Kiu ya Kumtafuta Mungu kwa bidii

Kiu ya Kumtafuta Mungu kwa bidii

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,118
Reaction score
1,565
Isa 26:9 SUV
[9] Kwa nafsi yangu nimekutamani wakati wa usiku; Naam, kwa nafsi yangu ndani yangu nitakutafuta mapema; Maana hukumu zako zikiwapo duniani, Watu wakaao duniani hujifunza haki.

Sio ajabu ukiwa unapitia katika hali ya majaribu makali, ile kiu yako ya maombi, kusoma neno, kuhudhuria ibada kanisani, isiwepo kabisa kwako.

Hizo ni nyakati ngumu, sio ajabu mtu akiwa anapitia katika hali njema, kila kitu kipo sawa kwake, anaweza kupoteza ile kiu ya ndani na kuwa bize na mambo yake binafsi aliyobarikiwa na Mungu.

Tukisoma andiko la msingi hapo juu, tunaona kiu ya mtu aliyekuwa anamtafuta Mungu kwa bidii, hasa wakati wa usiku wa manane, wakati ambapo kuna utulivu mkubwa.

Ndugu huyu alionyesha wazi ile kiu yake ya ndani ya kumkaribia Mungu wake, si kwa mwili peke yake, alihitaji kuishibisha nafsi yake, ambayo ni kitu cha ndani kabisa cha mtu.

Usiku wa manane au wa giza unawakilisha nyakati za upweke, changamoto, au tafakari ya kina. Hapa mtu anakuwa hamtafuti Mungu tu amsaidie, au kuzungumza naye juu ya jambo zito analopitia au analotaka atendewe, anamtafuta kwa sababu ya upendo wa kweli alionao.

Tunaweza tukawa na bidii na kibaumbele cha kumkaribia Mungu kila wakati, tukiomba, tukisoma biblia na kutafakari neno lake, hii inatujenga na kuonyesha wazi haja ya yetu ilivyo kubwa kwa Mungu wetu.

Tukimkaribia Mungu hivyo, itaonyesha wazi hatusubiri matatizo yatukumbe ndio tuanze kukumbuka ibada, ndio tuwe watu wa maombi sana, ndio tuanze kutafakari neno lake, hata kabla ya kupatwa na hayo tunakuwa na ukaribu na Mungu wetu.

Kiu ya kujenga uhusiano mzuri na Mungu haisubiri uwe na matatizo, inaweza ikawepo ndani yako kabla ya mabaya hajakufikia, ile bidii kubwa ya kuutafuta uso wa Mungu iwepo wakati wa amani na furaha.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom