Habari wana janvi?
Natumai muwazima wa Afya
Siku ya jana ni majanga week end yangu imechafua akili yangu.
Jana nilipata kodi ya kuenda mtende kuwapeleka vijana ktk day out kwa kweli kulikua kizuri sana watu 90 walioenda hio safari wakiwa wanawake 50 na wanaume 40 gari yng ilibeba wanawake 30 na gari nyengine zilikua mchanganyiko.
Licha ya kua gari yangu ilibeba wanawake watupu ila nilikua mpweke kwa kuhofu kuomba kampani kwa wanawake hao kua ni micharuko.
Nilipofika nilijibanisha pembeni kuwangalia wanawake wakivyovaa vibaya na kila 1 akiwa na vituko vyake.
Watu walivamia pombe kali kila 1 akawa anahitaji msaada wa kubebwa wasichana walizidi kua mizoga kwa pombe za bure watu walicheza na kugegedana bila ya nidhamu.
Jambo la kusikitisha ni mwanamke 1 kuzama baharini baada ya kuamua kuenda kujitia maji pwani kwa kupunguza ukali wa pole.
Machungu na sherehe iligeuka kua kilio.
Vijana starehe zina mwisho tuweni makini hebu fikiri mtu unaenda kwa mungu na hali kama hio makazi yako yatakuwaje?