Korea Kaskazini: Jaribio la bomu la nyuklia limefanikiwa kwa asilimia 100

mackie

Senior Member
Jan 26, 2017
141
197
dd8f67180d505c15926ab67e8d8c12ac.jpg

Korea Kaskazini imesema zoezi la kujaribu makombora yake lilifanikiwa kwa asilimia 100 siku ya Jumapili.

Kombora hilo ni aina mpya yenye uwezo wa kubeba vilipuzi vingi zaidi.

Vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vinasema jaribio hilo limeusisha kombora la masafa ya kati liitwalo Hwasong-Twelve.

Vinasema pia kuwa Rais wa nchi hiyo Kim Jong-Un alishuhudia moja kwa moja tukio hilo.

Marekani imetaka Korea Kaskazini kuwekewa vikwazo zaidi kwani inahatarisha usalama wa dunia.

Kombora hilo lililorushwa lilienda anagani urefu wa kilomita 2,000 na kusafiri kilomita 700 kabla ya kuanguka katika bahari Magharibi mwa Japan.

Korea Kaskazini ilisema siku ya Jumatatu ni jaribio la uwezo wa kombora jipya.

Jeshi la Korea Kusini limesema kuwa haliweza kuthibitisha madai hayo ya Korea Kaskazini.

Lakini limesema kuwa kombora hilo lilionekana kuweza kuruka angani, hatua ambayo ni muhimu katika utengenezaji wa makombora ya masafa marefu kulingana na kituo cha habari cha Yonhap.

Majaribio ya mara kwa mara ya makobora ya masafa marefu yanayofanywa na taifa hilo yanakiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa na yamesababisha wasiwasi miongoni mwa jamii ya kimataifa pamoja na Marekani.

Marekani na Japan zimetaka kufanyika kwa mkutano wa dharura katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne.

Shirika la habari la Korea Kaskazini KCNA limesema Jumatatu kwamba jaribio la kombora jipya la masafa marefu la Hwasong 12 lilifanyika kama ilivyopangwa.

Limesema kuwa jaribio hilo lililenga kuonyesha kwamba kombora hilo jipya lina uwezo wa kubeba kichwa cha Nyuklia.

04181d4d4b4e60ac5960127a4fafebe1.jpg

There are no excuses that justify N. Korea's actions. This was close to home for Russia. China cant expect dialogue. This threat is real.
— Nikki Haley (@nikkihaley) 14 May 2017
Kim said the North would stage more nuclear and missile tests in order to perfect nuclear bombs needed to deal with US "nuclear blackmail
28c95b4bfc7afa8925aeb632fc0e41e7.jpg
 
Wakianza vita huenda Africa ikawa sehemu ya kupata wanajeshi wakuweza kusaidia huko.
Nchi za africa wanategemea misaada sana kwahiyo hii itakuwa ndiyo gear ya hawa jamaa kutulaghai.
Tena huyu wa kwetu atahidiwa ndege 5 boeing za abiria na marupurupu mengine. Kumteka maskini wala haitaji akili kubwa na nguvu nying sana. Mlingishie vitu vizuri vizuri atakuja mwenyew
 
Wakianza vita huenda Africa ikawa sehemu ya kupata wanajeshi wakuweza kusaidia huko.
Nchi za africa wanategemea misaada sana kwahiyo hii itakuwa ndiyo gear ya hawa jamaa kutulaghai.
Hahaha 2tawekwa frontline kwasababu akili zetu zinakaribiana na m*ny*n*.
 
Back
Top Bottom