MR.NOMA
JF-Expert Member
- Feb 1, 2014
- 338
- 502
Wananzengo Habari za Jumapili! Natoa wito kwa Serikali hasa mamlaka husika kwa kuangalia viwango vya vinywaji na vyakula kutoa tamko haraka na kupiga marufuku kabisa biashara ya Konyagi ya kupima/ k va t ya kupima, maana hi kitu tayari watu wameanza kunyweshwa gongo na uchafu mwingine bila kujijua.Nimeshakutana na watu kadhaa wakilalamika juu ya Hilo lkn hamna mtu anayechukua hatua.Kuna jamaa alinisimulia alipimiwa toti ya Konyagi kwenye baa moja eneo la Mbezi Mwisho Baada ya kuinywa alisikia harufu ya mafuta ya taa mdomoni na baada ya dkk chache Tumbo lilianza kukatakata ilibidi awahi maziwa.Tafafhali Serikali wahusika mtusaidia kupiga marufuku biashara hii ya toti ya Konyagi/ k vant ili tuokoe nguvukazi ya taifa letu na Kama itawezekana makampuni ya vinywaji hivi yajiongeze yaje na vichupa vidogo zaidi vya ujazo mdogo Kama kiroba ili wasipoteze wateja.Point yangu ni afya za watu zipo hatarini,maana kuna wauzaji wenye tamaa,wanajaza vinywaji haram kwenye chupa za Konyagi/ K vant.Nawasilisha.