Kobe wa ajabu anayepindua gari

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
21,371
Reaction score
37,908
Kobe mkubwa anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka zaidi ya 120, (pichani), bado anaendelea kuishi kwenye shamba la kahawa la Kibo na Kikafu, Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.
Kobe huyo anadaiwa kuwa na nguvu kubwa kiasi cha kuweza kuangusha hata baadhi ya vitu likiwemo gari.
Inadaiwa kwamba kobe huyo amekuwepo katika shamba hilo tangu enzi za ukoloni kabla ya Tanzania haijapata uhuru.
Meneja wa shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 2,054, Jackson Matenge, alisema kobe huyo anajulikana kwa jina la Tony na kwamba hivi karibuni alionyesha uwezo wake baada ya kulipindua lori la tani saba na kusababisha ajali.
Alisema kobe huyo alikuwa amelala barabarani ambapo lori hilo liliegeshwa mahali alipokuwepo na aliponyanyuka, alilipindua lori hilo lakini hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa.
Naye Mwenyekiti wa Vyama vya Msingi vya Masama Saawe, Modio na Masama, Roo na Sonu Ngira, Hatibu Mwanga, alisema mwaka 1952 akiwa na umri wa
miaka minne, walikuwa wakicheza na kobe huyo akiwa mkubwa kama alivyo na kwamba hadi sasa ana miaka 58 lakini bado ana nguvu.
Alisema wakoloni waliokuwa wanamiliki shamba hilo kabla ya serikali kuyataifisha mwaka 1975, ndio waliomuweka shambani humo ambapo baada ya kuondoka walirudi na kutaka kumnunua kwa zaidi yaSh. milioni 100 lakini wanachama walikataa na kudai kuwa hiyo ni sawa na hirizi ya shamba hilo.
Alisema wazungu hao walirudi tena na kuomba kuuziwa kobe huyo lakini bado walikataliwa na kwamba idadi kubwa ya wazungu hufika katika shamba hilo kwa ajili ya kumuona kobe huyo na kupiga naye picha.
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya hiyo, Dk. Norman Sigalla aliutaka uongozi wa shamba hilo kumjengea mazingira mazuri ya kuishi kobe huyo ili aweze kutumika kama sehemu ya utalii kwa watalii wa ndani na nje.
CHANZO: NIPASHE

Duh hii kali wanaoishi karibu na hilo shamba tunaomba habari za huyu kobe



 

Attachments

  • Kobe.jpg
    18.9 KB · Views: 325
haya ni maajabu ya dunia Kobe mwenye uwezo wa kupindua loli ?
 
haya ni maajabu ya dunia Kobe mwenye uwezo wa kupindua loli ?

Tanzania watu wanaathiriwa sana kutamka matamshi kutokana na asili ya mtu atokapo.Kwa mfano watu watu wa kanda ya ziwa hasa mkoa wa Mara mahali pa l wenyewe wanaweka r.watu wa pwani mahali pa r waweka l,labda First lady anatoka maeneo ya pwani tumsaidie badala ya kumkejeli.




Hapa umesaidia nini?.
 
kobe mwenywe hata urefu wa futi mbili hafiki, je amepinduaje lori la tani saba?
 
loli.... naona anatoka mbeya ... ndagha fijo na LOLI...... hehe heiya..
 


Lori limepinduliwa na huyu????? mh!
 
Hilo la umri pengine ni kweli.


Inapokuja kupindua gari ya tani saba, pengine tunahitaji uthibitisho zaidi.
 
Wakuu, kupindua gari?? kama ni mboga ya kwenye bakuli imetiwa chumvi mfuko mzima atii,
 
Hilo la umri pengine ni kweli.


Inapokuja kupindua gari ya tani saba, pengine tunahitaji uthibitisho zaidi.

Heshima kwako SMU,

Kwanza nakushukuru kwa kujaribu kutulea data zaidi kuhusiana na umri anaoweza kuishi kobe.

Kuhusu kupindua lori tani saba nadhani pia inawezakana,kama ukisoma habari yenyewe kwa umakini utabaini gari lilipinduliwa kwasababu lilikuwa limeengeshwa sehemu kobe aliyokuwa amepumzika/kalala.Kobe anapokuwa amelala anaingiza kichwa na miguu ndani ya gamba lake anapoamka anatoa kichwa na miguu ili aweze kutembea kitendo cha kuanza kutembea lazima kitaongeza urefu na kama kuna kitu juu yake [Lori] lazima litanyanyuliwa.
Nikiri kwamba hata mimi nilipoiona hii story kwa mara ya kwanza akili yangu iligoma kukubaliana hili jambo linawezekana lakini baada ya kutafari sana nikagundua ni kitu kinachowezekana.
 

hivi kweli ana nguvu kiasi cha kupindua kilo elfu saba?
Je mifupa yake ni calcium au chuma cha pua?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…