Dada Evarm Pole, nikupongeze kwa kujali ujauzito wako(kutoa taarifa/kuulizia ushauri mapema mara tu baada ya maumivu).
Kama ni mimba ya pili na kuendelea(tunge/ningependa kujua) tofauti ya mimba hii na ile iliyopita, lakini kama ni mimba ya kwanza ni vizuri kutambua maumivu yanaelekea upande wowote? Je, yanapungua kutokana na mkao wowote? Je, ulijigonga tumboni eneo la kiunoni?
Pamoja na maswali hayo ningependa kusema kuwa. Maumivu eneo linalozunguka kitovu ni kitu cha kawaida(HASA mimba unapoanza kukua), ..hii ni kutokana na msukumo/mgandamizo(pressure) ya mtoto anapokuwa anapozidi kukua kwani ni katika kitovu ndipo mishipa hii ya damu inayotumika kumpatia mtoto aliye tumboni(tumbo la uzazi) virutubisho yaani(chakula, hewa, n.k).
Hivyo maumivu yanaweza kuhisiwa mjamzito anapoinama, mimba inapozidi kukua na wakati fulani mtoto akiwa anacheza. Hata hivyo maumivu haya hupungua(huwa yanakuja na kupotea), ni vizuri kupumzika, kupunguza kufanya kazi nzito.
Iwapo maumivu yatazidi, kutokupungua, n.k ni vyema kufika katika Kituo cha Afya(Kwa kuwa uko mbali na hospitali) kwa uchunguzi kwani pamoja na ujauzito maumivu ya tumbo(kitovuni) yanaweza kusababishwa na mambo mengine pia.