nenda makao makuu ya jeshi watakupa jibu sahihi
Just for learning:
...Nikiwa form 6 tulikuwa tunafarijiana, "ukiwa na form 6 unafikia nyota jeshini na ukimaliza chuo kikuu ndo unazikomesha, hata nyota 4"
Japo mie ni nazi iliyoivia mnazini na sasa imechumwa na mama ntilie anaikodolea macho, bado napenda kutembelea majikoni kabla ya kuvunjwa na kukunwa!
Je, ni vigezo gani hutumiwa kuchagua kijana kusoma kozi ya staff cadet?
Kwa uelewa wangu, kijana amalizapo mafunzo ya JKT huingia mafunzo ya JWTZ. Huko hujifunza mbinu zaidi za kimapigano na kukabiliana na adui. Baada ya mafunzo hayo vijana wazalendo huingia ktk utumishi kama infantry, navy au anga. Sasa naomba kujifunza, je ni vigezo gani vijana hawa hupaa ktk kozi nyingine? Je, ni vigezo gani huzingatiwa kuchaguliwa kwa mafunzo ya Ukomandoo? Je, kuna wanawake ambao hupata kuwa makomandoo?
Tupanuane uelewa ili kuepuka kukariri kuwa vyeo jeshini vinagawiwa kama njungu au karanga kwenye vikao vyetu vya kahawa!
Just for learning!
Karibuni.
Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
tisa mbili hakuna komandoo mwanamke. we nenda RTS ukimaliza subiria kuitwa kwenye usaili wa cadet usipobahatika kuitwa kwenye usaili wa cadet ujue utabakia kua private soldier
Hakuna kozi ya staff cadet ktk jwtz.
Unapokosoa rekebisha sio unaacha ina hand.
Mleta mada kozi inaitwa Officer Cadet sio Staff Cadet inafanyika TMA.
Point of correction....siyo TMA (Tanzania Military Academy) bali hutolewa CSC (Command and Staff College) zamani wakiita kwa kiswahili CTU - Chuo cha Taifa cha Uongozi (wa kijeshi)
Though CSC na TMA zote zipo pamoja Monduli