mkonowapaka
JF-Expert Member
- Feb 19, 2010
- 1,492
- 772
wadau
niliamu akuuchukua uashaur wenu wa dhati kbs kwa vitendo na leo nawasilisha nilipofikia na changamoto nilizokutana nazo..
nilianza mchakato kwa kwenda Ruaha Mbuyuni mwaka jana october.Sikua na niliemfahamu kule.Nilifanikiwa kufanya mazungumzo na watu kama watatu niliokutana nao pale na bahat mmojawapo alikua tayar kuambatana na mimi kucheki mashamba.Nikalipia heka moja laki 3 ya msimu utakaoanza January yamwaka huu...Kulipia mapema ni muhimu.
Nilianza mchakato mwingine wa mbegu.Nikanunua mbegu.Ikahifadhiwa.Ikaoteshwa january.
Mbegu ilihitaji uangaliz wa karibu ikiwemo kunyeshea na kung'olea..bahat mbaya niliyemweka hakuwa siriaz.Mbegu ikajaa majani.haikufaa tena....nikapoteza laki 4
nikaumiza kichwa nikatafuta mbegu za haraka ambazo zimeishakuota.Nikapata.Nikalima.Nikaandaa majaluba.Nikaotesha.
KIjana niliyemweka hakua siriaz sana.akanitia majangani.
Sasa kitunguu kinaendelea vema na ninatarajia kukivuna mwezi ujao mapema sana............
wadau mliopo hapa nipeni bei za sokoni nimefanya research Buguruni gunia ni kama 120,000...au kama tunaweza fanya biashara niPM..mzigo upo shambani pale ruaha mjini kbs pembeni y amto
natarajia magunia kati ya 30 na 40......kwa hekari,kadirio la chini
Vitunguu vinachukua muda gani kuvuna?
Around 5 months
haki ya nani umeniwahi
Mungu akipenda muhimu mwingine tutakuwa wote.
Naomba uniambie kwa kuwa shamba la eka moja la vitunguu
nijipange kuwa na shilingi ngapi, daaaaah naonaje wivu jamani.
Homie, ukianza kusaka shamba unitonye ili tuunganishe nguvu.Seriously!
Shamba unataka maeneo gani?
pale ruaha mbuyuni
nimeambiwa ndiyo maeneo ya vitunguu.
Mafanikio kwenye kilimo cha biashara ni usimamizi wako
Kiongozi hii ni general formula kwa investment yoyote, it does not matter how good a business idea is. What matters is the way you execute it. Unaweza ukawa na business ambayo ni common sana, ila ukatoka kwa vile tu the way unavyoikomalia inakufanya uwe outstanding.Mafanikio kwenye kilimo cha biashara ni usimamizi wako
Hongera.mi last yr niliacha kaz nikaingia kichwakichwa kulima tomato nimepoteza 8ml kwa kutokuwa na elim ya kutosha.