Korea Kaskazini yarusha Kombora na inadaiwa kuwa limetua katika Sayari

kichakaa man

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
5,500
5,163
Haya kiduku kafanya mambo yake tena .
Naomba msome

[Hébergement Internet, Cloud, et Serveurs dédiés - OVH]

HABARI

Silaha ya balistika ya Korea Kaskazini yadaiwa kufika kwenye sayari

Mei 14, 2017

[https://gdb]

Watu wanaangalia habari za Korea Kaskazini kurusha silaha ya balistika wakiwa katika kituo cha treni Korea Kusini.

Shirikisha

Korea Kaskazini imerusha kombora Jumapili katika anga za juu zaidi zisizo za kawaida katika njia inayopita silaha za balistika.

Hiyo ni dalili kuwa kunauwezekano kwamba Korea Kaskazini tayari iko katika uwezo mpya wa teknolojia ya balistika inayoendeshwa na nguvu ya nishati na mafuta yenye uwezo wa kupaisha kombora hilo mpaka kilometa 4,500.

Jaribio hilo kwa mujibu wa tamko la ikulu ya White House, “inalazimu kuwa ni ilani kwa mataifa yote kutekeleza vikwazo vikali zaidi dhidi ya Korea Kaskazini.”

Mapema, Japan na Korea Kusini mara moja zililaani kitendo cha Korea Kaskazini na kusema kuwa ni tishio kubwa kwa eneo hilo na ukiukaji wa azimio la Umoja wa Mataifa kuhusiana programu ya silaha ya Korea Kaskazini..

Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, aliagiza serikali yake “kuandaa hali zote za tahadhari,” kwa mujibu wa taarifa ya ofisi yake.

“Urushaji wa kombora hili la ballistika ni tishio kubwa kwa nchi zetu. Wizara ya Ulinzi na majeshi yetu ya ulinzi yanaendelea kufanya kazi kwa karibu na Marekani na Korea Kusini katika kukusanya na kuchambua taarifa mbalimbali,” Waziri wa Ulinzi wa Japan Tomomi Inada amewaambia waandishi mjini Tokyo.

“Tutafanya juhudi zote tunazoweza kuhakikisha kuwa amani na usalama unakuwepo nchini kwetu.”

Waziri huyo amesema inawezekana kuwa aina mpya ya silaha ya balistika ambayo imerushwa katika pembe ya sayari ya juu kabisa, ambayo imekwenda umbali wa kilometa 2,000 na kuruka kwa dakika 30, kabla ya kurejea katika pwani ya Japan baada ya safari yake ya kilometa 700.

Hata hivyo China imetaka pande zote kujizuilia ili kuepusha hatari inayoongezeka katika eneo hilo wakati Wizara ya Mambo ya nje ikitoa kauli ya kupinga kitendo cha Pyongyang kukaidi azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Beijing ni mshirika mkuu pekee wa Korea Kaskazini na ni nchi kuu inayofanya biashara na Pyongyang.

Rais wa Russia Vladimir Putin, ambaye hivi sasa yuko Beijing kwa ajili ya mkutano wa kimataifa, ameeleza wasiwasi wake kuhusu jaribio la kombora na kuongezeka kwa hatari, kwa mujibu wa msemaji wa Ikulu ya Kremlin.

Mahali lilipoangukiwa kombora hilo ni kilometa 400 kutoka pwani ya mashariki ya Korea Kaskazini kwa mujibu wa serikali ya Japan.

CHANZO NI VOICE OF AMERICA . VOA
 
adhibitiwe kukuza teknolojia yake?
Iwe teknolojia ya amani sio hizi za kisharishari. Sasa kuelekeza kombora sayari nyingine ambako hana uhakika ni akina nani wanaishi humo na uwezo wao ukoje anamaanisha nini zaidi ya kutaka kutuvuruga tu hapa. Jamaa wakiamu kujibu si itakuwa balaa. Kumbuka wao wanaitizama duni kama kitu kimoja na wakipiga hawatachagua pa kupiga.
 
akina nani
 
Hata mimi nimeshindwa kuelewa anazungumzia nini labda huko kwenye hiyo sayar kuna viumbe wanaishi na mamlaka zao hivyo wakiamua kujibu itakuwa balaa kwa mujibu wa dudus lakini sio mimi lkn hivi hiyo sayari iliyoguswa ni ipi na naomba nifahamishwe umbali kutoka usawa wa ardhi hadi kufika kwenye sayari iliyo karibu na dunia maili / km ngapi?
 
