Kocha wa Ndanda FC

RRONDO

Platinum Member
Joined
Jan 3, 2010
Posts
60,381
Reaction score
139,178
Naangali SPORTS BAR YA CLOUDS FM,wanamuhoji kocha wa ndanda fc sasa hivi
ni kijana mdogo sana na ana uelewa wa hali ya juu kwenye mpira.

Sijawahi kumsikiliza mtaalam wa soka mwenye akili hapa tanzania kama huyu jamaa,kumbe sio bahati mbaya ndanda fc kupanda daraja. Ana exposure ya hali ya juu ambayo ni nadra sana kwa wachezaji wetu na wataalam wetu wa soka

Kocha huyu alikuwa anasoma degree ya Physics SOUTH AFRICA,akaacha na kuamua kusomea ukocha. Amesomea ukocha hapa tanzania na UK na ana vyeti vya FA. Kama TFF wakiwapa moyo vijana kama hawa watasaidia sana maendeleo ya soka nchini
 
huyu ni jamaa namfahamu vizuri sana. umri wetu unalingana..ni familia yetu ni rafiki zangu.
nilijua kwamba atafika hapa alipofika..
big up DENNIS KITAMBI.






 




 
ngoja akutane na hela Azam tutarud hapa kuongea vizuri yupo wapi yule mliemsifia hivi hivi wa mbeya city.

Wacha maneno yako kijana, Juma Mwambusi bado ni kocha bora kwa sasa na hilo halina ubishi.
 
Wacha maneno yako kijana, Juma Mwambusi bado ni kocha bora kwa sasa na hilo halina ubishi.

sikatai ila mpunga aliopata kutoka Azam umemuharibia hyo sifa amekua sawa na wengne tu wakawaida sana
 
sikatai ila mpunga aliopata kutoka Azam umemuharibia hyo sifa amekua sawa na wengne tu wakawaida sana

Alipeanwa mpunga mechi ipi na kwa madhumuni gani? Una ushahidi?
 
"MTWARA KUCHELE" hii ndo staili ya ushangiliaji ya wana Mtwara kwa sasa.
 
Sijui umri wako, lakini kama kocha mwenyewe ni mdogo kama inavyokisiwa (na kwa hivyo nakukisia kuwa umemzidi umri), kumpa shikamoo mdogo wako ni laana kwake.
On a more serious note, inafurahisha kupata wadau wa mpira walioibukia nje ya Tanzania na hatimaye kurejea nyumbani. Na wanapokutana na timu changa kama ilivyo Ndanda, kunapatikana kemia (chemistry) mwafaka baina yao. Anapaswa kupanda ngazi taratibu. Tatizo ni ikiwa -samahani kwa watakaoudhika- naye atakuwa ni kivuli cha Simba ama Yanga, kama ilivyo ........!
 

Physics noma, ni wachache wanaoijua vizuri. Waliosoma Physics hasa A-level wengi waliangukia pua kwa kupata D au E hivyo sioni ajabu jamaa kuachana na Physics ili awe kocha na leo anatupatia burudani uwanjani. Big up coach kwa kukimbia utalaam na kugeukia usanii.
 
Shkamoo ni zaidi ya heshim ya Mkubwa kutoka kwa mtoto, ni namna mpya ya kisasa ya kueleza kukubaliana haswa na kitu ambacho mwingine amefanya.

 

Attachments

  • Shikamoo TANESCO.jpg
    71.9 KB · Views: 336
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…