Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Nimesoma na kupitia CV nyingi sana za WatanZania wengi, na wengi wetu kuna jambo ambalo naweza kuliita kosa karibia wote tunalifanya nalo ni pale kwenye Lugha!
Wengi wa Watanzania kama siyo wote kwenye umahiri wa Lugha huandika English, Swahili wakati ilipaswa kuwa Swahili, English kwa maana kama ukiandika English, Swahili ina maana wewe unafahamu zaidi English klk Kiswahili yaani wewe Kiswahili umejifunza lkn Kiingereza ndiyo Lugha yako lkn kama ukianza na Kiswahili, English ambavyo ndiyo inavyopaswa kuwa kwa MtanZania wa kawaida ina maana lugha yako uliyokuwa nao ni Kiswahili halafu English umejifunza!
Ukiandika hivi yaani Kiswahili, English inakusadia sana kuondoa maswali hasa kama unaomba kazi kwenye makampuni ya kigeni hasa ya kizungu kwa maana Wazungu wote wanafahamu kwamba wewe haiwezekani English ikawa Lugha yako ya kwanza kama umezaliwa na kukulia TanZania, lkn kama ukiandika English, Kiswahili watakuuliza maswali utajichanganya na mwisho kupoteza imani na wewe!
Hivyo nawashauri WatanZania wote hasa wanaopenda kuomba kazi Makampuni ya kigeni zingatia hilo siku zote kuwa mkweli ili usipoteze nafasi ya kazi kwa jambo dogo kama hilo andika Kiswahili, English kwani Wazungu tayari wanajua kwamba wewe English umejifunza!
Na hasa sasa hivi kuna Makampuni mengi ya kigeni hasa kwenye eneo la Mafuta na Gesi wengi wanatafuta MtanZania ambaye hana shida na Kiswahili na pia mwenye uelewa na Kiingereza hivyo ukiandika English, Swahili kuna wageni wengi hata Waganda, Wakongo, Wakenya wataandika hivyo sasa tofauti iko wapi? lkn ukiandika Kiswahili, English Wazungu watakuchukuwa wewe kwanza!