Mke akiwa safarini kwao aliandika ujumbe redioni, 'NAMRUSHA ROHO FULANI(JINA KA MUME WAKE). UJUMBE ASITEME BIGIJII KWA KARANGA ZA KUONJESHWA'.
Baada ya mume kuusikia majibizano yalianza kwa meseji.
Mume: Ujumbe wako unamaanisha nini?
Mke: Fikiria mwenyewe.
Mume: Nimeshafikiria,nimeshindwa.
Mke: Filkiria tu.
Mume: Mimi ni nani kwako?
Mke: Tusivuruge ndoa yetu bure kwa mambo ya kupita. Wewe mume wangu.
Mume: Ikiwa hivyo ndivyo nitake radhi kisha unijulishe maana yako. Ujumbe sikuupenda.
Mke: Hata mimi najua sina la kukufurahisha. Nisamee.
Haya toeni ushauri juu ya wawili hawa nani yuko sawa na nani kajichanganya.