Kodi zetu zinaendesha maisha ya viongozi tu

Nathason2

JF-Expert Member
May 20, 2015
598
680
Itakumbukwa kuwa siku za karibuni serikali ilitangaza adhma yake ya kuhamishia makao makuu ya Nchi DODOMA hili sio suala jipya kwenye uongozi wa Tanzania awamu zote zilizotangulia zilijiwekea adhma hii kuhamishia makao makuu ya serikali Dodoma moja ya sababu ni gharama kubwa za uendeshaji wa serikali Hapa jijini Dar es salaam.kwa nini gharama ni kubwa?

Mosi Pango la nyumba wanazoishi viongozi Viongozi wetu walio wengi wanaishi luxurious sana,wanaishi maeneo ambayo pango za nyumba ni kubwa sana wengi wao wanaishi huko kandokando ya bahari ya hindi gharama za kupanga nyumba huko ni kubwa mno kiasi ambacho gharama za Pango la nyumba za viongozi huwa ni kubwa sana.masaki oysterbay na maeneo mengine kupanga nyumba sio chini ya milioni 20 kwa mwezihivo kiongozi mmoja analipiwa sio chini ya milioni 240 kwa mwaka

Pili:matumizi ya Mashangingi Viongozi wetu wamegoma kabisa kutumia magari ya kawaida wao wanatumia mashangingi hapa wengi wenu mnajua ni kiasi gani cha fedha kinateteketea kwenye mafuta,minor services na majo services unaweza kukuta kwa mwaka gari moja limekunywa zaidi ya milioni 200.

Tatu: Ulinzi wa Viongozi,ni kweli viongozi wetu wanapaswa kulindwa lakini sio kwa stahili wanayolindwa hivi sasa, viongozi wetu wengi wao wanalindwa na makampuni binafsi licha ya kuhatarisha maisha yao suala la ulinzi binafsi na ghari zaidi kuliko kutumia polisi wetu. Hapa tujiulize swali jepesi tu kwa nini polisi walinde Taasisi binafsi na washindwe kwenda kuwalinda viongozi wetu?kulinda nyumba ya kiongozi mmoja kampuni hulipwa sio chini ya milioni 5 kwa mwezi kwa mwaka ni million 60.

Nne:stahili za Viongozi,Licha ya unono wa mishahara ambayo mh Raisi alitamka wazi kuwa kunakipindi ilifikia million 40 nkwa mwezi Hapa kwenye stahili zao sasa kwa kweli simama mwenyewe bwana maana peke yetu hatuwezi,Viongozi wetu wanalipiwa maji,umeme,simu,wanawekewa sama za nyumbani,achilia mbali benefit kama za matibabu ya kiwangi kisichomithilika hapa kwenye stahili kila kiongozi lazima aondoke na milioni 5 kwa mwezi kwa stahili zingine na milioni 18.5 kwa ajili ya samani za nyumbani kwa mwaka.

Ukipiga hesabu za haraka Utagundua kuwa ili kumwezesha kiongozi mmoja kimaisha watanzania tunatakiwa kumchangia sio chini ya milioni 700 ili aendelee na maisha ya kawaida hapa usiweke ziara wala matibabu nje hii nikulala kuamka kwenda ofisini na kurejea nyumbani, richa ya Viongozi wetu kuwa Burden kubwa kwenye kodi zetu bado Viongozi wetu wamerudi kuwakomalia watumishi wa ngazi za chini pamoja na madiwani wetu kuwa ndio wanaoisababishia serikali hasara na gharama kubwa kwenye uendeshaji wake.

Endapo mh raisi atathubutu kulimulika eneo hili vizuri na akilibana ipasavyo yumkini tunaweza kujenga tuviwanda twingi twa toothpick na tukawapatia vijana wetu ajira nzuri tu.

Rai yangu:Watanzania tunawaomba viongozi wetu kuweni wazalendo kwa vitendo na sio kuhubiri uzalendo kuhimiza wananchi walipe kodi ili kufinance Matanuzi yenu na familia zenu,tunataka maendeleo na sio Maneno yenu ambayo hayaoneshi njia.Njooni basi tuishi huku kimara,mbezi,tabata n.k huko kwenye upepo mzuri waachieni akina mengi wanaoishi kwa gharama zao wenyewe.
 
Word
 
Me ndio maana nikisikia kiongozi kafariki kimoyo moyo huwa nashukuru laana zinapungua. Kiongozi aliyeniuma na ambaye hadi sasa ananiuma ni nyerere tu, maana ndie alikuwa mzalendo kweli na hakufuja wala kujilimbikizia mali kwa mgongo wa uongozi.

Ila hawa wasenge waliobakia wote ni wezi na matapeli tu wanatufelisha maisha hadi leo.
 
Halafu TBC walisema watakuwa live mkutano wa Lissu,hapa naangalia tbc Youtube naona hakuna kitu.Yaani hii nchi kazi kugharamia wasanii huku watoto hata madawati hawana,Stupid!!!!
 
Hivi ww una msimamo gani?
Maana huelewekagi ni mweusi au mweupe
 
Me ndio maana nikisikia kiongozi kafariki kimoyo moyo huwa nashukuru laana zinapungua. Kiongozi aliyeniuma na ambaye hadi sasa ananiuma ni nyerere tu, maana ndie alikuwa mzalendo kweli na hakufuja wala kujilimbikizia mali kwa mgongo wa uongozi.

Ila hawa wasenge waliobakia wote ni wezi na matapeli tu wanatufelisha maisha hadi leo.
We jamaa
 
Masuala haya huwa na utata kuyajadili maana huwa tunagawanyika,kuna watu wanatetea hayo mambo kwa sababu nao wanafikra za kula hayo mema. Unaweza kukuta mtu ni mpinzani ila anatetea kabisa hayo mambo.
 
Back
Top Bottom