Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Simba yamfungia Hassan Kessy kutocheza mechi 5 kwa kumchezea rafu Christopher Edward wa Toto na kutolewa kwa kadi nyekundu, Haji Manara athibitisha.
===================
Klabu ya soka ya Simba imemsimamisha mchezaji wao Hassan Kessy Ramadhan mechi tano kwa kosa la kumchezea madhambi mshambuliaji wa Toto Africans Edward Christopher. Katika Mchezo uliochezwa April 17 mwaka huu Uwanja wa Taifa Kessy alimchezea Christopher faulo, hivyo kupewa kadi nyekundu, na uongozi Simba umeamua kumfungia mechi hizo ili kupinga Vitendo vya Utovu wa nidhamu.
Kufungiwa mechi tano kwa Kessy maana yake ni kuwa amefungiwa hadi Mwisho wa msimu kwani Simba imebakisha mechi tano katika msimu huu. Hii inamaanisha kuwa Hassan Kessy Ramadhan si mchezaji tena wa Simba maana mechi tano alizosimamishwa ni sawa na mwezi mmoja ambao ni muda wa mkataba wake uliosalia.
Chanzo: Radio Free Africa