Kosa kubwa lilikuwa ni kumuoa huyu mwanamke

Majaribu2013

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
952
1,047
Hii siyo habari ya kutunga ni ukweli ninaoupitia katika maisha yangu.

Ilikuwa mwaka 2010 nilipotoka kwetu Nyegezi Mwanza kwenda Mbeya kikazi, ilikuwa ni kazi ya miezi miwili tulifikia katika hotel ya Mt. Livingstone. Wiki la pili tulitakiwa kuwa Kyela kwa ajili ya kazi kwa wiki nzima ambapo tulifikia Matema Beach hotel. Tulifanya kazi zetu kila siku asubuhi hadi mchana na tulipumzika hadi kesho yake.

Siku moja jioni tukiwa tumejipumzisha alitokea binti pale akawa amekaa akinywa vinywaji, ni binti mzuri sana ambaye ngozi yake ilikuwa kama chocolate mweupe kiasi, alikuwa amejazia vizuri sana na akionekana mwenye furaha na mzuri sana. Nilijisogeza karibu na kuanza kupiga naye story huku tukinywa vinywaji visivyo na kileo.

Tulitambulishana na hatimaye kubadilishana namba za simu. Tulichat mara kwa mara hasa mida niliyokuwa nimetulia. Binti alisema yeye amesoma mambo ya uhasibu lakini bahati mbaya hakuwa amepata kazi. Siku ya mwisho kufanya kazi pale Kyela alikuja tena jioni tulikunywa vinywaji na chakula cha usiku na kuagana. Niseme tu kweli kuna wanawake ni wazuri jamani siyo mchezo. Nilitamani sana ningepata muda wa kuwa naye lakini mazingira hayakuruhusu.

Niliporudi Mbeya mjini niliendelea na kazi zilizotuleta kwenye mkoa huu wa baridi, huku nikiendelea kuwasiliana na huyu mwanadada hatimaye nikamualika aje Mbeya siku moja. Nakumbuka siku hiyo ilikuwa Jumamosi ambapo aliamkia safari kuja na kufika saa nne asubuhi alikuwa amefika, nilipokea na tukawa pale hotelini. Tulishinda siku nzima pale tukipiga story na kubadilishana mawili matatu. Ilipofika mida ya jioni tulienda kupasha kwenye kauwanja flani wanacheza mpira wa mikono karibu na TRA.

Yeye alikaa tu na kuniangalia baadaye tukarudi wote na kuingia hotelini. Nilioga nayeye akaoga kisha tukala chakula na kulala. Usiku ule ulikuwa wa ajabu sana, msichana huyu alijua sana mapenzi jamani aliniacha asubuhi akarudi Kyela nikiwa mwepesi na mlaini sana kiasi hata kwenda kutubu dhambi kanisani nilishindwa.

Penzi likakolea na kunoga, hata niliporudi Mwanza alikuja kama mara tatu hivi hatimaye tulioana kwa ndoa kubwa ya mbwembwe sana. Siku hiyohiyo ya ndoa usiku tuliporudi ndani nilishituka sana kwani nilimuona kama hana amani akiwa amekaa kimya, nikamuuliza kuna tatizo akasema hakuna yupo kawaida. Hali hii iliendelea, akawa anakaa kimya kununa hata kwa wiki nzima bila sababu kabisa. Ukimuuliza hasemi chochote anajibu kwa kifupi tu hakuna tatizo.

Kwakweli ghafla nilikuwa nimeingia kwenye tundu la simba bila kujua kwani ilikuwa kununiwa mwanzo mwisho, hakuna amani na furaha kabisa ndani, maneno makali. Nilijitahidi sana kujitathimini wapi nimemkosea na kujikuta sioni popote huku yeye akisema hakuna kitu. Ulifika wakati nikamwambia naomba nikupeleke nyumbani ukapumzike utarudi ukiwa okey alikataa katakata.

Mpaka leo hii tuna watoto wawili ndoa yangu na mke wangu huyu ni mateso tu. Tumekaa vikao vya familia sana akiulizwa anasema simtunzi wakati nimefungulia supermarket ya ukweli tu pale jijini kati na nimemwambia be free hakikisha biashara yako haifi, tunza ndugu zako na wewe mwenyewe.

