Klabu Bingwa Afrika: Yanga 1 - 1 Al Ahly, 9 Aprili 2016

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
MASHINDANO: Klabu Bingwa Afrika, Raundi ya 3, Mchezo wa Kwanza

TAREHE: 9 Aprili, Saa 10 Jioni

MAHALI: Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam


Kikosi cha Ahly Kilichokuja Dar ni:

Makipa: Sherif Ekramy, Ahmed Adel na Mosad Awad.

Mabeki: Ahmed Fathi, Bassem Ali, Mohamed Hani, Saad Samir, Rami Rabia, Ahmed Hagazy na Sabri Rahil.

Viungo: Hossam Ghaly, Hossam Ashour, Amr El-Sulaya, Ahmed El-Sheikh, Walid Soliman, Moemen Zakareya, Ramadan Sobhi na Abdalla El-Said.

Washambuliaji: Malick Evouna, Amr Gamal na Emad Meteb.

KIKOSI CHA YANGA:
1. Ally Mustapha
2. Juma Abdul
3. Mwinyi Haji
4. Kelvin Yondani
5. Vicent Bossou
6. Thabani Kamusoko
7. Deus Kaseke
8. Salum Telela
9. Amissi Tambwe
10. Donald Ngoma
11. Yousouf Boubacary

BENCHI:
Deo Munishi
Oscar Joshua
Pato Ngonyani
Geofrey Mwahiuya
Simon Msuva
Paul Nonga

Mechi ndiyo imeanza na kila timu inaonekana iko makini.

Dk 1, Ngoma anawatoka mabeki wa Ahly, lakini kabla hajapiga wanaokoa na kuwa kona, inapigwa na Boubacary, anaigonga Tambwe unatoka na kuwa goal Kick.

Dk 3, Al Ahly wanafanya shambulizi la kwanza lakini Yanga wanakuwa wepesi kung'amua mbinu zao

Dk 5, Juma Abdul anapiga mpira wa adhabu, shuti kali lakini linaishia mikononi mwa kipa

DK 10, Bossou anafanya madhambi karibu kabisa na lango la Yanga, faulo.

Dk 12 hadi 14, Yanga wanaonekana kuchangamka lakini safu ya ulinzi ya Ahly iko makini sana na wamejaza watu zaidi ya watano GOOOOOOOOOO Dk 11, Amri Gamal anaipatia Yanga bao kwa kichwa baada ya kupiga mpira wa kichwa kutokana na faulo iliyowachanganya mabeki wa Yanga waliodhani angepiga shuti...

Dk 16, Yanga wanagongeana vizuri, Kamusoko anampa pasi nzuri Abdul anapiga shuti kali lakini mpira unamgonga beki na kutoka nje, kona. Inachongwa na Boubacary lakini ni kona butuuu

GOOOOOOOOO Dk 18, krosi safi sana ya Boubacary, beki Hossam Ghaly ambaye ni nahodha wa Al Ahly anautumbukiza mpira wavuni yeye mwenyewe...

Dk 21, Gamal anapiga kichwa safi akiunganisha kona lakini mpira unatoka nje kidogo. KIpa Mustapha anaonekana kukasirishwa na walinzi

Dk 22, Yanga wanafanya shambulizi kubwa, krosi nyingine safi ya Boubacar lakini anaokoa, mpira unamkuta Ngoma anapiga shuti dhaifu, kipa Shariff Akram anadaka kwa ulainiii

Dk 23 hadi 26, mpira unachezwa katikati zaidi na ilivyo ni opening game, kwani mashambulizi ni kwa zamu

Dk 27, Said anamtoka Bossou na kupiga shuti la 'akili' lakini mpira unatoka kidogo nje ya lango la Yanga.

