukwelikwamba mwenye mamlaka ya juu ndani ya CHADEMA, mwenye control ndani ya CHADEMAni Mbowe umewezesha chama hicho kuungwa mkono na wachaga kwa kiasi kikubwa. Kumbukachama hiki kimeshawahi kuongozwa na mwenyekiti (Makani) ambaye sio mchaga nakatika kipindi hicho kilikuwa hakina strong support ya wachaga.Wachaga wanaelewa hata ikitokea Rais wa Nchi ni Dr. Slaa naMwenyekiti wa CHADEMA ni Mbowe, katika mazingira hayo anayetawala Nchi niMbowe. Mwenyekiti wa chama chenye wabunge wengi anaweza kusababisha Raisakapigiwa kura ya kutokuwa na imani na yeye, na hivyo akapoteza Urais.Mwenyekiti wa Chama anaweza kuhakikisha awamu ya pili anapitisha jina lamgombea Urais mwingine, na hivyo Rais aliyekuwepo madarakani akaongoza kipindikimoja. Ukweli huu ndio uliyoifanya CCM ikatae kofia mbili; wakasema mgombeaRais atakayepitishwa na chama lazima pia awe mwenyekiti wa chama. Faida ya chama cha siasa kuungwa mkono na wachaga sio yakupuuzwa. Wachaga wanadesturi ya kujitolea kwa hali na mali. Chama kikiungwamkono na wachaga kina uhakika wa kupigiwa debe kwa sababu ni desturi ya mchagakutetea chenye faida kwake. Eneo lolote la utawala ambapo mwenye madaraka nimchaga basi hapo ujuwe CHADEMA wana-uhakika wa kupata msaada kisiri siri. Tembeleamikoani uangalie wafanya biashara wa kichaga wanavyojitolea kusaidia CHADEMA. Hukomikoani Mkuu wa kituo cha polisi akiwa mchaga basi CHADEMA wanauhakika wakupatamsaada kisiri siri. NCCR MAGEUZI miaka ya nyuma ilishawahi kupata hii strongchaga support wakati huo ikiongozwa na Mrema; katika uchaguzi wa mwaka 1995kilikuwa cha pili.Hata kama NCCR-MAGEUZI imepata mchaga mwingine (Mbatia) sasahivi, na TLP inaonekana kuongozwa na mchaga (Mrema) hii haitoshi kufanyawachaga waviunge mkono hivi vyama kwasababu zifuatazo: Kuna kipindi kirefu hawawatu walikuwa hawana jukwaa la kufanya siasa nikimaanisha walikuwa sio wabunge.Ubunge unakupa jukwaa, unachoongea kinapewa uzito. Kuna kipindi kirefu hawawatu walikuwa wanaonekana ‘CCM B', hata uteuzi wa Mbatia na dada yake ndani yabunge la katiba na la afrika mashariki uliimarisha imani kwamba Mbatia ni ‘CCMB' mpaka pale alipowageuka CCM na kuungana na UKAWA. Mrema kwa upande wake kunaswala la afya na kutokuwa ambitious.Nieleweke vizuri; sisemi kuungwa mkono na wachaga inatoshakufanya chama cha siasa kushinda uchaguzi na kuunda serikali; ninachosema hapani vigumu kuwa na chama cha upinzani chenye nguvu Tanzania bara bila ya kuungwamkono na wachaga.Ubaya wa Mbowe ni kwamba siku CHADEMA ikipata mwenyekitiambaye sio mchaga, huu ungwaji mkono wote kutoka kwa wachaga utafifia auutatoweka kabisa. Na mfano mzuri ni kumbuka NCCR-MAGEUZI pale Mremaalipoonekana hana Control ya chama, wachaga waliacha kuunga mkono hicho chama. Ubaya wa Mbowe ni kwamba huu ungwaji mkono mkubwa kutoka kwawachaga umefanya watanzania kutoka kabila zingine kushindwa kutofautishaCHADEMA na uchaga. Imekuwa vigumu kukutana na mchaga ambaye hashabikii CHADEMA.Na hii imefanya watanzania kutoka kabila zingine kujiuliza hivyi mapenzi yawachaga na CHADEMA yanahusiana na sera (policy) au utambulisho (identity);Kwamba utambulisho wako kama mchaga ni kushabikia CHADEMA. Tabia hii ya wachagaimeibua maswali mengi; Je wachaga ambao vipau mbele vyao ni kuwa matajirikifedha wanaamini watafaidika nini juu ya uwepo wa Mbowe kama mwenyekiti waCHADEMA? Haya ni maswali ambayo watanzania kutoka kabila zingine wanajiuliza.Uzuri