Kongole Serengeti Boys

mabuba

Senior Member
Dec 5, 2006
133
90
KONGOLE SERENGETI BOYS

Pongezi ziwafikie, japo mpo ugenini,

Faraja mwatupatia, hata ile ya sirini

Hakina mwaleta faraja mchezoni,

Kongole zenu vijana , vifua mbele twatembea

Uwezo muonesha soka kulisakata,

Kama Chenga kwa Angola mmezikata,

Sasa zamu yao Niger ulimi kuwakata

Kongole zenu vijana , vifua mbele twatembea

Mmeuleta umoja, pasi na mashaka,

CCM washanglia, Chadema wamemakinika,

KAFU wanasherekea, TLP Wanaruka

Kongole zenu vijana , vifua mbele twatembea

Dua zote sasa kwenu, Sala na maombi pia,

Mapambio yawasindikiza, Kaswida kuwafagilia,

Umoja mmeuleta, sote twashangila

Kongole zenu vijana , vifua mbele twatembea

Shime vijana wetu, sifa mtuletee

Kikombe mkibebe, Watz mtufikishie,

Tanzania ikatangazwe, Dunia ikasikie

Kongole zenu vijana , vifua mbele twatembea

Shime ukatie shime, uchawi sio jina lako,

Umakini ukazingatie, Pauseni awe kwako,

Shukrani ziwe njema, dua zako iwe yako

Kongole zenu vijana , vifua mbele twatembea

Nakutaja wewe Kabwili, Kipaki umeonesha,

Juma pia nakutaja, Chenga umeharalisha,

Nawe Makame ulipo, Goli umelengesha,

Kongole zenu vijana , vifua mbele twatembea

Kibabage, Nkosi, Msengi nawe Naftal,

Mkomola, Job, Ng`anzi, Suleiman pia Shomari,

Mhilu, Bakari, Mtesigwa, bao kawapigeni,

Rashid, Ada na Mwenda, Mchezo waonesheni,

Brazio, Ali, Kayego, msitoke mtanangeni,

Kongole zenu vijana , vifua mbele twatembea

Hima hima vijana, mbele msiache songa

Mbele mkalete kombe, wote tupate kupanga,

Taifa linawasubiri, msije mkabananga,

Kongole zenu vijana , vifua mbele twatembea.

Kisena Mabuba

Mwanamtaa
 
Hujazingatia vina pamoja na mambo muhimu ya mashairi... Ujumbe mzuri lkn. Umeuharibu ...kuanzia ubeti wa pili mpk mwisho... Pongezi Kwa kujaribu. Ingekuwa mashairi huwa rahisi hivo, basi kila mtu angeutunga
 
Unaumwa ugonjwa unaoitwa ukosoajikojo
 
Hujazingatia vina pamoja na mambo muhimu ya mashairi... Ujumbe mzuri lkn. Umeuharibu ...kuanzia ubeti wa pili mpk mwisho... Pongezi Kwa kujaribu. Ingekuwa mashairi huwa rahisi hivo, basi kila mtu angeutunga
Mimi sio mwana mapokeo
 
Tusubiri game ya kesho ndipo tuanze tambo

kale katim ka-niger nuksi sana tena hatareee

kama sio kubebwa Mali walishachapwa...goli likakataliwa, penati ikakataliwa nk

vijana wetu wajitume kwelikweli na Mungu awe upande wetu

Amin
 
Back
Top Bottom