UKAWA walikosesea kudai katiba mpya ya Warioba badala ya kudai katiba yenye vipengele muhimu tu kwao. UKAWA ingezingatia tu vipengele vya katiba mpya vinavyohusika na uchaguzi kama vile tume huru, madaraka ya rais, uhuru wa binadamu, kuhoji matokeo mahakamani, n.k, mbele ya safari ndo wangehangaika kubadilisha vifungu vingine ambavyo havijakaa vizuri. sasa wao waling'ang'ania "all or non" na matokeo yake ni lawama ambazo hazina msingi za kuibiwa kura. Nafahamu kuwa mjadala wa katiba utakapoanza watakosea tena maana wataendelea kung'ang'ana na katiba ya Warioba ambayo iko mbali sana kuja.