kubanja..

G_real

JF-Expert Member
Aug 23, 2019
684
851
Habari za saizi wakuu nikiongelea kubanja kila mtu anaelewa namaanisha nini. Kuna siku nilienda kwenye gradue ya form4 ya mdogo wangu mbeya pale soko matola kwenye ukumbi wa mkapa kipindi hicho nilikuwa na sumbuliwa saana na kifua ko nilikua na banja kinoma.

Hiyo siku nilikaa na watoto wazuri kinoma afu mi ndo nilikua katikati wakati wanaendelea na matangazo kulikuwa na utulivu saana mle ndani ghafla nikashikwa na banja haloo nilijibana mpaka mishipa ya kichwani ilinitoka uvumilivu ukanishinda nikapasua dooh ukumbi mzima waligeuka kuniangalia mimi sijawahi kupata aibu kama ile.
 
Banja huwa inachana hadi mashati, kuna mtu ulimchania shati hapo
 
Back
Top Bottom