Km 2000 = 2000,000 metre
Dakika 30 = 1800 seconds

Sperd = distance
--------------
Time

= 2000000 m
----------------
1800. Sec

= 1,111.11 m/ sec

Yaaaaani bomu linasafiri kwa umbali wa mita elfu moja mia moja na kumi na moja nukta moja ndani ya sekunde moja,

Ni shaaaaaaaaa,
 
Shaaaaaaaàaaaßssss
 
Haya kiduku kafanya mambo yake tena .
Naomba msome

[Hébergement Internet, Cloud, et Serveurs dédiés - OVH]

HABARI

Silaha ya balistika ya Korea Kaskazini yadaiwa kufika kwenye sayari

Mei 14, 2017

[https://gdb]

Watu wanaangalia habari za Korea Kaskazini kurusha silaha ya balistika wakiwa katika kituo cha treni Korea Kusini.

Shirikisha

Korea Kaskazini imerusha kombora Jumapili katika anga za juu zaidi zisizo za kawaida katika njia inayopita silaha za balistika.

Hiyo ni dalili kuwa kunauwezekano kwamba Korea Kaskazini tayari iko katika uwezo mpya wa teknolojia ya balistika inayoendeshwa na nguvu ya nishati na mafuta yenye uwezo wa kupaisha kombora hilo mpaka kilometa 4,500.

Jaribio hilo kwa mujibu wa tamko la ikulu ya White House, “inalazimu kuwa ni ilani kwa mataifa yote kutekeleza vikwazo vikali zaidi dhidi ya Korea Kaskazini.”

Mapema, Japan na Korea Kusini mara moja zililaani kitendo cha Korea Kaskazini na kusema kuwa ni tishio kubwa kwa eneo hilo na ukiukaji wa azimio la Umoja wa Mataifa kuhusiana programu ya silaha ya Korea Kaskazini..

Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, aliagiza serikali yake “kuandaa hali zote za tahadhari,” kwa mujibu wa taarifa ya ofisi yake.

“Urushaji wa kombora hili la ballistika ni tishio kubwa kwa nchi zetu. Wizara ya Ulinzi na majeshi yetu ya ulinzi yanaendelea kufanya kazi kwa karibu na Marekani na Korea Kusini katika kukusanya na kuchambua taarifa mbalimbali,” Waziri wa Ulinzi wa Japan Tomomi Inada amewaambia waandishi mjini Tokyo.

“Tutafanya juhudi zote tunazoweza kuhakikisha kuwa amani na usalama unakuwepo nchini kwetu.”

Waziri huyo amesema inawezekana kuwa aina mpya ya silaha ya balistika ambayo imerushwa katika pembe ya sayari ya juu kabisa, ambayo imekwenda umbali wa kilometa 2,000 na kuruka kwa dakika 30, kabla ya kurejea katika pwani ya Japan baada ya safari yake ya kilometa 700.

Hata hivyo China imetaka pande zote kujizuilia ili kuepusha hatari inayoongezeka katika eneo hilo wakati Wizara ya Mambo ya nje ikitoa kauli ya kupinga kitendo cha Pyongyang kukaidi azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Beijing ni mshirika mkuu pekee wa Korea Kaskazini na ni nchi kuu inayofanya biashara na Pyongyang.

Rais wa Russia Vladimir Putin, ambaye hivi sasa yuko Beijing kwa ajili ya mkutano wa kimataifa, ameeleza wasiwasi wake kuhusu jaribio la kombora na kuongezeka kwa hatari, kwa mujibu wa msemaji wa Ikulu ya Kremlin.

Mahali lilipoangukiwa kombora hilo ni kilometa 400 kutoka pwani ya mashariki ya Korea Kaskazini kwa mujibu wa serikali ya Japan.

CHANZO NI VOICE OF AMERICA . VOA
Aliyeandika hii habari huko VoA amekurupuka. Sayari hazijawahi kuwa chini ya Kilomita Milioni 56 kutoka duniani.MERCURY ilifika distance hii miaka 2000 iliyopita.Mars pia ishawahi kufikia umbali huu na sometimes inafika mpaka kilomita milioni 570 kutoka duniani. Sijui anazungumzia Sayari gani.Ni kombora gani lifike kwenye sayari na litue baada ya dakika 30. Pengine mwandishi ana maana nyingine.

CURIOSITY ROVER ilirushwa toka duniani November 26, 2011 na Kufika sayari ya Mars August 6, 2012 kwa chombo kilichokwenda 20,000km/h kwa safari ya umbali wa kilomita milioni 570. Safari ya zaidi ya miezi 9.
 
Naona wamechoka kuwachokoza wamarekani sasa wameamua wahamie kwa alliens. Huyu mjinga asipodhitiwa ni maafa kwa dunia nzima.
47578d45f63780cc8b395b79a8a52300.jpg
 
Back
Top Bottom