Kongamano la CHADEMA Vyuo Vikuu Dodoma

pipoozzzzzz power mwendo mdundo wao waache wachonge na zero brain zao sie tupige job ya kuelimisha na kuwaamsha watanzania waliko lala.
 
Kazi nzuri sana hiyo, lakini isiishie kwa wasomi tu bali iende mpaka vijijini ambako CCM ndo wanapata mtaji mkubwa sana. Tuanze sasa kubadilisha fikira za wananchi wa Tabora ambako CCM bado inapata ushindi mkubwa sana. Nitakuwa msitari wa mbele kwa kazi hii.
 
mh mbunge dada REGGIA ahsante saana kwa taarifa hii njema juu ya mdahalo huo. lazima kuwe na base ya chama km ccm wanategemea akina mama vijijini sisi tu deal na vijana wote kwa ujumla sababu tumeona ktk vuguvugu la mapinduzi linaoendelea kwenye nchi za kiarabu ni vijana ndio wenye kuanzisha ukombozi na kuhamasisha rika nyingine ktk kujikomboa.vijana hawa wasomi wakirudi makwao itakuwa rahisi kuhamasisha vijana wengine kutafuta demokrasia halali. kingine mikutano km hii inajenga sana cha ki itikadi kuliko kusubiri karibu na uchaguzi. tuendelee kudai katiba mpya ndio msingi wa uchaguzi huru na wa haki 2015, tupo pamoja!!
 
thanks kutu update, tupo pamoja na ninyi pamoja sana dada.
 
Tunashukuru kwa updates. Tumeshindwa kufika kwa wakati cause usafiri unasumbua Education.
 
Una amanisha nini kusema Live! Inarusha na kituo cha TV? Au Radio?
 
Wekeni na mada hii Mkutano mwingine mkiandaa: Umhimu wa Wasomi wa Vyuo Vikuu kupata mbinu za kitaalamu katika Kuzomea!
 

ongeza Mh Regia! Tupo pamoja.
 
CDM tv inaanza lini au hata redio basi, hebu changamkeni, saa ya ukombozi wa umma kwa teknohama:redfaces:
 
Mtaji wa CDM msiuachie huo...wekezeni kwa vijana wasomi...young,energetic and innovative...matunda yake sio mbali ni hapo 2015
 
Well well intellectual mind is heart of ukombozi, simamieni kwenye hili most of us educated tunatoka interior(vijijini) kwa hiyo hizi harakati soon zitafika kwetu huku vijijini tulikozaliwa tukienda likizo after semista agenda ni ukombozi tena na mtindo wao wakutunyima field kizembe tutakuwa na muda wakutosha wakutoa elimu. Na jambo kubwa ni kuelimisha wenzetu wasiopata fursa hizi sisi kama wasomi ndio tunaweza kubadili muelekeo wa taifa hili not otherwise .binafsi nimechoshwa na ccm simply imeprove failure kwenye issue nyingi
 
Yupo anamsaidia Mkiti wake mtarajiwa ku handle crisis ya CC kujiuzulu. Wanashirikiana na rafiki yake R1
 
Asante kwa Taarifa. Lakini umenishangaza kitu kimoja, kutaja strategy hadharani na huku ukijua fika kuna upinzani. Ilikuwa inatosha kusema tunakutana na vijana wa DOM na si kueleza kirefu kuwa ni mkakati wa kujitanua kwa vijana. Strategy huwa haitajwi wazi hivyo, maana ni kuwaambia watu mnafanya nini ambao ni washindani baadae na wao wanaiba strategy hiyo wanaiboresha kisha mnashindwa kufanikiwa. Ni mangapi mlikuwa mnayaanzisha CCM wanayabeba na kuyatumia kufanikiwa na kuwaacha nyie mkilalalama ohh ilikuwa yetu ile!!!!
 
Mbowe ameshamaliza na ikafuata na mada kama ratiba inavyoonyesha.

Mada zimegawanyika katika sehemu tatu.
1. Wasomi Vyuo Vikuu Dodoma na Mustakabali wa Taifa ambayo na yenyewe imegawanyika katika sehemu tatu- 1. Siasa,Uzalendo na Maendeleo iliyotolewa na Godbless Lema 2. Dodoma.Kituo muhimu cha Ukombozi wa Tanzania inayotolewa na Christina Lissu hivi sasa. 3. Rasimali za taifa,fursa na Vikwazo itakayotolewa na Wenje.


2. CHADEMA na Mustakabali wa Taifa na yenyewe imegawanyika katika sehemu tatu-1. Uanachama,Falsafa na Itikadi itakayotolewa na Estther Matiko 2. BAVICHA,Nguvu ya Mabadiliko itakayotolewa na Regia Mtema 3. Kuelekea Uchaguzi wa Mitaa 2014 na Uchaguzi Mkuu 2015 itakayotolewa na Susan Kiwanga

3. Katiba Mpya na Mustakabali wa Taifa itakayotolewa na John Mnyika.


Sasa hivi Wenje ndio anatoa mada yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…