Kova amkwepa Kibanda

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,767
Reaction score
288,342
KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Sulemain Kova, amekwepa kufafanua hatua iliyofikiwa na kamati aliyoiunda kuchunguza tukio la kuvamiwa na kuumizwa vibaya kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absolam Kibanda.

Kibanda ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Rai, Mtanzania, The African, Dimba na Bingwa, alipata masahibu hayo usiku wa Machi 6, mwaka huu.

Mhariri huyo alipigwa nondo kichwani, kutobolewa jicho la kushoto ambalo sasa limeng'olewa kabisa, kunyofolewa kucha na kukatwa kidole.

Licha ya jeshi la polisi kupitia kwa Kamanda Kova kuunda timu ya wataalamu 12 kuchunguza suala hilo, hadi sasa takriban wiki tatu hakuna mtuhumiwa aliyekamatwa kuhusika na tukio hilo.

Akizungumza na gazeti hili kwa simu jana jioni, Kova, ambaye alizungumza kwa kifupi, alisema kuwa hakuna mtu aliyekamatwa hadi sasa.

"Mimi sio sehemu ya timu ya upelelezi, litakapotokea jambo lolote tutawajulisha," alisema Kova ambaye hata hivyo Juni mwaka jana, aliunda timu kama hiyo kuchunguza sakata la kutekwa, kuteswa na kuumizwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Nchini, Dk. Stephen Ulimboka, na mpaka leo haikuwahi kutoa ripoti yake.

Hatua ya Kova na timu yake kupiga danadana katika uchunguzi wa matukio hayo mawili ya kutisha yanayofanana imeibua mjadala kwa wananchi na kudai jeshi hilo kwa namna moja linawakumbatia wahusika.

Jeshi hilo, ndani ya wiki moja limeweza kufanya uchunguzi wa video iliyoingizwa mtandaoni ikimuonyesha Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Lwakatare, akidaiwa kupanga mikakati ya uhalifu wa kuwadhuru baadhi ya watu.

Lwakatare na mtuhumiwa mwingine Josephat Lidovick tayari wamefunguliwa mashtaka ya ugaidi na uchochezi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mmoja wa maofisa wa polisi ambaye aliomba kuhifadhiwa jina, alilidokeza gazeti hili kuwa matukio hayo ya Dk. Ulimboka na Kibanda yanakuwa magumu kuyachunguza na kutoa majibu kutokana baadhi ya wajumbe wa kamati kutiliwa mashaka.

"Ulimboka aliwahi kumtaja mmoja wa maofisa wa polisi kuhusika na tukio la kuteswa kwake na hivyo kupinga kuteuliwa kupeleleza sakata lake, lakini mtu huyo huyo ameteuliwa tena kwenye tukio la Kibanda, hapo jiulize kuna siri gani. Kwa nini awe huyu kila tukio?" alihoji ofisa huyo.

Ofisa huyo aliongeza kuwa hata mtuhumiwa pekee anayeshtakiwa katika tukio la Dk. Ulimboka, Joshua Mulundi, jeshi la polisi halipaswi kujivuna kwani halikumkamata bali alisalimishwa na walinzi wa kanisa moja jijini Dar es Salaam, alipomtilia shaka kuwa amerukwa na akili.

[TD="bgcolor: #FFFFFF"]
Kova amkwepa Kibanda

na Mwandishi wetu
Tanzania Daima

[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
 
Custom white a.k.a Kova (kamjingiji) nikama daraja ndani ya mto nile lililojengwa na mabua ili CCM, IGP NA CHAGONJA wapitie kuelekea 2015 Kwa kuua, kutesa na kungoa vitu mbalix2 kwa watu makini....
 
Kuna ukweli ndani yake kwani Dr. Ulimboka alipoteswa wamekamata mtu mmoja tena asiyekuwa na akili timamu, tukio la Kibanda hajakamatwa hata mmoja ila kwa yule kamanda wa mwanza aliyewawa hapo awali wamekwisha kamatwa watu wa5 na kufikishwa mahakamani hapa nadhani kuna cha kujifunza na kuhoji kwanini utendaji wa police kuwa tofauti kwa watu tofauti? Je huyo mtesaji wa ulimboka hajataja mtu hata mmoja mpaka sasa? Kwanini huyo police aliyetajwa kuwa hafai kuwa miongoni mwa tume maana ni mhusika kwanini asingeondolewa na kukamatwa kwa mahojiano? Baada ya kujiuliza maswali yote haya napata jibu kuwa kuwawa kwa kamanda wa mwanza haikuhusisha police ila hili la kuteswa kwa kibanda na ulimboka halihitaji kufanya uchunguzi wa kugundua police ndo waliohusika ktk haya na serikali isidhani inawakomoa wao ama wananchi bali ni kujipalia makaa na kufungua njia kwa upinzani kujitwalia madaraka kirahisi pasipokutumia nguvu nyingi
 
Kuhusu suala ka Ulimboka na Kibanda, mtakuwa mnamwonea kamanda kova bure kwani alishaga jitoa kitambo.
 
Kuhusu suala ka Ulimboka na Kibanda, mtakuwa mnamwonea kamanda kova bure kwani alishaga jitoa kitambo.


Hapo ndo penye utata, wajibu wake ni nini? Mi nadhani maadili yake ni kusema ukweli badala ya kukwepa nakusema kajitoa! kumbe kila anaye paswa akisema kajitoa NI NANI ATAKAYE MFUNGA PAKA KENGERE?
 
Haiwezekani pamoja na vyombo vya usalama kibao eti waliomtesa jamaa hawajakamatwa .. kwangu J.K ni mtuhumiwa namba1
 
Haya mambo ni kama maigizo vile.
 
BAK, if you ask me about my fair comment regarding investigation in the police force i would humbly comment that "as a matter of fact competent investigators employed by the police force can comfortably sit in a bajaj"
 
Serikali ya CCM ndo iliyoratibu matukio yote mawili na kutekelezwa na TISS pamoja na jeshi la polisi nchini....Hivyo hawawezi kujichunguza na kuweka mambo hadharani, watajivua nguo.
Lile tukio la Mwanza hhawkulitekeleza wao ndo maana wote kuanzia IGP mpaka mkuu police post kule mwanza alihusika kutafuta wahusika na hatimaye wakapatikana , tena ndani ya wiki moja tu!
​SERIKALI INAHUSIKA KUWATESA ULIMBOKA NA KIBANDA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…