Hivi naomba kuuliza kwanini tumekuwa tukitozwa kodi mara mbili katika bidhaa moja na katika nchi moja??Mathalani unanua gari Zanzibar unalipia ushuru wote TRA zanzibar lakini ukija na basi pale malindi gari haitoki mpaka wakupigie hesabu nyingine tena wanakwambia system yao inaitwa (sycuda)Kama ni miss spell lakini nadhani nitakuwa nimeeleweka!!Unatoa tena pesa kuinusuru gari isipigwe mnada!!Je nikwanini serikali inafanya malipo mara mbili katiaka bidhaa moja na katika nchi moja??
Sababu ni kuwa na vyombo vya kodi/mapato viwili ambavyo si vya muungano. Zanzibar wana ZRB na bara wana TRA. Kila kimoja kinajiongoza na kinajitegemea. Ni sawa na kutoa na kuingiza bidhaa nchi tofauti.
nchi moja wapi wakati zanzibar imeshajitangazia kuwa ni nchi kamili yenye rais mwenye mamlaka yote , ina mipaka ya nchi inyotaka itambuliwe kimataifa. bora muungano uvunjike tubaki na TANGANYIKA NCHI YETU TUNAYOIPENDA