Kivipi unaweza kujizuia na mihemko

Zogoo da khama

JF-Expert Member
May 20, 2013
623
582
Amani na iwe kwenu

Wana bodi kwa kipindi kifupi cha Jan - Feb nimeshuhudia matukio 3 ya kufedhehesha ndani ya daladala.

La awali tukiwa mdani ya basi toka Kimara kuja Posta kufika Mapipa dada analalamika jamaa anambana sana, kila akijinasua, jamaa hampi nafasi lugha chafu zinatawala, dada anaomba pooo! Kaka anaachia bodi Jangwani safari inaendelea.

La pili jamaa alijiandaa kwani hakufunga zipi na alivaa rambo kuzuia uchafuzi wa mazingira, shati hakuchomekea, tunapofika Akiba dada anamkunjaa jamaa huku akimwamuru afunge zipu yake, bado anashangaa anapokea makofi toka kwa mshangazi kulikoni jibu hivi mkoje dudu lake kavalisha rambo ananiletea, wanawake wote hao bado unafanya mambo ya ajabu, duu hii tatizo sasa.

Leo tuko Baruti foleni ya Ubungo ishaanza denti hatulii utafikili amekanyaga moto, tunafika Ubungo maji dada yamemshinda anarusha ngumi, vipi tena nikome shenzi wee, amefanyaje? Kwani hamuoni! Kivipi kila nikisogea ananiletea nikalishika nikamfinya bado anakuja, anafikili mi malaya.

We denti huna adabu shuka haraka hapana nilikua naangalia pesa zangu alitaka kuniibia, unasoma wapi oooh chuo cha electronics mmmh kila mtu anatafsili yake dada akashuka Shekilango denti Manzese Darajani.

Fedheha ilioje ni kweli mtu anashindwa kujizuia tamaa yake? Inakuwaje na ni mhemko wa kiwango gani hadi kufanya maandalizi ya kuvaa rambo ukajibamize kwenye makalio ya wadada?

Ni kujiendekeza au ni mzuka umebanda, tujadili.
 
Back
Top Bottom