wa Shibuda ni kutokuwa na bei, kuwa na ujasiri na uwezowa kusimamia mtazamo anaoamini ni sahihi hata pale unapotofautiana na viongoziwake. Ujasiri huu ndio uliomfanya vyama vya upinzani wampende alipokuwa yukoCCM, kwasababu alikuwa akiwakosoa CCM wenzie. Kutokuwa na bei ndiko kulikomfanya asielewane na Makamba.Ikumbukwe Makamba alikuwa timu ya pesa (yaani Lowasa na Rostamu). Ujasiri huundio ulikuwa unamfanya Shibuda amuunge mkono Spika wa bunge wakati huo mzee wastandard and speed, Samuel Sitta bila ya kujali alikuwa anapambana na nguvu yapesa (yaani Rostam na Lowasa). Lakini mwisho siku nguvu ya pesa iliwezakushinda kupitia Makamba, kwa kuhakikisha jina la Shibuda halipitishwi na CCMkugombea ubunge. Hii ilimfanya kuhamia CHADEMA. Chama chochote Shibuda atakachokwenda atakwenda na wasifu autabia yake ile ile ya kutokuwa na bei, ujasiri na uwezo wa kusimamia mtazamoanaoamini ni sahihi hata pale unapotofautiana na viongozi wake. Ubaya wa Shibuda ni kwamba hawezi kuacha tabia yake kwasababutu kahamia CHADEMA. Kama alivyokuwa CCM alikuwa na ujasiri wa kuthubutukutangaza kugombea dhidi ya Mwenyekiti (kikwete) wake ambaye pia ni Rais waNchi, kama aliweza kupingana na timu ya pesa (makamba, rostam, lowassa), kamahakuweza kuogopa kuondoka CCM chama tawala chenye fursa zote za kutengenezapesa, huwezi kutegemea ndani ya CHADEMA atakuwa mtu wa kusema "ndio bwanamkubwa". Hilo haliwezekani.Ubaya wa Shibuda ni ameingia CHADEMA akaendeleza wasifu wakeule ule wa kusimamia mtazamo anaoamini ni sahihi hata pale unapotofautiana naviongozi wake. Wakati CHADEMA imekataa matokeo ya Urais na kukataa kumtambuaKikwete kama Rais, yeye Shibuda alikubali matokeo ya Urais na kumtambua Kikwetekama Rais, ingawa CHADEMA baadae walikuja kuchukua msimamo huo huo wa Shibudana kukubali kumtambua Kikwete kama Rais. Wakati CHADEMA walipinga kulipwa posho yeye SHIBUDA aliungamkono ulipwaji wa posho akaita "ujira wa mwiha". Na mpaka sasa hivi hakunaushahidi kwamba CHADEMA hawapokei posho. Hivyo inawezekana CHADEMA wamechukuamsimamo wa SHIBUDA wa "ujira wa mwiha".Wakati kipau mbele cha CHADEMA katika kurekebisha KATIBA nikupatikana kwa serikali tatu, yeye Shibuda anaona kipau mbele iwe ni kulinda nakuboresha haki za wakulima na wafugaji ndani ya katiba. Inawezekana baadaeCHADEMA wakachukua mtazamo/msimamo wa Shibuda kama walivyofanya huko nyuma.CHADEMA inapomtumia Kasulumbayi na vyombo vya habari ilikupambana na Shibuda ni umakini wa hali ya juu. Tundu Lissu baada ya kumtishiaShibuda kwa kusema atamchukulia hatua kali kwa kuwepo kwenye bunge la katiba,kila akiulizwa swali na waandishi wa habari (waliotumwa na CCM) juu ya Shibudaanasema sitaki kumuongelea huyo mzee. CHADEMA wameona ni vizuri, umakini nasahihi kupambana na Shibuda kupitia msukuma mwingine kuliko mchaga au mtu wakabila nyingine. Hawataki wasukuma wawe na mtazamo hasi juu ya CHADEMA.Hawataki wakulima na wafugaji wawe na mtazamo hasi juu ya CHADEMA. Hapaunazungumzia kabila na kundi la watu lenye idadi kubwa ya watu kuliko kabila aukundi lingine lolote Tanzania.Wakati mbinu hii ya CHADEMA inawezekana ikawa sahihi, lakinilabda Kasulumbayi sio msukuma sahihi wa kumpambanisha na Shibuda. Nasema hivikwasababu ambayo nimeshaitaja hapo juu; historia na rekodi ya Kasulumbayi katikasiasa haionyeshi anao ujasiri na uwezo wa kusimamia mtazamo anaoamini ni sahihihata pale unapotofautiana na viongozi wa chama