Yanga lazima wawe makini kwa kuwa kadiri muda unavyokwenda, inaonekana Ahly ndiyo wanauthibiti zaidi mchezo

Dk 28 hadi 30, Yanga wanaotea mara mbili kupitia Yondani aliyepanda na Ngoma. Hali inayoonyesha inabidi wajipange kuutegua mtego huo

Dk 32, Yanga wanafanya shambulizi jingine safi kabisa, lakini Telela anashindwa kumalizia mpira wa mwisho, goal kick

KADI Dk 33, Kipa Akram analambwa kadi ya njano kwa kupoteza muda. Hii ni kadi ya kwanza katika mechi hii

Dk 34, hadi sasa Yanga wamefanya madhambi mara 5 na Ahly mara 4

Dk 37, Ngoma anawahadaa mabeki wa Ahly na kupiga shuti lakini kipa Akram yuko makini anadaka vizuri kabisa

Dk 38 hadi 40, Ahly wanamiliki mpira muda wote lakini wanaonekana "kununua" muda kwani wanajua kubaki na mpira ndiyo ulinzi wao.

Dk 41 hadi 45, bado inaonekana Ahly kuwazidi ujanja Yanga, wanamiliki mpira katika eneo lao au kucheza taratibu
DAKIKA 1+ YA NYONGEZA

MAPUMZIKO


Dk 46, Zacharia anamchambua Mwinyi na kupiga shuti linalogonga mwamba, ilikuwa hatari kwelikweli

Dk 49, bado Ahly wanaonekana kuwa bora kwa kujiamini zaidi huku Yanga wakionekana bado na hofu baada ya kupoteza mpira kila mara baada ya pasi mbili, tatu.

Dk 52, bado inaonekana hakuna shambulizi kubwa ambalo wamefanya Yanga katika kipindi hiki ukilinganisha na Al Ahly

KADI Dk 54, Telela analambwa kadi ya njano kwa kumuanguha Abdallah Said. Bado Ahly wanaonekana kumiliki mpira zaidi.

Dk 56, Kaseke anampa Kamusoko pasi nzuri kabisa lakini anapiga mpira juuu. Hakuwa makini wakati anajiandaa kupiga mpira huo...

Dk 58, Boubacary alikuwa akijaribu kuwatoka mabeki wa Ahly anaangushwa na kuwa faulo nje ya 18.

Dk 59 anapiga mpira huo wa Kamusoko lakini anabutua juuuuuu...!!

Dk 61, Yanga wanaonekana kupoteza mipira mingi zaidi huku kiungo chao hasa cha ukabaji kinaonekana kutokuwa na uhakika

SUB Dk 62, Geofrey Mwashiuya anaingia kuchukua nafasi ya Boubacar

Dk 65 bado mpira umepooza, Ahly wanaonekana wamewa "win" Yanga, kwani hawajafanya shambulizi kali katika kipindi cha pili huku wao wakionekana kufanya wanachotaka

Dk 66, hatari kwenye lango la Yanga lakini mabeki wa Yanga wanaokoa
Ahly wanaokoa na kuwa kona. Inachongwa lakini haina madhara

Dk 66, Ngoma anamchambua nahodha na Ahly na kuingia vizuri kabisa lakini mabeki wa

SUB Dk 68 Ahly wanamtoa Subh anaingia Waridi Suleyman
Yanga nao wanamtoa Tambwe na kumuingiza Msuva

Dk 60 na 71, Yanga wanaonekana kuchangamka hasa katikati ya uwanja, wanagongeana vizuri lakini mipango ya mwisho katika umaliziaji inaonekana kutokuwa na nguvu

SUB Dk 73 upande wa Ahly Hossan Ahour anaingia nafasi ya Hossan Hgally ambaye ni nahodha.