Vikao vyote mpaka kwa wachungaji havijmsaidia kitu. Namuona kama simba ndani, hakuna amani kabisa. anaweza kucheka sana na rafiki zake lakini wakitoka tu anabadilika rangi kama simba, sina tena hamu ya tendo la ndoa na yeye nimekuwa mtu msongo wa mawazo sana hamu ya ngono muda mwingi imepotea.

Siku ambazo nimekuwa ninahamu kali ya kufanya mapenzi nimekuwa nikiteseka sana, hali hii imeniletea tabia mbaya sana maana hali hii ikinitokea nikiwa safarini nimekuwa nikilala sana na watoto wa mapokezi kwenye mahotel ninayofikia. Mfano nikienda Dar hotel yoyote kubwa nikifikia nikimkuta binti mapokezi huyo imekula kwake, usiniulize huwa unawapataje hawa kila mtu na ujanja wake.

Sina hamu kabisa ya kufanya naye mapenzi kwa vile ni kama mmekaa maadui na hali hii imetokea baada ya tabia yake kuzidi kuwa tishio. Sitaki kuwa na mchepuko pamanenti wala demu pamanenti niko radhi nilale na mdada ninaye mpenda na nimlipe kisha baada ya hapo tuachane.

Sasa nimechoka haya maisha, nimeamua niache kazi na nitoroke niiache familia yangu. Watoto wote nimewafungulia akaunti na zina pesa za kutosha kusoma mpaka chuo kikuu kwa kila mmoja na maelekezo ya kuzitoa ni hivyohivyo mpaka watakapomaliza shule. Nataka nikimbilie Zanzibar nikajaribu kuanza maisha mapya huko bila wao kujua. Nitabadili kila kitu na nisipatikane kabisa kwa ndugu wote.

Wanawake wa wengine ni simba waliovaa ngozi ya kondooo hawafai kwa ndoa.
 
Pole sana hakuna hata raha ya ndoa sasa hao watto mmepataje au huwa unambaka pole kaka nina aunty zangu mm wapo huko kyela hizo tabia kuna baadhi wanazo huwa hawadumu na waume zao kabisa sbbu ya tabia zao lkn sidhani kama n wote wa kyela wapo hivyo.

Zamani haikuwa zaidi sana ila sasa imekuwa zaidi kiasi hamna hata hamu
 
Kukimbia familia sio jambo jema,
Japo nimesikiliza maelezo ya upande mmoja lakini sikuungi mkono kukimbia familia yako.
Watoto wanatamani kulelewa na wazazi wote wawili.
Nakuomba uvumilie uendelee kumwomba Mungu na usikubali kushindwa na mwanamke.
Ikiwa mke anakushinda, unaweza kuwa kiongozi ktk jamiii?
Tuliza akili endelea kumshawishi abadili tena kwa upole.
Vilevile pesa au mtaji sio suluhisho la mke kuwa na furaha, ni jumla ya maisha yenu ndiyo husababisha amani na furaha.
Wazo lako sio jema
 
mkuu pole wala usikimbie mji we muache endelea na maisha yako hapo unapofanya kazi tena ikiwezekana waambie na ndugu zako na mchungaji wako na weka msimamo unaachana naye wacha uonekane mbaya lakini amani ya moyo wako ni muhimu....kuanza moja si kosa mkuu ... endelea kutunza watoto wako .. ila kuna wanawake aisee sijui any way
 
mkuu pole wala usikimbie mji we muache endelea na maisha yako hapo unapofanya kazi tena ikiwezekana waambie na ndugu zako na mchungaji wako na weka msimamo unaachana naye wacha uonekane mbaya lakini amani ya moyo wako ni muhimu....kuanza moja si kosa mkuu ... endelea kutunza watoto wako .. ila kuna wanawake aisee sijui any way
Usihukumu kwa kusikiliza upande mmoja, nimegundua wale wanaokimbilia kushitaki na kulalamika ndio wakosaji zaidi.
Utajuaje kama anarudi usiku wa manane?
Utajuaje labda mchepukaji aliyekubuhu na mke akigundua au akatilia shaka atakuwa na amani?
 
Back
Top Bottom