chake; historia na rekodi ya Kasulumbayihaionyeshi ni mtu asiye na bei kwasababu hajawahi kupingana na watu wenye pesanyingi (Makamba, Rostam, lowassa, Mbowe). Kwa lugha nyepesi Kasulumbayi badohajaji-thibitisha kwa wakulima na wafugaji na wala kwa wasukuma wenzake. Ukiongea na msukumawa kawaida huko Maswa mashariki anakwambia Kasulumbayi uhai wake kisiasa ukokwenye vyombo vya habari na waandishi walio nunuliwa na CHADEMA lakini siokwenye jimbo la Maswa mashariki. Wakulima, Wafugaji na Wasukuma wamemuamini Shibuda baada yakuona hana bei, anao ujasiri na uwezo wa kusimamia mtazamo anaoamini ni sahihihata pale unapotofautiana na viongozi wake. Sio tu Wakulima, wafugaji nawasukuma wanahitaji mtu wa aina hii kusimamia masilahi yao, kundi lolote katikajamii linahitaji mtu wa aina hii kusimamia masilahi yake. Kuna maneno yanatumika kama nyenzo ya kupambana na Shibuda.Maneno hayo ni msaliti, pandikizi, katumwa na CCM. Lakini ukiangalia kwaumakini unagundua hata uongozi wa CHADEMA hawaamini wanachokisema palewanaposema Shibuda katumwa na CCM. Huyu Shibuda kama alikuwa katumwa na CCM kuiangamiza CHADEMA alikuwana nafasi nzuri ya kufanya hivyo pale ugomvi wa Zitto na Mbowe ulipokuwaumepamba moto, pale Kitilia Mkumbo na Mwigamba wanafukuzwa CHADEMA, palewafuasi wa Zitto na Mbowe walipokuwa wanapambana nje ya mahakama huku wakiwawameshika mabango. Pale waislamu walikuwa wanaona Zitto anafukuzwa CHADEMAkwasababu ni Muislamu. Lakini Shibuda badala ya kuungana na Zitto katikakipindi hiki ambacho kilikuwa kinatoa nafasi nzuri ya kuiangamiza CHADEMA, yeyeShibuda aliamua kuwa mtazamaji. Na hata waandishi wa habari walipomuulizakwanini hamuungi mkono Zitto yeye akasema kila mtu atabeba mzigo wake. Viongoziwa CHADEMA wanajuwa Shibuda ni mwanasiasa mjanja na mzoefu ambaye anatambuawakati muafaka wa kufanya jambo; angekuwa na nia mbaya na CHADEMA angetumiakipindi hicho kuishambulia CHADEMA, lakini hakufanya hivyo kwasababu hana niambaya na CHADEMA.Usalama wa Taifa unaelewa ni hatari kwa afya ya CCM na Taifakama itatokea kabila lenye idadi kubwa ya watu, wasukuma (force of number) na kabilalenye ari, wachaga (aggressive force) watakuwa na mpango mmoja na vile vilekama itatokea hawaelewani. Lakini kwa vile imeshatokea wachaga kujitambua waokama CHADEMA unaitaji nguvu upande wa pili itakayo wamudu wachaga na nguvu hiyoni wasukuma. (Because Chagas [aggressive force] have already identifiedthemselves as CHADEMA, you need another force to counter that, and that forceis Wasukuma [force of number]). Hatari inayojaribu kuepukwa hapa ni ileiliyotekea Kenya, pale Odinga na Kibaki walipoungana, pale wajaluo na wakikuyuwalipoungana na kuitoa KANU (CCM) na Rais Moi.Ninachojaribu kusema hapo juu ni kwamba usalama wataifawalifanya kila linalowezekana Kuhakikisha Shibuda na CHADEMA hawawi na mahusianomazuri pale tu Shibuda alipoingia CHADEMA. Majungu, fitina na uchawi wa kilaaina ulitumika kuhakikisha Shibuda na CHADEMA hawawi na mahusiano mazuri.Lakini pia katika upande wa pili wa shilingi yeye Shibuda anaelewa mfumounavyofanya kazi kwasababu amekuwa katika mfumo huo mda mrefu. Shibuda alielewaakiingia tu CHADEMA usalama wa taifa utaanza kumlenga na asipokuwa makini hatausalama wake utakuwa hatarini.Ni kisema maisha ya Shibuda yalikuwa hatarini na anao ujasiriwa hali ya juu ili unielewe lazima ukumbuke Kolimba na Chacha Wangwe.Shibuda kwa kuelewa usalama wake