Dk 73, Ahly wanafanya shambulizi jingine kali, lakini Bossou anaingia na kuosha mpira 'kindava'

Dk 74 hadi 76, Yanga wanaitumia kwa kugongeana, lakini kama ilivyo kawaida wanakwenda kumalizia kwa shuti dhaifu kabisa la Haji Mwinyi. Kipa Barthez yuko chini baada ya kuumia ubavuni, anatibiwa

SUB Dk 81, Deogratius Munish 'Dida' anaingia kuchukua nafasi ya Barthez ambaye baada ya kutibiwa amechukuliwa na kuingizwa kwenye gari la wagonjwa

Dk 82, Ngoma anageuka katikati ya mabeki watatu wa Ahly, lakini shuti lake linakwenda nje

Dk 84, kipa Dida anamzoa beki wake Yondani wakati akiokoa mpira, lakini beki huyo anainua

SUB 85 upande wa Ahly, wanafanya mabadiliko ya mwisho Zacharia anatoka na nafasi yake inachukuliwa na rais wa Gabon, Malick Evouma.

Dk 86, inaonekana Ahly wameridhika na walichokitaka, lakini wanalazimika kuwa makini kwa kuwa Ahly wanaweza "kuwaotea" na kuwamaliza.

Dk 87 hadi 89 timu zaidi zinagongeana pasi ambazo hazina manufaa kwani hakuna hata moja iliyopiga shuti lililolenga lango

DAKIKA 4+ ZA NYONGEZA

Katika dakika 2 za nyongeza, Yanga wanagongeana vizuri lakini umaliziaji unakuwa ni uleule.

Evouma anajirusha na kuanguka ndani ya eneo la hatari lakini wamuzi kutoka Ivory Coast anamuambia amka twende

MPIRA UMEKWISHAAAAAAA

81f3164a-5c5b-4c5d-b5b2-cf2897254a40.jpg
 
Kwakweli nina homa kali sana ya huu mchezo wetu dhidi ya hao waarabu,ngoja nilale kwanza....
Huenda nikiamka nitakuwa sawa.
Kila la kheri Yanga
 
KIKOSI CHA YANGA KINACHOANZA DHIDI YA AL AHLY LEO, HIKI HAPA…
1. Ally Mustapha
2. Juma Abdul
3. Mwinyi Haji
4. Kelvin Yondani
5. Vicent Bossou
6. Thabani Kamusoko
7. Deus Kaseke
8. Salum Telela
9. Amissi Tambwe
10. Donald Ngoma
11. Yousouf Boubacary
BENCHI:
Deo Munishi
Oscar Joshua
Pato Ngonyani
Geofrey Mwahiuya
Simon Msuva

Paul Nonga
 
KIKOSI CHA YANGA KINACHOANZA DHIDI YA AL AHLY LEO, HIKI HAPA…
1. Ally Mustapha
2. Juma Abdul
3. Mwinyi Haji
4. Kelvin Yondani
5. Vicent Bossou
6. Thabani Kamusoko
7. Deus Kaseke
8. Salum Telela
9. Amissi Tambwe
10. Donald Ngoma
11. Yousouf Boubacary
BENCHI:
Deo Munishi
Oscar Joshua
Pato Ngonyani
Geofrey Mwahiuya
Simon Msuva

Paul Nonga

ndala 0 - 5 Al Ahly..
 
KIKOSI CHA YANGA KINACHOANZA DHIDI YA AL AHLY LEO, HIKI HAPA…
1. Ally Mustapha
2. Juma Abdul
3. Mwinyi Haji
4. Kelvin Yondani
5. Vicent Bossou
6. Thabani Kamusoko
7. Deus Kaseke
8. Salum Telela
9. Amissi Tambwe
10. Donald Ngoma
11. Yousouf Boubacary
BENCHI:
Deo Munishi
Oscar Joshua
Pato Ngonyani
Geofrey Mwahiuya
Simon Msuva

Paul Nonga
Niyonzima mbona hayupo kwenye list?
 
MASHINDANO: Klabu Bingwa Afrika, Raundi ya 3, Mchezo wa Kwanza

TAREHE: 9 Aprili, Saa 10 Jioni

MAHALI: Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

============================
============================
Nawatakia watani wangu wa jadi ushindi mnono dhidi ya al ahly. Msiogope takwimu, piganeni, gangamaleni, atumwi mtu sokoni Leo na inshallaah mtashinda.
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Back
Top Bottom