Emc2
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 16,808
- 16,874
comrade igwe said
Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Mzee Philip Mangula amesema viongozi waliopita na kusoma katika chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere zamani kilijulikana kama Chuo cha uongozi Kivukoni walikuwa na maadili kweli kweli na walikuwa wanaishi maisha ya wananchi wanaowatumikia kwa maana walijua shida za wananchi haswa, Mh Mangula ameongea hayo leo tarehe 13.4.2017 katika kongamano la kumbukizi ya Mwalimu Nyerere iliyofanyika Katika chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere nje kidogo ya jiji la Daresalaam eneo la Kigamboni.
Mh Mangula alisema viongozi walisoma chuo cha Kigamboni walifunzwa na kujua maadili mema ya uongozi, miiko ya uongozi na imani katika chama na nchi, alisema wakati wa uongozi wa Mwalimu Nyerere yeye akiwa katika kamati ya maadili na usalama ya Chama, kulikuwa na jicho kali sana sana kuhusu tabia za wale wanategemea kugombea nafasi katika chama au nchi, hivyo wajumbe wa kamati ya maadili iliwachunguza sana wale walioomba nafasi mbalimbali za uongozi na wakibainika na kashfa zozote zinazohusu udini, ukabila na rushwa walichujwa na kuondolewa katika kinyang'anyiro cha uongozi.
"Wagombea wenye kulalamikiwa kuhusu udini, rushwa na ukabila hivyo waliundiwa kamati ya kuwachunguza viongozi ho wenye kulalamikiwa kuhusu maadili na wenye udini na kuwaondoa katika nafasi zao," alisema Mh Mangula, alitoa mfano kwamba kulikuwa na majimbo matatu kutoka Tanzania bara ambapo waliomba nafasi za uongozi wote walikataliwa "tuliwakatalia katika nafasi za uongozi baada ya kubainika kuhonga ili kupewa nafasi".
TBC LIVE
Francis12 said,
Leo kuna kongamano linafanyika. Mmoja wapo waalikwa ni Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Warioba. Muda huu anaongea hayo baadhi mambo ameongelea...
'Katika majadiliano Mwl Nyerere alikuwa haingilii mpaka watu wamalize'- Jaji Warioba.
Kiongozi bora awe na uwezo wa kugundua kama amekosea asahihishe, Mwl Nyerere alikuwa na uwezo wa kugundua na kujisahihisha'-Jaji Warioba
Kiongozi bora lazima uwe na msimamo na Mwl Nyerere alikuwa na msimamo ndio maana walikuwa wanasema aambiliki'-Jaji Warioba