Kituko cha Askari wetu na Uonevu

bnhai

JF-Expert Member
Jul 12, 2009
2,824
2,381
Juzi nilikuwa ninapita barabara ya Mandela, Dar es salaam. Foleni ilikuwa kubwa sana majira ya saa 6-7. Nilivyofika maeneo ya Tabata nikaamua kupita ile njia ya kushoto nikatokee Msimbazi Centre. Bahati mbaya, kushoto kwangu kulikuwa na daladala mbili zimeziba njia na kuacha upenyo mdogo.
Ghafla ikatokea pikipiki ya askari polisi plate number PT 3433 na nyingine ya raia zikitokea pande tofauti na wote wakiwaza kupita ule upenyo. Nusura wagongane. Waligusana kidogo kwa kuwa wote walijitahidi kufunga brake. Wale askari kwenye PT, yule wa nyuma aliruka ghafla na kuikalia ile "bodaboda" na kutaka kuanza kuiendesha. Akamsukuma huko yule raia aliyekuwa ametaharuki na kuanza kutaka kuondoka na ile pikipiki. Swali la kujiuliza, kwanini unyanyasaji ule mbele ya raia?
Kama ni ajali (kama kweli ilikuwepo), kwanini taratibu zisifuate? Kwanini waliamua kuvamia chombo cha raia yule? Kuna tatizo kufuata sheria au wao ni kukomoana tu?
 
Unajua kiongozi, UZALENDO wa kweli hauna mipaka ila wenye mamlaka huwalazimisha wananchi kuwa na mipaka kwa kauli na matendo yao.
 
Back
Top Bottom