JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,112
- 3,536
Salamu wanajamvi!
Ndivyo unavyo weza kusema. Amani ya Tanzania inalindwa na wapinzani. Uvumilivu wa wapinzani usio na kikomo ndio nguzo kuu ya amani tuliyo nayo sasa. Kimsingi wapinzani wameheshimu misingi ya kuvumiliana na kuheshimiana na wakati mwingine kupisha shari.
Ukiangalia upande mwingine wa shilingi utaona kuwa CCM ni kama wameichoka amani. Vitendo vyao vimethibitisha hilo pasipo shaka.Nitatoa mifano kadhaa kuthibitisha hilo.
Katika vikao halali CUF walimvua uanachama mwanachama wao Habibu Mnyaa. Msajili wa vyama ana taarifa zote kuhusu kuvuliwa uanachama wa CUF Habibu Mnyaa. Lakini pamoja na yote hayo CCM kwa kumtumia mtu wao kutoka tume ya uchaguzi, Mnyaa ameruhusiwa kugombea ubunge wa EALA bila idhini ya katibu mkuu wa CUF ! Huku siyo kutafuta ugomvi?
Kiongozi unapo wataka wanachama na viongozi wa CCM wasiwajulie hali wapinzani na kwamba kufanya hivyo ni kukisaliti chama, Je, na viongozi wa vyama vya upinzani wakiwahubiria hivyo wanachama wao , nini mstakabali wa umoja na amani yetu?
Leo CCM wanataka kupanga safu ya viongozi wao ndani ya CHADEMA, mamlaka hiyo wanaipata wapi? Kama viongozi hawa heshimu kanuni, taratibu na sheria maana yake ni kwamba wameichoka amani. Jana Maalim Seifu Sharifu Hamadi amenukuliwa akisema anazo taarifa zisizo na mashaka kuwa kiongozi wa RITA ameitwa huko juu kupewa maelekezo ili aifute bodi mpya iliyo sajiliwa na CUF, Je, huko siyo kuvuruga amani? Maalim amesema uvumilivu umekwisha, hatakubali kutiwa vidole machoni tena, nini hatima ya ubabe na matumizi mabaya ya taasisi zetu?
Kumtumia Lipumba kuivuruga CUF kupitia msajili wa vyama ni kosa na kwa mtazamo wangu kama CUF wasingekuwa wavumilivu na kuiamini mahakama leo hii tungekuwa tunazungumza mambo mengine kabisa. kwa sasa Nchi hii CCM na UPINZANI wapo nusu kwa nusu, kwahiyo tuwe makini na kauli zetu tunapo fanya siasa. Polisi na jeshi hawalindi amani, amani ya kweli hulindwa na wananchi.
Sasa hivi kwa hakika amani ya Nchi wanao ienzi na kuiendeleza kwa vitendo ni wapinzani.Ni wavumilivu na wanaitakia mema Nchi yetu. Msajili wa vyama nadhani ima hajitambui au hajui wajibu wake. CCM wakifukuza wanachama wao anaheshimu uamuzi wao, CUF wakiwafukuza wanachama wasio fuata kanuni, taratibu na sheria, yeye ana warudisha!! Haitakii mema Nchi hii. Kwani vyama vinapo wapa uanachama msajili anahusika wapi?
Kivitendo CCM wameichoka amani ila kinadharia wanadhani wanaienzi amani.Tukio la kuvamia kituo cha radio na television na mitutu ya bunduki kwao wao ni dogo kwakuwa mhusika ni wa kwao! Taratibu tunaichoka amani.