unaweza kuwa hatariniilibidi alipoingia tu bungeni kwa tiketi ya CHADEMA atengeneza mazingira rafikina serikali ya CCM. Na hii ndio iliyopelekea yeye kuwa wa kwanza kukubali matokeoya uchaguzi na kumtambua Rais Kikwete kabla ya CHADEMA kukubali kufanya hivyo.Hii ni siasa ya hali ya juu, inaweza kufanywa tu na mtu anaelewa mfumo unafanyakazi vipi. Ndio maana unapoona mtu anamlinganisha Shibuda na Kasulumbayi unaonani utani uliokithiri.Shibuda anao upeo wa kujuwa kwamba CHADEMA yenye nguvu ndio inayofanyaCCM watake kumtumia Shibuda. A powerful CHADEMA is what makes Shibuda relevantto CCM. Kwa hali hii Shibuda atapendelea CHADEMA inayoisumbua CCM ili aendeleekuwa na umuhimu kwa CCM. Ndio maana si kushangaa alipoacha kumuunga mkono ZittoKabwe. Akasema kila mtu atabeba mzigo wake. Hakuna kitu kinachomfanya Shibuda asieleweke kwa mwanachamawa kawaida wa CHADEMA kama kuonekana katika majukwaa ya CCM wakati yeye niCHADEMA. Nakumbuka huko nyuma alionekana jukwaa moja na Kinana na Nape wakatiCCM ilipoenda kuhutubia wakulima na wafugaji karibu na jimbo lake. Naalipoulizwa kwa nini alikuwepo kwenye mkutano wa CCM, alisema wasukuma wanguwanamatatizo yaliyo kithiri na serikali iliyopo madarakani ni ya CCM, hawa ndiowako kwenye nafasi nzuri ya kutatua hali mbaya za wakulima na wafugaji. Alisemaukijuwa matatizo ya wasukuma yalivyo makubwa utajuwa jambo la msingi na kipaumbele ni kupata utatuzi wa matatizo yao na sio siasa za mimi naonekana wapi aunaonekana na nani. Siasa sio kipau mbele changu bali utatuzi wa matatizo.Majibu ya Shibuda hapo juu yalinikumbusha governor wa NewJersey, Chris Christie alipokuwa anajaribu kutatua matatizo ya watu wakewalipokumbwa na mafuriko katika kipindi cha uchaguzi Marekani. Kipindi hikiObama alikuwa anaandamwa na shutuma juu ya shambulizi la ubalozi wa Marekani,Benghazi, Libya. Kura za maoni zilikuwa zinaonyesha Obama yuko chini kidogo yaRomney. Lakini pamoja na hali hii governor kupitia chama cha Republican, ChrisChristie alikubali kuonekana na Obama na kumsifia Obama jinsi anavyosaidia watuwake wakati wa mafuriko. Hii iliwachukiza wanachama wenzie wa Republicankwasababu ilimnyanyua Obama kwenye kura ya maoni na kumfanya mgombea waRepublican, Romney awe chini. Alipoulizwa indirect question na waandishi wahabari kwanini anamsaidia Obama wakati sio mgombea wa chama chake alisema, "I've got a job to do here in New Jersey that's muchbigger than presidential politics, and I could care less about any of thatstuff."Ndio,kuna wakati siasa za vyama inabidi zisiwe kipau mbele; kipau mbele iwe niutatuzi wa matatizo ya watu kama Shibuda anavyosema, kama Chris Christieanavyosema.
 
Maelezo yooote hayo, ungeanza kwanza kujiuliza ni yupi aliyechokwa zaidi?

Hapa Tz tuna hili zigo la miaka zaidi ya hamsini, na kila uchao linatunga mikakati dhalimu ya kuendelea kung'ang'ania madarakani ikiwemo ya ufisadi wa ajabu na kadhalka!

Kama wewe hujalichoka hili zigo ila unaona CDM ndio kachokwa.....your head needs to be examined
 
Hebu watazame wananchi wa Musoma hapa...

attachment.php


attachment.php
 
Nasikitika kuona kuwa huna HOJA kuntu uliyokuja nayo zaidi ya hako KAKIINGEREZA FEKI ulikokuja nako hapa. Ya nini upoteze muda wa kuchafua UKURASA wakati unafahamu fika kuwa huna sababu ya msingi ya kufanya hivyo? Au ndo unakamilisha usemi wa "MPUMBAVU USEMA ILI MRADI AONEKANE KASEMA HATA KAMA HANA CHA KUSEMA"?
 
Back
Top Bottom