Uchaguzi 2020 Kitila Mkumbo hili la kukosekana maji eneo Mbezi Makabe na viunga vyake sio zuri sana kwako linakutia doa

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,896
22,664
Pamoja mimi ni mwanaccm na mpigakura wako kama walivyowapigakura wengi wanao tegemea kukupigia kura kwa kuwa nilijiandikisha eneo la Kimara nilikokuwa naishi hivyo kuwa msikivu na ulitendee kazi jambo hili kwa kuwa pia wewe ni member mwenzetu humu jukwaaani.

Ni wiki ya pili sasa Wananchi wa eneo tajwa wanalalamika kuhusu kukatika kwa maji bila majibu , eneo la mbezi makabe ni eneo kubwa na lina wanachi wengi ambao wamekosa huduma hii muhimu,nilichogundua wala hawaisemi DAWASCO wanakugaja wewe labda kwa kuwa unagombea ubunge pia.

Hapo Wizarani unao maofsa wengi wa kushuglikia haya" watume haraka"wawakanye hao DAWASCO waache mchezo hasa kipindi hiki tunachoelekea kwenye jambo letu muhimu wasituahatibie shugli.

Wiki mbili ya kukosa maji sio mchezo kama ni hujma tujue bwana Mtemvu asije kukosa jimbo kwa jambo la uzembe.

CC Kitila Mkumbo ,katibu mkuu wizara ya maji na mgombea jimbo la ubungo.

USSR
 
Back
Top Bottom