Kodi za line ya sim za mikononi zingesaidia

kizimkazi

Member
Joined
Mar 10, 2009
Posts
59
Reaction score
7
Wanajmii,...

Kodi za line ya sim zingesaidia sana kulikomboa hili taifa kutoka kwenye muelekeo uliopo na kulipeleka katika muelekeo sahihi, kwakuwa ni mazoea yetu kuona kwamba hatuguswi moja kwa moja na kodi,inakuwa vigumu mtu kuona kodi yake inaliwa au inatumika sivyo

Tumeishi muda mrefu tukijiweka kwamba kodi hulipwa na wafanya biashara au wafanyakazi,hivyo kupelekea kwamba mtu wa kawaida asio kuwepo katika kundi hilo(mfanya biashara au mfanyakazi) kutoguswa moja kwa moja na matumizi mabaya ya kodi,na utakapo sema kodi zetu zinaliwa au zinatumika na wachache basi kundi hilo linajihisi haliguswi au halija poteza kitu.

Ila kama kodi ya sim ingeeendelea ingefika mahali kila mtu angekuwa na uchungu wa pesa anazolipa na ingekuwa rahisi kueleweka pale tunapolalamika kodi zetu zinaliwa na wajanja wachache.Tungekuwa sote ni wahanga wa kulipa kodi na tungekuwa tunataka kujua zinatumiakje?.

Sasa hivi kundi kubwa la watu hawaelewi inaposemwa "RAISI ANAZURURA KWA KODI ZETU" bado watu hawjui ni kodi gani hizo na yeye anakatwa wapi hiyo kodi?,hivyo inaishia kudharau au kuona maneno ya wanasiasa.

Ila tungekuwa soote tunakatwa kodi kupitia line ya sim basi hata muuza karanga angekuwa na uchungu na pesa ya kodi na ingemuwea rahisi mtu huyo kuamua kufanya mabadilko ya uongozi kama haufai.Na sidhani kama kufutwa kwake ni kuwahurumia wananchi bali kuogopa kwamaba hapa tutakuwa tumeliunganisha kundi kubwa la kuipinga serikali.

Kwa mfano hivi sasa swala la umeme ni wale tu wenye umeme majumbani ndio wanayahisi maumivu,ni vipi mpiga kura wa kijijini atayaona hayo maumivu ya umeme? jibu hayaoni na hatogundua tatizo la uongozi uliopo kwa sababu haguswi moja kwa moja.

Hivyo naamini kodi ya line za sim ingesaidia sana kufanya kila mwenye sim angepata maumivu ya kodi yake,na ingemuwea rahisi kuiuliza serikali kodi yangu inatumika ipasavyo? na kama haitumiki ipasavyo basi mtu huyo ingemuwea rahisi kuamua nani wa kumpa ridhaa ya kupanga na kutumia kodi yake ipasavyo kwa kutumia sanduku la kura.
 
Usinichekeshe, kwani kodi ya simu ingekuwa na maumivu tofauti na tunayoyapata kwenye kodi nyingine ambazo tayari tumekuwa tukizilipa? Hatutaki kusikia kodi zaidi kwa sababu hata tunazozilipa hatuoni manufaa yaakee, fullstop
 
Wakitaka songombingo ya nchi nzima watoze kodi ya simu.

Serikali huwa zinapinduliwa kwa jambo dogo sana.

Waingereza walitimuliwa USA kwa kichapo cha nguvu kisa ongezeko la Senti moja kwenye ushuru wa majani ya chai.
 
Nakubali sana kwamba zitakuwa na maumivu kidogo,na hazitashinda maumivu ambayo tunayapata kwa kodi zengine, Ila hizi za sim zigekuwa zinalipwa na karibu kila mwananchi,kwakuwa watumiaji wa sim ni watu wa aina zote. Kwa sasa kodi zinalipwa na matabaka mawili tu ya mijini, 1.wafanya biashara wakubwa ambao si wapiga kura. 2. wafanya kazi ambao hawatoshi kuwaondoa madarakani watawala wa sasa.
 
Wakitaka songombingo ya nchi nzima watoze kodi ya simu.

Serikali huwa zinapinduliwa kwa jambo dogo sana.

Waingereza walitimuliwa USA kwa kichapo cha nguvu kisa ongezeko la Senti moja kwenye ushuru wa majani ya chai.

Uko sahihi mkuu na hicho ndio nilichokiona, na ndio nikasema kuondoa kwao si kuwahurumia wananchi ila kuogopa kuunganisha nguvu za watu wa kuwapinga. Na ndio nikasema kodi ingeendelea kuwepo basi ingesaidia kuwaondoa hawa watawala wala kodi.
 
Back
Top Bottom