Kuandika mungu, Mungu hakuondoi/badilishi maana ya neno!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Nimekuwa nikioona mara nyingi sana hapa JF watu wakiandika neno mungu au Mungu wakimaanisha kwamba ni vitu viwili tofauti, hapana Mungu na mungu ni kitu kile kile!

Wasichokifahamu wengi au labda niseme baadhi wanaofanya hili kosa ni kwamba jina lolote huanza kwa herufi kubwa na haijalishi maana ya hilo jina ni nini kama ni Shetani, Mungu, Malaika au sijui Jini maadamu ni majina (nomino) basi ni lazima yaanze na herufi kubwa lkn haimaanishi kama wengi wanavyofikiria kwamba kuna ukuu wowote ni sheria/kanuni tu ya lugha kwamba jina lolote lazima lianze na herufi kubwa hivyo kuandika mungu ukafikiri kwamba kuna tofauti na Mungu ni umburula wa hali ya juu !

Na wala usifikri kwamba kwa kuandika jina la mtu kwa herufi ndogo unamdharau huyo mtu hapana, ni kwamba unafanya kosa la lugha tu na hakuna uhusiano wowote ule na ukubwa au udogo wa mtu, au heshima au dharau kwa mtu husika ni kwamba umefanya kosa la lugha basi, lkn maana inabakia kuwa ni ile ile!

Hivyo kwa mfano ukisema siamini mungu na siamini Mungu ni jambo lile lile na hakuna tofauti yoyote isipokuwa tu umefanya kosa la lugha, hivyo kama ni dhambi kusema huamini Mungu pia ni dhambi kusema huamini mungu kama wewe unaamini kwenye dini zinazosema hivyo!
 
kkaangalie katika kitakatifu wameandikaje nndio utapata majibu sahihi huwa inatakiwa kkuandikwaje
 
Bila kuathiri mlengo wa hoja yako na usahihi wa lugha naomba ufahamu kuwa Mungu/mungu sio jina ni cheo/hadhi kama ilivyo mfalme,rais,meneja,mbunge,mjumbe n.k
Mungu/miungu ina majina yao.
Hata huyo anayeandikwa kwa kuanza na herufi kubwa pia ana jina lake.

Biblia inataja miungu kwa MAJINA yake.

MOLEKI, Ashtorethi, Baali, Dagoni, Merodaki, Zeu, Herme, na Artemi ni baadhi ya majina ya miungu ya kiume na ya kike yanayotajwa katika Biblia.

Tafadhali usiniulize yule tunayemwimba kwenye wimbo wa taifa ni Mungu/mungu yupi na jina lake ni nani?

Asante kwa mada jadilifu.
 
Back
Top Bottom