Kocha Mourinho aipa taji Man City

Kocha Mourinho aipa taji Man City

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amesisitiza Manchester City bado wananafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu pamoja na kikosi chake kukalia usukani kwa mara ya kwanza tangu Septemba.

Chelsea imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kunyakua ubingwa msimu huu, baada ya kuifunga City 1-0 kabla ya kuichakaza Newcastle 3-0.

Winga wa Chelsea, Eden Hazard alifunga mabao matatu kwenye mchezo huo wa Jumamosi.

Wakati Arsenal wakichakazwa 5-1 na Liverpool, City walipoteza pointi baada ya kulazimishwa suluhu na Norwich City, Chelsea kwa sasa wanaongoza ligi ikiwa imebakia michezo 13 kabla ya msimu kumalizika.

Hata hivyo, Mourinho ameendelea kusisitiza kuwa Chelsea haiwezi kutwaa ubingwa, kwa kuilinganisha timu yake kuwa ni sawa na ‘farasi mdogo’ katika mbio za ubingwa baada ya kuifunga City.

“Nataka kusitisha hadithi ya farasi, lakini sitoweza kubadilisha mawazo, Manchester City ni Jaguar. Huwezi kuiweka L-plate nyuma ya Jaguar. Tupo hapa tulipo kwa sababu tunajua nini tunachokitaka msimu huu na tuna lengo moja kubwa, kumaliza katika nne bora.”

Aliongeza kuwa: “Nasema nahisi hivyo. Siwezi kubadilisha hisia hizo. Tunacheza vizuri na imetuchukua muda mrefu kufikia hapa.

“Tumekuwa na wachezaji wenye viwango vya juu na wametusaidia kupata matokeo. Tupo kileleni ni kitu ambacho huwezi kuficha.

“Matokeo makubwa wakati wote yanakuja kama bahati, lakini yanatokea. Hakuna aliyetegemea matokeo makubwa Anfield. Man City yenye safu bora ya ushambuliaji usingetegemea kama wangetoka sare ni matokeo ya kushangaza.”
 
hizo ni mind games za Morinyo,ubingwa anautaka sana angekuwa hautaki ubingwa asingeshiriki kwenye ligi.
 
Back
Top Bottom