Slas Nature
Member
- Oct 18, 2013
- 36
- 72
'
Habari za jumapili ndugu zangu.! Bwana Yesu asifiwe.!
watu wengi sana wanapoanza mahusiano kuna jambo moja kubwa sana ambalo linawatokea na wanaona ni kawaida bila kujua ni kosa kubwa mno na mwishowe huwa na majuto makuu. Jambo lenyewe ni hili;
"wengi wanapoanza mahusiano hupendana kwa mioyo yao yote, akili zao zote na nguvu zao zote" na kila mmoja hujitahidi kumuonyesha mwenzie kuwa amepata mtu sahihi. naamini ukilitazama jambo hili utasema ni sahihi na hakuna shida yeyote lakini leo nataka nikupe mambo yatakayokusaidia kujua kuwa jambo hili si sahihi kibiblia na ujue nini cha kufanya.
hebu tusome neno hili katika Kumb 6:5 "Nawe mpende Bwana Mungu wako, kwa nguvu zako zote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote"
Umeona hapo? Mungu hajasema umpende mtu kwa moyo wako wote, roho yako yote na nguvu zako zote, amesema umpende BWANA MUNGU WAKO. sasa inapotokea unaamua kubabilisha nafasi ya Mungu kwenye moyo yako na unamuweka mtu fulani basi ujue utapata vita kali mno kwenye hayo mahusiano maana maandiko yanatuambia "Bwana ni mungu mwenye wivu ..." (Nahumu 1:2) hivyo HATAKI nafasi yake ndani ya moyo wako umpe mtu.
Inawezekana ukasema lakini huyu mtu ndo ananiweka mjini au ndo ananiwezesha na kunisaidia kila kitu hivyo namtegemea yeye kwa kila kitu... oooh.!! usije ukafanya kosa hili maana maandiko yanasema hivi;
Yeremia 17:5 "Bwana asema hivi, amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake na moyoni mwake amemwacha Bwana"
Hivyo ni kosa kubwa sana kibiblia kumpa mtu moyo wako hata kama una hisia nae kiasi gani, lazima moyo wako ubaki kwa Mungu hata kama mwili unakusukuma kufanya hivyo. na ndio maana Paulo anatushauri katika kitabu cha 1Thesalonike 4:4 inasema "Kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima"
Hivyo jifunze kuuweza mwili wako ili moyo wako ubaki kwa Mungu maana ukitoa nafasi mtu aingie ndani ya moyo wako na wewe ukamwacha Mungu gharama yake ni kubwa sana na ndio maana wengi wakiumizwa na kuachwa hukimbilia na kurudi kwa Mungu na wengine wanakimbilia makanisani maana yake anataka kuurudisha ule upendo wa Mungu ndani yake ambao alimpa mtu badala ya Mungu.
Ni maombi yangu Mungu azidi kukufunulia upate kujua zaidi juu ya jambo hili.
Uwe na wakati mwema.